NEMC: Msako wa wapiga kelele uko pale pale

NEMC wakazie hapo hapo Kuna baa nyingi hakuna kelele na watu wanajaa wenye mabaa wafate sheria
 
Wengine wanakunywa kwa sababu kuna bendi au mziki

Upo kwa ajili ya ligi mkuu na ubishi wa kiwaki. Mziki sio lazima kelele ziwe juu kuzidi viwango mbona kila kitu kipo wazi sheria nazo zinafafanua viwango vizuri kabisa. Chalamila anaongea kama tahira. Hakuna aliyekataza mziki wala kelele. Lakini wamekata kuzidi viwango na sheria zipo sio mtu kalopoka tu Kama yeye tahira maandazi
 
afadhali tarehe 28 nemc walipumua vizuri na watu walilala vizuri bila makelele
 
Twendeni na chalamila
Hatuwezi kwenda na Chalamila ambaye anachoangalia ni kuwafurahisha wafanyabiashara na anayetaka kupindisha sheria kwa utashi wake binafsi ,kiongozi mzuri ni yule anayefuata sheria na sio kutumia maoni yake ,makelele yana kero na madhara makubwa lakini yeye hatambui hilo ,hatuwezi kuwa na jamii ya viongozi wanaokanyaga sheria
 
Hakuna anayepangiwa muda ,kinachosimamiwa ni usalama wa mazingira, makelele yamekuwa na madhara makubwa kwa watoto kuwa viziwi na kufariki ,kuleta matatizo ya moyo na imesababisha vifo ,watoto wameshindwa kujisomea ,watu kukosa utulivu na muda wa kupumzika yote haya ni madhara hasi kwa jamii ,sauti ipigwe kwa kiwango kilicho salama kama ambavyo sheria inataka ,tukizingatia biaahara tu tutakuwa na jamii ambayo haina afya na imeathirika ,NEMC inao wajibu kisheria kusimamia uhai wa mazingira na viumbe hai nao wanatekeleza wajibu wao kisheria
 
Hao si ni mambwaa tu yakikaliaa kiti wanaona rahis kucontrol wengne ila akifukuzwaa kazi ndo anajua uhalisia ulivyo
NEMC hawa control wengine bali mazingira ,NEMC wanasimamia na kulinda usalama na ustawi wa mazingira na viumbe hai ,maisha ni zaidi ya fedha bali afya ni jambo la msingi saana ,tena tuwapongeze sana NEMC kwa kutekeleza majukumu yao bila kumuonea mtu haya , wafanyakazi wanao wajibu wa kutekeleza kazi zao kwa kufuata sheria za Nchi na kwa umaksusi hizi za mazingira ,kwanini wamiliki wa ma BAR wasipige mziki ambao hautakuwa kero kwa makazi ya watu ?? Kuna haja gani ya kusumbua walio nyumbani?? Hii haikubaliki NEMC wachape kazi hatutaki makelele
 
Mazingira ya Dar kelele hazikwepeki sababu ya mipango miji mibovu
 
Uendeleee bado tunahitaji kustopisha kabisa hizi zilizidi kelele mlichofanya NEMC nichakupongezwa ila msitishwe na hawa wakina Msukuma ambao wao wanaangalia matumbo yao tu na kulinda biashara zao kazeni pitieni mpaka waseme basi sisi watu wamtaani bado tunawapongeza japo siasa imeingia
 
Umeongea vizuri sana lakini kwa kuwa baadhi ya watanzania hawajui wakitakacho hawatakuelewa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…