NEMC tunawapa maua yenu

Political Jurist

Senior Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
143
Reaction score
120
NEMC TUNAWAPA MAUA YENU.

Pongezi nyingi saana kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa hatua kubwa na nzuri walioanza ya kushughulika na Uchafuzi wa Mazingira hususani Kelele na Mitetemo inayotolewa na Wamiliki wa Nyumba za Starehe.

Ni vigumu watu kuelewa hususani kwa wale ambao hawaishi jirani na maeneo hayo ,kumekuwa na kero kubwa sana ,watoto/wanafunzi kushindwa kujisomea usiku ,imekuwa kero kwa wale wenye wagonjwa kukosa Muda wa kupumzika ,kelele zile zinaongeza uchovu kwani watu watokapo makazini wanakosa au kushindwa kupumzika ,kelele pia zimekuwa changamoto kwa wale wenye matatizo ya Moyo lakini pia kelele hizi zikiachwa zitakuwa na madhara ya Muda mrefu ikiwemo Matatizo ya Masikio na Magonjwa ya Moyo.

NEMC mmeonesha njia ,kumbe watu wanaweza burudika bila kuwakwaza wengine ,Nchi ni yetu sote na ustaarabu ndio jadi yetu ,naamini kuanzia sasa kutakuwa na ustaarabu.

NEMC tunawatia moyo ,simamieni Sheria bila kumuonea mtu ,Burudani na Biashara zifanyike kwa ustaarabu bila kuleta madhara kwenye Afya ya Jamii yetu .Na ili Taifa liwe na maendeleo endelevu linahitaji jamii ya watu wenye afya njema.

Kazi nzuri NEMC tunawapa Maua yenu.

#MazingiraYetu
#UhaiWetu.

 
Haka ni kaupepe tu kanapita NEMC
HAWANA MENO.

MIMI NINGESHAURI WAWE NA SIMU KAMA POLISI AU TAASISI NYINGINE MAENEO YENYE KELELE WAJULISHWE.

Ikiwezekana APP.
 
Maua yenu haya apa๐ŸŒน๐Ÿ’๐Ÿฅ€๐ŸŒท๐ŸŒบ๐ŸŒธ๐Ÿต๏ธ๐ŸŒป๐ŸŒผ๐Ÿ’ฎ
 
NEMC waje na huku maeneo ya nyumbani wafanye yao. Kuna watu bado hawasikii
 
Na makanisani wapunguze saut hasa makanisani ya kilokole
 
Wafike na huko miskitin asubuh mtu umelala zako unaamshwa bila sababu
 
Kwanza nimpongeze saana Mhe waziri na kamati yake kwa kuhahakisha kuwa Mazingira yetu yanakuwa salama. Aidha nawapongeza watendaji wa NEMC. Jamani kulikuwa na makelele ya mabaa Hadi kero. Lakini kwa Sasa naona kimyaaaaaaa. Yaani kumetulia Hadi raha. Hongera saana NEMC.
 
Ila Sumu kuendelea kuuwa watu kwako ruksa?

Nemc iko mfukoni mwa Lake oil.
 
Hata mimi nawapongeza. Ninapofanyia kazi pana Bar na maskani pana Bar pia. Ilikuwa mchana moto usiku moto. Si mchezo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ