NEMC yaitoza Lake Oil faini ya bilioni 3.3 kwa kutozingatia utunzaji wa mazingira

Ok ..wale jamaa hawana haraka . wakijenga wanajenga kweli Pia huduma zao ziko high quality
Ok ..wale jamaa hawana haraka . wakijenga wanajenga kweli Pia huduma zao ziko high quality
Sijapata wasaa nao ila all i need is wese lisiloungua haraka kama ilivyo lake oil! Madala dala na boda boda wote wanakimbilia kule sababu inawalipa 😅😅😅😅😅 huwezi kuta dala dala anajaza wese Total
 
Dah kuna kituo cha mafuta mwanza nimekisahau jina kipo geti la nyumba la kuingia Rock City mall aisee ni kikali balaaa
 
Vituo hivyo inabidi vibomolewe! Sio fine tu.Upuuzi mtupu. Kuna kituo wamejenga maeneo ya Victoria. Hakifai kua pale.
 
umeongea point sana.. kuna issue ya branding halafu kuna issue ya ubora wa mafuta... watu wanadhani masheli yaliyorembeka vizuri ndo yana mafuta mazuri kitu ambacho sio
 
😀😀comedy, watendaji wa ardhi mipango miji, halmashauri wamekalia kupokea bahasha tu, huku mtu anajenga, kuna kituo cha Lakeoil Mbagala, AISEE! Kipewe tuzo, kiko sehemu HATARISHI hatuombei ila kikilipuuuukaaah!

Tutakuja kulaumiana kwanini hawakuambiwa wakivunje. Faini haitoshi vingine wavunje, Al-Saedy Morogoro kajenga kituo ukuta unapakana na nyumba, Abood kajenga kituo shule ya Msingi Msamvu haiko mbali, basi tuzidi kumtegemea Mungu.

Everyday is Saturday................................😎
 
Kabla Kituo cha Mafuta hakijajengwa, kuna vibali lazima mtu uwe navyo, na cha kwanza kabisa inakuaga EIA (Environmental Impact Assessment) ambacho hao hao NEMC ndio wanakitoa.

Sasa kweli mtu ajenge Letrol station bila kibali iko?
 
Nimeona mpaka katikati ya makazi wamejenga aisee.. Ila NEMC walikuwa wapi? Vibali vya ujenzi vilitokaje bila kuwashirikisha? Je baada ya kulipa faini watavunja au wataendelea na biashara?
Biashara ya kujenga Fuel pump sio kama hivyo kaka, sheria inataka usiendeleze eneo hata kufyeka bila kupata kibali, sasa ukute walishapata eneo wakaanza matengenezo madogo ndipo hapo NEMC wanakula 20M kwa kila kituo
Sio kwamba biashara haitaendelea, itaendelea ila hiyo sheria ni ya moto usipime.
 
Nimeona mpaka katikati ya makazi wamejenga aisee.. Ila NEMC walikuwa wapi? Vibali vya ujenzi vilitokaje bila kuwashirikisha? Je baada ya kulipa faini watavunja au wataendelea na biashara?
Wakishalipa basi watasajiliwa rasmi Kama wadau wakubwa wa maendeleo
 
Industrial espionage na Industrial sabotage ni vitu viwili vinavyofanya kazi pamoja,kama vile uchawi na majini huwa haviachani sana,ukiona mtu au Kampuni inapigwa faini ya mabilioni kunakuwa na maswali ya kufikirisha.
 
lake oil hawatalipa fine na wataendelea kufanya biashara zao Nemc hawajui hiyo biashara ni ya mzee Mh yumo humo utaona hii habari itakuwa kimyaa wala hutoisikia tena ya fine au ya kufunga vituo
 
UKITAKA KUJENGA LAZIMA UPATE KIBALI ANAYEKUPA KIIBALI LAZIMA AWE AMEJIRIDHISHA KUWA UMEKIDHI VIGEZO VYOTE SASA BASI LAKE OIL MSILIPE ANAYETAKIWA KULIPA NI MKURUGENZI ALIYETOA KIBALI CHA KUJENGA KITUO CHA MAFUTA
 
UKITAKA KUJENGA LAZIMA UPATE KIBALI ANAYEKUPA KIIBALI LAZIMA AWE AMEJIRIDHISHA KUWA UMEKIDHI VIGEZO VYOTE SASA BASI LAKE OIL MSILIPE ANAYETAKIWA KULIPA NI MKURUGENZI ALIYETOA KIBALI CHA KUJENGA KITUO CHA MAFUTA
Kibali cha kujenga na EIA report ni vitu viwili tofauti

Tambua EIA ina kagua athari za maradi husika ktk mazingira sasa mbali na EIA kuna ukaguzi mwingine hufanyika baada ya mradi kuamza kazi kwa kipindi fulani endapo ikionekana una viashiria vya uchafuzi wa mazingira kwa kimombo wanasema Environmental audit (EA)

Sasa ikibainika mradi unachafua mazingira hapo lazima ulipe faini ya fedha

EIA hufanyika kabla ya mradi kuanza
 
Kwaiyo nemc wanaona wivu vituo vya mafuta kuenea maeneo mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…