Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa elimu na kusisitiza suala zima la utunzaji na usimamizi wa Mazingira katika soko kuu la Kariakoo litakalokuwa linafanya kazi kwa masaa 24.
Akizungumza katika Maonesho ya uzinduzi wa biashara ya saa 24 katika Soko kuu la Kimataifa Kariakoo leo tarehe 27 Februari 2025, Meneja wa Kanda ya Temeke Bw. Abel Sembeka amewataka wafanyabiashara na wageni kuacha tabia ya kutupa taka ovyo katika maeneo yasiyo rasmi huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kuzingatia uchumi mzunguko (circular economy) kwa kutenganisha taka ngumu kuanzia kwenye chanzo ili kuweza kurejeleza taka kwa ajili ya kuweka Mazingira safi na salama.
Meneja Abel Sembeka ametolea ufafanuzi juhudi za NEMC kushirikiana na Mamlaka husika kama DAWASA na Halmashauri za Jiji la Dar es salaam kudhibiti utiririshaji wa maji taka katika maeneo yote ya Soko na nje ya Soko ili kuhakikisha mazingira ni rafiki kwa wageni watakaotembelea Soko kupata huduma mbalimbali.
NEMC inawakaribisha wadau wote wa Mazingira kutembelea Banda lake ili kupata elimu ya usimamizi wa mazingira katika maonesho ya uzinduzi wa biashara ya saa 24 katika Soko kuu la Kariakoo kuanzia tarehe 26 hadi 27 Februari 2025.
Mbali na NEMC wengine walioshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na BRELA, TAN TRADE, TARURA TRA, NSSF, WMA, DAWASA, TIC, TANESCO, NMB,CRDB STRATEGIES INSURANCE, n.k.