Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Ni gumu sana kulielezea au kulifahamu. Kila mtu ana tafsiri yake juu ya maendeleo.
Japan imeendelea. Japan ina uwezo mkubwa wa kutengeneza magari na wananchi wake wana kiwango cha juu cha hali ya maisha. Pia wana barabara za juu kwa juu. Lakini Japan haina bomu la nuklia.
Marekani imeendelea. Hawa ingawaje hawana uwezo mkubwa wa kutengeneza magari kama Japan, na wala barabara zao si nzuri kama za Japan, lakini pia wananchi wake wana kiwango cha juu cha maisha. Marekani ina mabomu ya nuklia, ambayo pia yanaonesha maendeleo ya kiufundi.
Na ndiyo hivyo China, Australia, Ujerumani na karibuni bara lote la Ulaya.
India. India haijaendelea na bado ni ulimwengu wa tatu. Lakini India ina GDP ya zaidi ya dola trilioni 3 hata kushinda Uingereza, Ufaransa au Switzerland. Inatengeneza magari, ina nuklia! Ila wananchi wake hawana kiwango cha juu cha hali ya maisha.
Natumaini sasa umejua maendeleo hasa ni nini. Kwa mifano hiyo iliyopita, kigezo cha maendeleo ni maendeleo ya watu, na wala si vitu, hata kama vitu hivyo ni majengo mazuri ya shule, zahanati, na barabara za juu kwa juu.
Hawa wanaozidisha tozo wanatuambia wanfanya hivyo kwa kuleta maendeleo! Watanzania wengi hawawezi kula milo bora (balanced) mitatu kwa siku.
Kuchukua fedha kutoka kwa huyu ili ukajenge barabara inakuwa ni maendeleo? Ya nani?
Waziri atajibu 'tukijenga barabara, zahanati, shule, soko.....kutokana na fedha yake ya milo mitatu, ndipo ataendelea'. Sidhani wengi wataridhishwa na mantiki hii.
Laiti tozo zingewalenga tu wale wenye uwezo wa milo mitatu kwa siku. Nadhani wote tungetunga mashairi ya kuisifu tozo. Ama tozo kwa mtindo wa mtego wa panya (aingia aliyedonoa na asiye) ni vigumu kuitetea!