Neno "Hongera" linavyotumika kupotosha jamii.

Neno "Hongera" linavyotumika kupotosha jamii.

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Aghalabu imekuwa ni kawaida sana kwa watumiaji wa simu za kikononi kupokea ujumbe "HONGERA" sehemu isipostahili kwa mfano;
1, Ukijiunga kifurushi cha kupiga simu utapokea neno "Hongera umefanikiwa kujiunga minikabang" sasa hongera inakujaje na sijaungwa kwa bahati mbaya wala bahati nasibu?
2, Makampuni ya kubet sasa ndio imekuwa kero kupita maelezo na sijajua huyo anayewapa namba zetu ni nani ? Utaona mesegi "Hongera namba yako imechaguliwa kucheza DAKAPESA jaribu bahati yako" Yani kunitapeli mnatoa hongera?

Watanzania na mitandao ya simu tupende kujiongeza sio kila neno linalotafsirika kiingereza linapaswa kutumika kila mahala toeni hongera mtu akishinda bahati nasibu msitoe hongera mtu akinunua bidhaa zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna wale wakijua mkeo amejifungua, wanakuja na midomo yao wazi wakisema hongera wakati hawajui ulitumia siku ngapi wakati mbuzi kagoma kwenda.
 
kuna wale wakijua mkeo amejifungua, wanakuja na midomo yao wazi wakisema hongera wakati hawajui ulitumia siku ngapi wakati mbuzi kagoma kwenda.
Haha
images(49).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti "hongera umefanikiwa kujiunga na kifurushi cha halichachi cha sh elfu moja"
 
Back
Top Bottom