Neno 'Inc' lina maana gani kibiashara?

mnyalukoloh

Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
74
Reaction score
31
Habari wadau.

Kama nilivyoandika kwenye kichwa hapo juu naomba kufahamishwa maana neno inc kama lilivyotumika kwenye kampuni ya Apple (Apple inc) na sehemu zingine.
 
Ni Inc ambayo kwa kirefu ni Incorporated company
Umeandika wino (ink) hapo umewachanganya wachangiaji


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ni Inc ambayo kwa kirefu ni Incorporated company
Umeandika wino (ink) hapo umewachanganya wachangiaji


Sent from my iPhone using Tapatalk

Kwa mfano umeanzisha kampuni na kukaribisha watu wawekeze na kuwa directors na kuwa na nguvu katika maamuzi ya nini cha kufanya katika kampuni hiyo Inakuwa incorporate company
Nadhani hivyo na wataalamu watakufafanulia zaidi


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mkuu kuna form tatu za biashara yaani sole propieter, partnership na Limited liability company.

Hii form ya juu ya company biashara inakuwa separate entity na wamiliki na liability zinaishia kwenye investment uliyowekeza kwenye biashara na haifiki kwenye mali binafsi.

Limited liability company zinapokuwa more advanced with predictable management structure zinaitwa Incorporated company ( Inc). Inc mara nyingi zinaoperate across nations, zina wamiliki wengi ambao hawapo kwenye day to day operations unaweza kuta inasimamiwa na Managing Director, president,CEO or the like maana niuamuzi tuu. Pia inategemea na inchi zilipokuwa incorparated lakini zinatakiwa kuwa Annual general meeting( mkutano mkuu wa wanahisa) na kutoa directors report tofauti na kampuni za kawaida za mfano Kiparamoto Food co ltd, pengine wamiliki wawili au wachache au mmoja ndio kila kitu.

Nadhani ukiona neno inc kwenye makampuni makubwa ya biashara hutashangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ulewa wangu inc kirefu chake ni incorporated.

Ni utaratibu wa kisheria ambao unaifanya kampuni kuwa na mali zake.

Yaani huu ni utaratibu unaotafautisha mali za wawekezaji na mali za kampuni.

Hivyo basi linapokuja swala la tax basi pesa za wawekezaji hazitoguswa isipokuwa faida ya kampuni ndio itakatwa kodi.

Mfano kampuni ikiwa ina deni kubwa kiasi cha kufilisika basi mali za kampuni ndizo zitahusika na sio pesa za wawekezaji.

Incorporated companied huwa zina utaratibu wa kuuza shares na wamiliki wanakuwa wengi na kampuni inaweza ikaendelea tu hata kama muanzilishi amekufa au ameuza shares.

Pia inc companies huwa na body of directors ambao ndio shareholders wenye nguvu ya kufanya maamuzi mfano kuajili ceo nk.
 
na minimum namba of directors ni wa ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…