Neno limited(ukomo) linatumika mwishoni mwa jina la kampuni kuonyesha kwamba madeni ya wanahisa hayatazidi thamani ya hisa za wanahisa( the liability of members of the company are limited to a state amount) .Hasa kampuni inapofilisika kama itashindwa kulipa madeni ya creditors ninyi wanahisa(shareholders) hamtalazimika kutumia Mali zenu binafsi kuwalipa wanaoidai kampuni. Tofauti na partnership(ubia) na sole proprietorship(biashara ya MTU mmoja) ni kwamba kampuni inafahamika kama MTU(a company is a corporate body, I.e it is created under law and has an entity of its own, quite separate from the members that comprise it. This is a very important difference and is in fact the main reason for the popularity of this form of ownership). Kwa kuongezea in kwamba mahakama inaitambua kampuni kama MTU kisheria ambaye anaweza kuingia mikataba, akashitaki na akashitakiwa, akakopa, akamiliki Mali na kufanya chochote ambacho ndicho kilichokusudiwa wakati Wa kuanzisha kampuni. Partnership and sole traders hawatumii ltd kwa sababu huwezi kumtenganisha mmliki na biashara take na kwa hiyo biashara ikifilisika atalazikia kutumia Mali zake binafsi ili awalipe wanaoidai biashara yake. Samahani kwa mahali popote ambacho sijaeleweka au sijaweka maelezo vizuri mkuu ila bila shaka utapata mwanga kidogo.