General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,064
Umefafanua vyema.Kuna wakati fulani , vijana wa CHADEMA maarufu kama Vijana wa Ufipani hasa Ben Saa Nane pamoja na Malisa G,walikuwa moto sana katika kuitetea Chama na mustakabali wake mitandaoni. Hii ilihusisha Facebook pamoja na hapa Jamii Forums.
Hii iliididimiza sana CCM hivyo kuamua kuunda tawi la mitandaoni lenye kuitetea na kuitangaza Chama pamoja na kujibu hoja za vijana wa CHADEMA. Hii ni pamoja na kuiponda CHADEMA pamoja na harakati zake za kisiasa.
Kundi hili la vijana walitakiwa kuwa na Smart phone au komputa mpakato 'laptop'.
CCM Ilienda mbali zaidi ikiwa ni pamoja na kuwanunulia vocha za Buku kila siku ili kuwawezesha kujiunga na Vifurushi 'Bundles' ili kufanikisha kazi zao ipasavyo.
Kwa hiyo Vijana hawa walikuwa wakipewa Tsh 7000 kwa wiki kwa ajili ya Vifurushi. Na walikuwa wakipewa Kwenye ofisi zao za Dar es Salaam zilizopo Lumumba.
Ndipo humu JF wakaamua kuwapachika jina maarufu sana Lumumba 7000 au Lumumba Buku saba..
Hii iliwazalisha vijana kama Lizaboni, Stroke pamoja na wengine.
Hiyo ndiyo maana na historia fupi ya Lumumba Buku Saba.
Lakini bahati mbaya sana Lumumba Buku Saba wamekuwa wepesi sana Vichwani. Hoja zao hazina mantiki kulinganisha na wenzao
Kuna wakati fulani , vijana wa CHADEMA maarufu kama Vijana wa Ufipani hasa Ben Saa Nane pamoja na Malisa G,walikuwa moto sana katika kuitetea Chama na mustakabali wake mitandaoni. Hii ilihusisha Facebook pamoja na hapa Jamii Forums.