LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Kwa muda mrefu sasa vyombo vya habari nchini Tanzania, vimekuwa vikiwataja ndugu zetu walio zaliwa na changamoto ya ukosefu wa melanini mwilini na uono hafifu " ALBINO " kama "MA-ALBINO" hususani pale wanapo kuwa wanawazungumzia kwa wingi wao. Kwa mfano utasikia redioni,. ama kusoma kwenye gazeti sentensi kama " MAALBINO WAUWAWA KIKATILI SHINYANGA "...MAALBINO WAPEWA MSAADA WA MAFUTA MAALUMU KWA AJILI YA NGOZI ZAO JIJINI ARUSHA " ama " MAALBINO WAOMBA SERIKALI IWALINDE ".
Ndugu watanzania wenzangu, nikiwa kama mtumiaji wa lugha ya kiswahili kwa zaidi ya miaka 20, naona neno "MA-ALBINO " sio neno zuri kutumika kwa ndugu zetu albino.... Mara nyingi kama sio mara zote , kiambishi "MA" kinapotumika kabla ya jina, huwa kinabeba mtazamo hasi " NEGATIVE ATTITUDE " juu ya jina husika. Mfano neno " MA-JAMBAZI, MA-FISADI, MA- MAGAIDI, MA-SHOGA, MA- JANGILI n;k "...... Ninapendekeza jina linalopaswa kutumika kuwaelezea ndugu zetu ALBINO hata kama wapo wengi ni hilo hilo ALBINO ( I mean jina ALBINO litumike kwa umoja na wingi pia ) kwa mfano badala ya kusema " MA-ALBINO WAPEWA SEMINA YA NAMNA YA KUTUMIA MAFUTA MAALUMU " itamkwe ' ALBINO WAPEWA SEMINA........" nadhani sentensi ya pili, haina unyanyapaa kama sentensi ya kwanza...
NIMECHUKUA HATUA GANI :
Mimi kwa kushirkiana na taasisi moja isiyokuwa ya kiserikali inayo jihusisha na maendeleo ya jamii na haki za binadamu, nimewaandikia barua Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ( TUKI ), Baraza la Kiswahili Tanzania ( BAKITA ), kuwataka ( sio kuwaomba ) washirikiane na mimi katika kuanzisha mchakato wa kufuta matumizi ya neno MA -ALBINO.. Katika mchakato huu tutashirikiana na vyombo vya habari ,taasisi za kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.( Nimeshawaandikia na LHRC kuwaomba kushirikiana nami katika hili )
MAWAZO, MAONI NA USHAURI WENU NI MUHIMU SANA KWANGU....WAITING TO HEAR FROM YOU SOON "
" There are so many leaders, doctors, teachers, graduates,lawyers e.tc out there, but without a difference, the plan of God is to make you one, with a difference. "