Neno " ma- albino " lipigwe marufuku kutumika.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Kwa muda mrefu sasa vyombo vya habari nchini Tanzania, vimekuwa vikiwataja ndugu zetu walio zaliwa na changamoto ya ukosefu wa melanini mwilini na uono hafifu " ALBINO " kama "MA-ALBINO" hususani pale wanapo kuwa wanawazungumzia kwa wingi wao. Kwa mfano utasikia redioni,. ama kusoma kwenye gazeti sentensi kama " MAALBINO WAUWAWA KIKATILI SHINYANGA "...MAALBINO WAPEWA MSAADA WA MAFUTA MAALUMU KWA AJILI YA NGOZI ZAO JIJINI ARUSHA " ama " MAALBINO WAOMBA SERIKALI IWALINDE ".
Ndugu watanzania wenzangu, nikiwa kama mtumiaji wa lugha ya kiswahili kwa zaidi ya miaka 20, naona neno "MA-ALBINO " sio neno zuri kutumika kwa ndugu zetu albino.... Mara nyingi kama sio mara zote , kiambishi "MA" kinapotumika kabla ya jina, huwa kinabeba mtazamo hasi " NEGATIVE ATTITUDE " juu ya jina husika. Mfano neno " MA-JAMBAZI, MA-FISADI, MA- MAGAIDI, MA-SHOGA, MA- JANGILI n;k "...... Ninapendekeza jina linalopaswa kutumika kuwaelezea ndugu zetu ALBINO hata kama wapo wengi ni hilo hilo ALBINO ( I mean jina ALBINO litumike kwa umoja na wingi pia ) kwa mfano badala ya kusema " MA-ALBINO WAPEWA SEMINA YA NAMNA YA KUTUMIA MAFUTA MAALUMU " itamkwe ' ALBINO WAPEWA SEMINA........" nadhani sentensi ya pili, haina unyanyapaa kama sentensi ya kwanza...

NIMECHUKUA HATUA GANI :

Mimi kwa kushirkiana na taasisi moja isiyokuwa ya kiserikali inayo jihusisha na maendeleo ya jamii na haki za binadamu, nimewaandikia barua Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ( TUKI ), Baraza la Kiswahili Tanzania ( BAKITA ), kuwataka ( sio kuwaomba ) washirikiane na mimi katika kuanzisha mchakato wa kufuta matumizi ya neno MA -ALBINO.. Katika mchakato huu tutashirikiana na vyombo vya habari ,taasisi za kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.( Nimeshawaandikia na LHRC kuwaomba kushirikiana nami katika hili )

MAWAZO, MAONI NA USHAURI WENU NI MUHIMU SANA KWANGU....WAITING TO HEAR FROM YOU SOON "

" There are so many leaders, doctors, teachers, graduates,lawyers e.tc out there, but without a difference, the plan of God is to make you one, with a difference. "
 
Mkuu kwa kuwa umeomba comments,ningeomba unifafanulie vizuri hapa:

Ikiwa "ma" inaweka negation,vipi ma-penzi,ma-vazi,ma-lezi,ma-kubaliano, nk? Au labda mimi ndio sijakuelewa mkuu?

Nimejaribu kupitia Kamusi ya Kiswahili Sanifu lakini sijapata neno la kiswahili linaloitwa albino.Vipi sasa utuhamasishe kutumia neno albino kama neno sahihi la kiswahili?

Nionavyo mimi tatizo sio jina,kwa sababu hawa ndugu zetu tumekuwa tuiishi nao tangu enzi na enzi bila shida.Matatizo yameanza miaka ya hivi karibuni ambapo wahuni kadhaa walichafua hali ya hewa na hawa ndugu zetu wakaanza kuonekana kama viumbe tofauti.Kumuita tu jina albino hakutarudisha heshima yao ktk jamii,bali jamii kuwatambua kama binadamu wenzetu kama ilivyokuwa tangu zamani bila kujali.

Najua kuna watu wanaingiza hela kwa kubuni tu majina hata bila kuangalia chanzo cha tatizo,ila mkae mkijua mtabadilisha sana majina hadi yale ya kilugha,lakini kama hamtazuia chanzo cha tatizo mimi nawaona nyie wote wasanii tu,hamna lolote.
 
samahani,kwani jina zeruzeru lina ubaya gani??
 
Hili ndilo neno la kiswahili fasaha ambalo tumekuwa tukilitumia miaka nenda rudi bila shida hadi wajasiriamali fulani walipojitokeka na kuanza kutengeneza pesa kwa kubadilisha lugha.Huu ni upuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom