Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Tumezoa kusikia neno "Matukufu" kila yanapotajwa Mapinduzi ya Zanzibar ya January 1964, Jee neno hili, Matukufu, lilitokea wapi na lina maana gani kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na kama ni kuhusu utukufu wa Mapinduzi hayo, Jee Mapinduzi ya Zanzibar yana utukufu gani hadi kustahili kuitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar?!.

Nakiri kupandisha uzi huu, kufuatia mchango wa mwana jf huyu, Maalim
Mohamed Said kwenye uzi
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa .
kuhusiana na neno Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Nawaomba wajuvi wa mambo ya Zanzibar mtujuze, Jee Mapinduzi ya Zanzibar ni Mapinduzi Matukufu, au ni Mapinduzi tuu?!, kama ni Mapinduzi Matukufu, Jee Mapinduzi yele yana utukufu gani?!.

Na nikimsoma Maalim Mohamed Said, amesema kwa mujibu wa Imani ya Dini ya Kiislamu, "Utukufu ni wa Allah pekee!", Jee hili ni kweli kuwa Kiislam neno Utukufu hutumika kwa Allah pekee?!, Jee sasa hawa Waislamu tena Swala tano, tunaowasikia kila siku wakitoa utukufu kwa Mapinduzi, ina maana kila anayeyaita Mapinduzi Matukufu jee anatenda dhambi dhidi ya utukufu wa Allah pekee?!.

Pia kuna maneno Ikulu ni mahali patakatifu!, Bunge Tukufu, hadi Mtukufu rais...inawezekana wote hawa wana kufuru?.

Paskali
 
Kwa Muktadha wa Uislam neno Tukufu ni isiyo na shaka wala makando kando (purified) mf Qur an Tukufu. Hapa Tanzania Kwny Siasa zetu Mwl Nyerere na Ally Hassan Mwnyi waliitwa Watukufu, aliekuja kukataa hilo neno ni Mzee Benjamin Mkapa December 1995 alipokuwa anatangaza Cabinet yake. Kenya ilikuwa huwezi kutaja Jina la Daniel Arap Moi bila ya kutanguliza Mtukufu. Hapa kwetu mpaka leo Si ajabu kusikia "...Mh. Spika kupitia Bunge lako tukufu..."
Kwa Zanzibar Mapinduzi yanaitwa Matukufu kwa wale wanaoyaunga Mkono lakin wasioyaunga Mkono wanasababu zao sio kwa kuwa yanaitwa Matukufu na hata tukilitoa neno tukufu bado yatapingwa tu.
Yanaitwa Matukufu kwanza kwa kuwa yalifanikiwa pia yalirejesha hadhi ya mtu Mweusi Zanzibar n.k
Kwny Siasa za Zamani neno tukufu linaweza kuwa sawa na neno Heshimiwa linalotimika leo japo halimaanishi. Huko Halmashauri ukitamka Jina la Diwani bila ya kuanza na Mh. DIWANI ni kosa kubwa kama kula pesa za ushuru wa soko
 
Pasco tuachie utukufu kwenye mapinduzi uendelee. Tulipata fursa ya kuwaoa waarabu ya bwerere. Huko Lumumba mnayo?
 
Mkuu Pohamba, kwanza asante kwa ufafanuzi kuhusu neno "tukufu", hiyo hii kauli ya huyu jamaa, japo ni Maalim Mohamed Said, kusema kwa kuwa "Utukufu ni wa Allah pekee!" ni maneno ya urongo!. Kiukweli humu jf, tunalishwa urongo mwingi!. Hivyo kumbe ni sahihi kuyaita Mapinduzi Matukufu!. Asante.

Paskali
Update
Mkuu Pohamba, kwanza asante kwa ufafanuzi kuhusu neno "tukufu", hiyo hii kauli ya huyu jamaa, Maalim Mohamed Said, kusema kwa kuwa "Utukufu ni wa Allah pekee!" ni maneno ya urongo!. Kiukweli humu jf, tunalishwa urongo mwingi!. Hivyo kumbe ni sahihi kabisa kuyaita Mapinduzi Matukufu!. Asante.

Paskali
 
Mmmmh mimi sio mtaalamu wa vocaburaries za Mungu, ila najua kuna dhuluma huwa inatokea kwa wazanzibari kuporwa ushindi kwenye kila chaguzi za zanzibar
 
Kwa nini yanaitwa "mapinduzi matukufu"?
Naomba kuelimishwa
ni katika kusaidia tuu!.

Pasco
 
Yanaitwa hivyo kuhalalisha haramu. Kitu kizuri hakihitaji ngazi ya kupandia huwa kinapanda wenyewe. Mapinduzi mbali kufanywa kutoka nje...Okelo ushahidi na pia mapinduzi yakaiondoa Znz katika ramani ya nchi yenye utambulisho Kimataifa na kuwa sehemu ya Tanganyika yenye serikali ya ndani.
Hivyo ili kuyafanya yawe halali basi walofanya hayo wanataja neno hilo kila mara kwenye sherehe zao au sehemu ingine. Na inaoneka hilo neno halikubuniwa na Wazanzibari wenyewe kama hayo mapinduzi yenyewe kwani katika uislam Utukufu ni Wa Allah pekee na inajulikana wazi Wazanzibar 99% ni waislam. Hivyo hizo ni ngano za wakuja
 
Umesahau enzi za mtukufu Rais?! Labda aliyelileta alitafsiri vibaya. Labda wanaojua kiarabu walete lile neno original.
 


Mkuu Nyerere hakuwahi kuitwa mtukufu. Yeye alikuwa ni Mwalimu tuu.......
 
Asante sana. Na mimi nilitaka kumshukia kwa kusema kitu cha uongo. Hakuna mtu aliyechukia kuitwa ''mtukufu'' kama Nyerere. Sina uhakika kama hii walimwita mara baada ya lakini hakuitwa hivyo kwa muda wote niliomsikia akihutubia

Baada ya alikubali kuitwa Baba wa Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…