Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,

Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Halafu wewe unaita mapinduzi haya matukufu haya ni machafuzi.
Mkuu amanij , sio mimi ndiye ninayaita Mapinduzi ya Zanzibar kuwa ni Matukufu, bali hill ndilo rasmi la Mapinduzi ya Zanzibar yanaitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
P
 
Ni upuuzi tu wa wenye mamlaka
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Subiri Bado kidogo tu
 
Mapinduzi haramu yaliyomwaga damu za watu wasio na hatia. Kamwe hayawezi kuwa matukufu.
 
Wewe mambo ya Wazanzibari huwa yanakukereketa kwa nini hasa? Wamekufanya nini baya Wazanzibari? Mbona husemi kitu bunge au rais anapoitwa mtukufu, utukufu wao uko wapi?
 
....Hasaa. Kuna uchaguzi wa mwaka fulani ndugu Paskali (huyu wa humu JF), kupitia Mwajiri wake, ALIMTANGAZA mshindi "halali" wa uchaguzi huo. Walimtoa Baruu.
[emoji28][emoji28][emoji28] Binadamu huwa tunasahau haraka au tunajisahaulisha, pindi maslahi yanapokua hatarini.

Mfano mzuri tu, waangalie viongozi wengi, wwnapofariki wasifu wao unavosomwa... mpenda haki, anaetetea wanyonge, mkarimu, msema kweli, n.k n.k..... ila kiuhalisia wanajua zaidi kama hizo sifa wengine hawana hata chembe.
 
Kwasasa huko visiwani kuna shamrashamra yakuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi.

Wazanzibar wenyewe huyaita “mapinduzi matukufu” je huwa wanamaanidha nini? Ni upi huo utukufu katika hayo Mapinduzi?

NB:
Fursa za Chattle zimehamia Visiwani
Karibu Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
Nakutakia maandalizi mema ya maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…