Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
Ukilemaa mkuu utandawazi unakupitia na wewe unaiga maana ni vitu ambavyo unaanza polepole kutokana na watu wengi kutumia hiyo lugha mwisho wa siku na wewe unaingia.Hivi hili nalo tutalaumu utandawazi kweli? Kwa wakati mwengine naona matumizi ya misamiati hii ni kusudi za mtu binafsi.
Ila kwa mbaali unakuta kuna umahili, mazingira na kujikweza ndani yake mpaka mtu anazungumza hivi. Kwa mfano mtu anapotamka "tangia" badala ya "tangu" ni dhahiri kuna kujibwetesha katika matumiz ya lunga na kukiuka kaida zake.
Kuna sehemu tumekosea na kulazimisha kuongea hizi lugha mpaka kwenye taasisi nyeti, tukianza na bungeni na kwenye vyombo vya habari hili tatizo litaisha maana kabla ya mtu kuzungumza au kuandika habari au kuisoma lazima kuna editor anafanya kazi yake. Hilo ni kosa la upotoshaji kama makosa mengine ila tunaangalia upotoshaji wa mambo ya kisiasa tuduh basi ni ugonjwa wa taifa
Ukilemaa mkuu utandawazi unakupitia na wewe unaiga maana ni vitu ambavyo unaanza polepole kutokana na watu wengi kutumia hiyo lugha mwisho wa siku na wewe unaingia.
si sahihi kabisa...nayoipenda-ga!! sijui asili ya kuweka ga mwishoni mwa neno ilitoka wapi!!!??? mimi mwanzoni nilfikiri wasukuma ndio wanatumia ga kwenye kila neno la kiswahili, kumbe kuna wengine pia???
Ni neno hilo ila ni neno kisarufi
unajua kiswahili au ni mtumiaji wa kiswahili Tihz? Ni mofimu kwenye mazingira fulanifulani sio neno...ziangalie sifa za maneno na uangalie ni aina gani ya neno.
Lakin pia ukumbuke tukizungumzia "ga" tunazungumzia likiwa ndani ya neno fulani hivyo hupata sifa ya kiambishi kutokana na uambishaji wake na mazingira fananifu kama hayo.