Neno "udhalilishaji wa wanawake" linatumika vibaya

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Jumapili njema

Leo nimeamua kuja na hoja kidogo kama nilivyoandika hapo juu asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa hawalitendei haki hilo neno hasa mtandaoni, wamekuwa wakileta tafsiri isiyo sahihi kuhusu udhalilishaji wa wanawake. Nashindwa kujua, je hawajui kweli au la!

Mfano hivi karibuni Mlela alimuacha Ebitoke, cha ajabu celebrities wakike wakaja juu nakumshambulia Mlela eti anawadhalilisha wanawake, eti cos Mlela hawezi kukaa na mwanamke mmoja. Kwani wakati anawatongoza hao wanawake alitumia mabavu au vitisho ili hao wanawake wamkubalie?

Navyojua mimi udhalilishaji wa wanawake maana yake ni kuwafanyia wanawake vitendo viovu bila ridhaa yao; mfano, kubaka, kuwaingilia nyuma ya maumbile bila ridhaa, kumpiga, kuvujisha picha ya faragha bila ridhaa au yeye kujua n.k. Hii ndiyo maana halisi ya udhalilishaji wa wanawake na si vinginevyo.

NAWASILISHA HOJA
 
Udhalili

Udhalilishaji

Udhalili ni hali. Udhalilishaji ni mwenendo wa hiyo hali; Aidha kwa kutenda au kutendewa.

Na udhalili ni kitu/hali ya uchini kabisa yaani ni duni hakina thamani. Hakina thamani kwa maana hakina stahiki ya jema au tija, hakina manufaa. Kama unakitumia ni ilimradi umekitumia tu.

Udhalilishaji ni kuyatenda hayo yanayofafanua maana ya udhalili dhidi ya fulani.

Mapenzi ni siri ya wawili: Ninachoamini laiti Yusuf angelikuwa ni mwenye muonekano wa kawaida haya yasingelitokea. Ikhtilafu inakuja pale mwanaume ukiwa na sharafa yenye kupendeza machoni mwa watu kuliko mwanamke uliyenaye, na mbaya zaidi mkatengana na kidume ukawa na mwanamke mwengine.

Utarushiwa maneno na jopo la wanawake na laiti hayo maneno yangelikuwa mkuki yangelimtia jeraha na kovu huyo mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…