Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzang,
Leo nawaletea kisa cha ndugu yetu Nestory Bingwa, ambae ni mjomba wangu kabisa wa kuzaliwa na mama yangu mzazi.
Huyu bingwa ni miongoni mwa watanzania wachache sana waliowahi kuingia nchi hii kitambo sana, kabla hata muasisi wa taifa hili hajaachiwa huru.
Baada ya kuishi Kaburu kwa takriban miaka nane, toka mwaka 89 hadi 96, bingwa alirudi nyumban kusalimia, na mara ghafla akatokomea katika kijiji fulan kilichopo huko Sumbawanga mkoani Rukwa bila kumuaga mtu yoyote.
Alikaa huko Sumbawanga miezi mitatu, kisha akarudi Dar na kudai kwamba yeye sasa ni mganga mwenye kuweza kutibu watu.
Kila mtu katika familia yetu alishangaa sana. Kwa sababu katika familia zetu zote mbili upande wa mama, na upande wa baba hakunaga mganga wa kienyeji. Sasa huyu mwamba uganga ameupataje, au amerithishwa na nani?
jibu alikuwa nalo mwenyewe.
Baada ya mishe ya hapa na pale kushughulikia ganda la usafiri, bingwa akarudia tena kiwanja chake alichozoea kama kawaida.
Mara tukaanza kusikia kuwa bingwa ni mganga, na anatibu watu mbali mbali hapa Kaburu. Hatukujua kama waliotibiwa walikuwa wanapona kweli au ndo ile ya "umekosea masharti" nk.
Akawa na kawaida ya kuja bongo kila baada ya miezi 6, anakaa bongo wiki 1 au 2 halaf anarudi tena Kaburu. Kumbe bingwa alikuwa na mtaalam wake huko Kibada, ambae alikuwa anampa dawa na kumuelekeza namna zinavyotibu na aina ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na dawa hizo. Lakin yeye alikuwa anafanya siri, hakutaka watu wajue kwamba ana mtaalam wake Kibada.
Ilivyofika mwaka 99 uncle alikuwa ni miongoni mwa wageni wachache wenye hela nyingi hapa Kaburu. Kuna watu walihisi jamaa anauza unga, yani ule uganga wake ni zuga tu. Kuna wengine walihisi anafanya kazi ya wizi wa usiku (mchomoko) kimya kimya nk.
Ila ukweli ni kwamba bingwa alikuwa anatumia kazi yake hiyo hiyo ya uganga kujitajirisha. Kwani alikuwa na wateja wa aina mbali mbali wakiwemo wageni, wazawa, wahindi, wa colored na sometimes mpaka wazungu waliokuwa karibu na wahindi.
Nchi hii waganga wote wa mchongo, na wa kweli ni matajiri. Maana wajinga ni wengi mno na kuwapiga ni rahisi mno.
Ndomaana nchi hii imekuwa kimbilio la wachungaji wajanja wajanja kutoka Nigeria, Congo, Zimbabwe, Malawi nk. Pia kuna mashekhe ubwabwa wanaojifanya wazee wa kupiga dua nk. ilimradi kila mtu ana namna yake ya kuwakamua hela wajinga wajinga.
MAMBO YALIHARIBIKA BAADA YA MTAALAM WAKE KUFARIKI.
Mwaka 2000 mtaalam wake alifariki, hivyo ikamlazimu atafute mtaalam mungine wa kumsaidia kupata dawa za kutibu wagonjwa wake. Akapata mzee mmoja wa kizaramo hapo Mwanalumango.
Kumbe mzee alikuwa mjanja mjanja. Sio mganga wala mtaalam. Akawa akimpa dawa, bingwa akifika huku akiwapa wateja wake hawaoni mabadiliko yoyote. Kibaya zaidi kuna wengine dawa zilikuwa zinawadhuru kwa kuwasababishia magonjwa mbali mbali (hapa nazungumzia zile dawa za kunywa)
Wateja wakaanza kumuona tapeli na kuanza kumuandama kwa kauli mara "turudishie hela zetu" mara "unataka kutuua" nk.
Bingwa akaanza kutafutwa kimya kimya. Kwa watu wanaoishi Kaburu wanafahamu ni nini kinachoweza kumpata mtu anaefikia steji ya kutafutwa kimya kimya.
Kwa vile bingwa alikuwa na hela, basi wala hakusumbuka kutoroka nchini na kurudi bongo ili kukwepa balaa lililotaka kumkuta.
Bongo nako aliona hapamfai kutokana na aina ya maisha ambayo alikuwa ashazoea kuishi huku Kaburu. Hivyo akaamua kujiongeza mapema na kuhamishia maisha yake Canada ambapo anaishi mpaka leo.