Netanyahu asema Israel ipo tayari kwa vita muda wowote dhidi ya Iran

Netanyahu asema Israel ipo tayari kwa vita muda wowote dhidi ya Iran

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,678
Reaction score
27,653
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema makubaliano ya usitishaji vita wa muda na Iran hayaihusu Lebanon na kwamba nchi yake itaendelea kuwashambulia wanamgambo wa Hezbollah hadi watakaposambaratishwa.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutolewa tangazo la kusitishwa vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran, Netanyahu amesema Hezbollah italengwa kila kona na jeshi la Israel.

Hapo kabla, iliarifiwa kuwa usitishaji vita ungeihusu pia Lebanon ambako wanamgambo wa Hezbollah walijiunga kuisadia Iran kwa kuvurumisha makombora kuelekea Israel.

Netanyahu pia amesema, Israel iko tayari wakati wowote kurejea vitani dhidi ya Iran akisema makubaliano ya sasa siyo mwisho wa azma ya Israel ya kufikia malengo yake ndani ya Iran iwe ni kupitia mkataba wa amani au kurejea tena kwa makabiliano ya kijeshi.
FB_IMG_1775670614762.jpg
 
General Mgunda amrisha makomando wako wa kupasua matofali wakammalize Netanyahu ili vita ya mashariki ya kati iishe maramoja.
 
General Mgunda amrisha makomando wako wa kupasua matofali wakammalize Netanyahu ili vita ya mashariki ya kati iishe maramoja.
Siku vita ni tech,vitu vinaagizwa kisha unaviongoza kwa mfumo vikapige wapi,vita sio kapasua matofali kwa kichwa
 
General Mgunda amrisha makomando wako wa kupasua matofali wakammalize Netanyahu ili vita ya mashariki ya kati iishe maramoja.
Hao wenyewe wanachoweza ni kuwaua waandamanaji wasio hata na fimbo.
 
Atangaze kisha asimtegemee Marekani
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema makubaliano ya usitishaji vita wa muda na Iran hayaihusu Lebanon na kwamba nchi yake itaendelea kuwashambulia wanamgambo wa Hezbollah hadi watakaposambaratishwa.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutolewa tangazo la kusitishwa vita vya Israel na Marekani dhidi ya Iran, Netanyahu amesema Hezbollah italengwa kila kona na jeshi la Israel.

Hapo kabla, iliarifiwa kuwa usitishaji vita ungeihusu pia Lebanon ambako wanamgambo wa Hezbollah walijiunga kuisadia Iran kwa kuvurumisha makombora kuelekea Israel.

Netanyahu pia amesema, Israel iko tayari wakati wowote kurejea vitani dhidi ya Iran akisema makubaliano ya sasa siyo mwisho wa azma ya Israel ya kufikia malengo yake ndani ya Iran iwe ni kupitia mkataba wa amani au kurejea tena kwa makabiliano ya kijeshi.View attachment 3569592
Hana ubavu wa ku shinda Iran ikiwa Hezbullah inamtia makamasi abaishia kupiga Raia wa Lebanon wako kwenye majumba yao.


View: https://youtu.be/njDVVUgJqpo?si=DC2yQmsPpzSvakuZ

Hezbullah leo kamtembezea kichapo si cha kawaida
 
Netanyahu pia amesema, Israel iko tayari wakati wowote kurejea vitani dhidi ya Iran
Aache uongo huyo muuaji. Kwanini wasipigane bila USA? Mbona Iran haipigani kwa msaada wa Russia/China?

Yaani Trump apigane weee alafu credit achukue huyu tapeli
 
Back
Top Bottom