Netanyahu aweweseka wakati akiwadanganya wajumbe wa Congress

Netanyahu aweweseka wakati akiwadanganya wajumbe wa Congress

Hakuna kitu hapo naona mwandishi mihemuko. Huwexi zima moto kwa 80% kisha uache 20% unawaka useme eti uko salama. Israel yapaswa kuingia Rafah imalize kazi. Ni jukumu LA Jordan kufungua mipaka ili wanawake na watoto wakajihifadhi huko,wanaume waendelee kunyukana mpaka mtanange ueleweke!
 
Ili kubadili mwelekeo wa Marekani dhidi ya Israel washawishi wa kiyahudi Marekani wamepeleka kikundi cha wajumbe wa Congress mjini Jerusalem kuzungumza na waziri mkuu wa nchi hiyo,Benjamin Netanyahu.

Katika mazungumzo hayo Netanyahu amewambia wajumbe hao kuwa ushindi wa Israel huko Gaza umebaki wiki kama tatu tu mbele na utapatikana kwa kuingiza vikosi vya IDF eneo la Rafah ili kuwapta viongozi wa Hamas.

Akawaambia wajumbe hao kwamba jeshi la Israel tayari limeshamuua Hamas namba 3 na namba 4 kati ya 10.Karibuni hivi itawaua namba 2 na moja.

Kwa kutamka hayo ni wazi kuwa Netanyahu anaweweseka kutokana na ugumu wa kupigana na Hamas na amesahau kuwa malengo ya uvamizi wake kwa Gaza ilikuwa ni kuwarudisha mateka nyumbani na kuwamaliza Hamas wote eneo hili.

Kuua namba moja mpaka kumi ya Hamas haikuwa miongoni mwa malengo makuu na kwamba kuua viongozi hao hakutamaliza Hamas na wala si mara ya mwanzo katika historia ya vita vyake na makundi kama hayo huko nyuma ambapo haikuwezekana kuwamaliza kabisa.

Wafuatiliaji wa mienendo ya kivita wanaamini kuwa viongozi hao wa Hamas hawapo wote Rafah na kwamba wameshatawanyikia maeneo mengine ya Gaza kama walivyopenya wapiganaji kadhaa kutoka kusini na kuingia maeneo tofauti ya jimbo hilo ambayo Israel ilikwishachoka kuyapiga na kuondoka.

Hali hiyo inafanya vita hivyo visiwe na ratiba ya kumalizika kwa wiki au miezi ya karibuni ijayo.

Silaha pekee ya matumaini anayotumia Israel kwa sasa ni kutumia chakula kama silaha ya kivita lakini kwa silaha haijawezekana kuwasambaratisha wapiganaji hao.

Israel has ‘no choice’ but Rafah offensive, Netanyahu tells US members of Congress

Huku kichapo kikiendelea kutolewa kwa hamas na washirika wake
 
Anafanyiwa operesheni ya ngiri leo usiku kakabidhi madaraka kwa naibu wake mpaka atakapopona . Naona hali inazidi kuwa mbaya
 
Back
Top Bottom