Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa kadri ya uelewa wangu na ufuatiliaji wa matukio kule Gaza nimegundua kuwa yanayoendelea Gaza ni makubwa lakini yanatendeka kukiwa na upungufu wa mtu muhimu tangu mwanzo wa vita katika eneo hilo vilivyoanza mwezi oktoba mwaka 2023.
Mtu huyo ni waziri mkuu wa nchi hiyo hasimu kwa wapalestina,Benjamin Netanyahu ambaye kwa mara ya mwisho aliojitokeza hadharani tarehe nne mwezi huu ikiwa ni siku moja tangu afanyiwe operesheni ya tenzi dume.
Siku hiyo alijitokeza akipingana na ushauri wa daktari wake.Alishiriki kwenye kura muhimu ya kuonesha msimamo wake kutokana na matukio ya siku hizo.
Baada ya hapo alirudi hospitalini akiwa amechoka sana na baadae kutakiwa achukue mapumziko ya muda mrefu na asishiriki moja kwa moja kwenye mikiki ya kisiasa.
Alirudishwa kwenye handaki kuhofia kusikia miripuko ya makombora kutoka Yemen muda huo makubaliano na Hizbullah yalikuwa yakiendelea kutekelezwa.
Taarifa nyingi kutoka ofisi ya waziri mkuu zimekuwa zikimtaja waziri mwengine machachari aitwaye Smotrich.