Never Give Up

Never Give Up

kapolisi

Member
Joined
Jul 18, 2015
Posts
25
Reaction score
5
*Pa Pa Pa*
(Kimya)

*Pa*


- Kezilahabi, 2008 [Kwenye Diwani ya Dhifa]



*Tafakuri Fupi Juu ya Shairi Hilo*

Ushairi ni taaluma kama taaluma nyingine tanzu. Maudhui katika Ushairi hubebwa ndani ya Shairi ambayo hufinyangwa ndani ya jiko la urembo wa mjengo wa shairi na semi zake (umbo).


Shairi hilo la *Pa* kwa mtazamaji wa kawaida unaweza dhani Mwandishi alichanganyikiwa usipofungua macho yako na kulitazama vizuri sio kuliona vizuri.......


Shairi hilo Limenifikirisha sana hasa ktk kipindi hiki tulichonacho...

*Uhalisia wa Shairi*

*Pa* zilizotumika ni mlio unaoweza kuwa aghalabu wa makofi au kishindo au ishara ya adhabu au kipigo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.... Kipigo ambacho kinaashiria kutokukubaliana baina ya pande mbili (migongano)

Ni dhahiri ipo mivutano baina ya Pande mbili.....
Aidha....
Watawala vs watawaliwa
Mabwana vs Watwana
Viongozi vs
Waongozwa
Mabepari vs Wafanyakazi.... Nk


Hivyo kichapo au mlio huo unaonesha mivutano..... Baina ya pande mbili....

Ambapo upande mmoja una nguvu kuliko mwingine kwa kuwa upande huo *mapigo* yake ni ya aina moja na upande wa pili haujarudisha mapigo bali uliendelea na msimamo.....

*Funzo*
Licha ya kuwa upande unaokula kichapo ulipata kichapo mara nyingi....
(mara tatu awamu ya kwanza)

Ila baada ya ukimya na tafakuri.....

Ukaendelea kuamini unachokiamini.. (Pa ubeti wa pili).....


*Mshindo Nyuma*
Never give up - Usikate tamaa kizembe ..... Hata upate maumivu kiasi gani..... (Never)
Kwani kuacha kuamini unachokiamini ambacho ndio kweli iliyo kwenye moyo wako ni Dhambi hata nje ya nyumba za Ibada...


*Msimamo wako sio tu Ndio Picha yako Ulivyo..... Bali ndio Ushindi wako*


Ibrambeya@gmail.com
 
Back
Top Bottom