"HII NI COPY AND PASTE KAMA ILIVYO",
Leo watoto wamefunga shule, kwenye group la WhatsApp la Darasa, Mwalimu ametutumia ujumbe huu, nikaona unaweza kuwa msaada kwa wengi [emoji116]
Wapendwa Wazazi na Walezi ,Mungu ni mwema.
Imefikia tena Wakati Watoto Wetu wananakiwa Warudi nyumbani tar 31/05/2023 kwa Mapumziko.
Nakuomba Sana:-
1. Simamia Mwanao afanye kazi zake zote alizopewa na Waalimu.
2. Mpangie kufanya kazi ndogo ndogo za bustani, kufua, kuku,mifugo nk usimlelee kama yai!
Labda kama una bima ya kuishi nae milele.
Mfundishe ajitegemee siku ukiondoka ghafla asitaabike sana kujua la kufanya.
3. Ongea na mtoto wako juu ya matumizi ya simu na TV mwambie huko ulaya watoto wengi hawapotezi muda, kila sekunde yao ina shughuli.
Movies na simu asilimia kubwa ni kumpoteza mwafrika na mtu mjinga.
Huwezi kufuatilia Series 400 ukawa timamu lazima kuna shida mahali katika Ubongo.
Waambie kuwa dk 1 ya jana alopoteza haitajirudia milele na kuwa kuna wakati watautamani muda wa leo na hautarudi.
4. Ongea na Mwanao juu ya masomo na malengo yake ya mbele na je yatafikiwa!
Muulize juu ya aina za marafiki zake, mwelekeze kwa upendo.
5. Mwambie mwanao dunia imevua utu na ubinadamu, mweleze juu ya Ushoga athari zake, hata na Upuuzi wa Elon Musk ili ajue achague nini duniani humu.
6.Mweleze mwanao juu ya familia yenu, wengi hawajui hata majina ya babu na bibi zao, hata wajomba na shangazi zao, ukifa ghafla ndo atapata nafasi ya kuwafahamu wanapoombwa kuwasaidia kumaliza shule, taf kipindi hiki wakawasalimie bibi na babu pia.
Mfundishe Mwanao kupika hata ugali wa mchicha wengi ni tatizo.
Kama una muda mfundishe kuendesha gari kuna siku atakuokoa utakapohitaji huduma ya haraka na huwezi kuendesha gari. Kwa mtoto aliyetimiza umri unaoruhusiwa kuendesha gari kisheria.
Mwisho mfanye mwanao awe rafiki, we ni polisi, mwanajeshi, mkuu wa shule, mkuu mkuu mkuu yeyote usipeleke ukuu/ cheo, utajiri nyumbani.
Watoto wanayo mengi wanataka kuwashirikisha tafadhali wapeni muda.
Waeleze pia kama haupo kesho unapendelea waishije au waweje.
Wafundishe matendo ya huruma hebu wapeleke vituo vya yatima,
Wazee hata waliopo jirani na Sukari kg 1 tu waongee nao utaona mabadiliko watakayokuwa nayo katika kuwaza na kutenda baada ya hapo.
Kumbuka hao watoto ni wako kwa jina ila Mungu amewapitisha kwako ili wakuzwe kuhudumia watu wengine, hata wewe unahudumia wengine katika kazi yako.
Mungu awabariki na Kuwalinda Taifa la Mungu.
Amen.
...imenukuliwa kama ilivyoandikwa na kutumwa
Sent from my SM-A715F using
JamiiForums mobile app