New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Waziri Mkuu asiwe mbunge bali achaguliwe na bunge na atoke bara.

Waziri Mkuu atajaza fomu ya kuomba uwaziri mkuu na ataomba kwa utaratibu kama wale wanaoomba ubunge wa EAC.


Lazima apate zaidi ya nusu ya kura za wabunge kwa hiyo uwezekano wa raundi zaidi ya moja yawezekana.

Waziri Mkuu ataapishwa na Rais.

Waziri Mkuu ataunda baraza la mawaziri na kuisimamia serikali. Bunge tu ndilo lenye mamlaka ya kuwafuta kazi Rais na Waziri Mkuu.

Hapo, tutakuwa tumetatua tatizo la wazenj kuuza nchi yetu na kutupora ajira maeneo yote yasiyo ya Muungano.

Kupigilia msumari, Waziri Mkuu akatazwe kuteua wazenj nafasi zisizo za Muungano hawa akina Mbarawa hawatatuuza tena.


Wakuu wa mikoa na wilaya lazima wawe ni madiwani wa maeneo yao na watachaguliwa na kuwajibika kwa mabaraza ya madiwani wa maeneo yao.

Mabaraza ya madiwani watakuwa ndiyo mamlaka ya uteuzi watumishi wote wa halamashauri au majiji. Hakuna Waziri Mkuu kuteua wakurugenzi wa halmashauri/majiji. Haya sasa yatakuwa ni majukumu ya mabaraza ya madiwani wa halmashauri/ jiji


Nafasi ya Rais kugeuza serikali za mitaa ni fursa ya kuwazawadia watu wake wa karibu itakuwa haipo.

Madiwani hadi wenye viti wa vitongoji kulipwa mishahara na kupunguza wimbi la ufisadi wa watajwa hawa kufidia dhuluma ya kufanyishwa kazi bila malipo
 
Nafasi za kugombea ubunge, udiwani na Urais kanuni za kifisadi za NEC ambazo zinampa DED mamlaka ya kutuchagulia viongozi zifutwe na vyama vyote vilivyosajiliwa vitawakilisha orodha ya wagombea wao nafasi zote NEC kupitia katibu mkuu wa vyama husika.

NEC itawatangaza wagombea husika kwenye gazeti la serikali na kuwatumia kila mgombea email ya stakabadhi ya kurasimisha matangazo husika.

Wagombea watakuwa wameteuliwa na kuendelea kushiriki kwenye chaguzi zetu
 
Tume ya uchaguzi itateuliwa na Rais kutokana na majina ya mapendekezo yatakayoletwa na vyama vya siasa. Kila chama cha siasa kitapeleka orodha ya majina 5 kwa Rais yakiwa ni mapendekezo ya wajumbe wa tume. Rais halazimishwi kuteua mjumbe yeyote bali atateua NEC yenye sura ya utaifa badala ya kuegemea na kupendelea chama chake.

Mapendekezo ya majina 5 ya vyama vya siasa watachaguliwa moja kwa moja na mikutano mikuu ya vyama vyao.

Hakuna chama cha siasa kitakuwa na wajumbe wa tume ya NEC zaidi ya 25% ya wajumbe wote.

Sifa za mwenyekiti wa tume kuwa jaji wa Mahakama kuu itafutwa maana uzoefu umetufunza kuwa ujaji siyo lazima utende haki. Sasa sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya NEC ni kukubalika na wajumbe wa NEC ambao ndiyo watamchagua Mwenyekiti wa NEC.

Tume itaajiri mtendaji mkuu wa NEC siyo Rais.

Tume ya uchaguzi itakuwa na matawi kila jimbo la uchaguzi na kuwa na waajiriwa wao na kukoma kukasimu mamlaka yao ya kikatiba kusimamia chaguzi zetu kwa serikali za mitaa ambazo ni vijiwe vya makada wa CCM tu.

Kila msimamizi wa jimbo la uchaguzi ambaye ni mwajiriwa wa NEC atakuwa na jukumu la kuandikisha wapigakura kura kila siku ya kazi hadi wiki mbili kabla ya uchaguzi.

Msimamizi wa jimbo la uchaguzi atawapa stakabadhi mawakala wote waliopitishwa na vyama vya siasa ndani ya siku 3 tangu kapelekewa maombi.


Matokeo ya kura zilizopigwa mbali ya kuwapa nakala ya kila kituo wagombea (kupitia mawakala wao) pia yatatumwa kielektronikia moja kwa moja kwenye tovuti ya NEC ambayo itakuwa wazi kwa kila mtu kufuatilia.

Utaratibu huu utatuondolea watumishi wa umma kuchakachua matokeo kwa kubadilisha fomu husika.
 
Swali ambalo limeulizwa sana mkataba huu ni wa muda gani? Wapi palipoandikwa miaka 100? Au wapi palipoandikwa miezi 12 ambayo TPA wamesema? Jibu lipo kwenye kufungu cha 23(4) cha mkataba.

Kifungu hicho kinasema mkataba ukishasainiwa, pande mbili za mkataba (serikali ya TZ na serikali ya Dubai) hakuna upande utakaoruhusiwa kukosoa (denounce), kujitoa (withdraw), kuzuia (suspend) au kuvunja mkataba (terminate) kwa sababu yoyote ile.

Kifungu hicho kinasema hata ikitokea upande mmoja ukashindwa kutekeleza masharti ya mkataba, bado hairuhusiwi kuvunja, wala kujitoa kwenye mkataba huo. Maana yake ni kwamba, Mwarabu akisema atapanua bandari ya Dar iwe kubwa zaidi, halafu akashindwa kufanya hivyo, haturuhusiwi kuvunja mkataba. Sijui unaelewa?

Hawakuishia hapo, kifungu hichohicho kinaeleza kwamba hata tukiingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na Dubai, bado haturuhusiwi kuvunja mkataba (we can not terminate the agreement even in severance of diplomatic relation). Yani hata ikitokea sisi na UAE tumevunja uhusiano wa kibalozi, tukamfurusha balozi wao, bado wataendelea kuendesha bandari yetu. Hata ikitokea tukapigana vita, bado haivunji mkataba. Waaarabu wataendelea kuendesha bandari yetu, penda tusipende.

Kwa lugha rahisi huu mkataba ni wa MILELE. Kwahiyo wale waliokua wanauliza kifungu gani kinachoeleza muda wa mkataba? Ni kifungu cha 23(4). Kinasema mkataba huo ni wa MILELE na MILELE mpaka Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa.

Hii ni zaidi ya ndoa ya Kikristo ambayo ukishaapa kanisani, hata kama ana matege, ni wako huyo mpaka kifo kiwatenganishe. Na huu mkataba kifungu cha 23(4) kinasema ukishasaini tu, ngoma ni MILELE. Hakuna namna ya kutoka. Bahati mbaya tumeshasaini tangu October 2022.

Halafu "mjinga" mmoja aliyekua ripota wa TBC huko Namtumbo leo kawa Msemaji wa serikali, amekaa kwenye V8 anatuona Watanzania wote wajinga. Anatuambia eti ni mkataba wa miezi 12. Shame.!

Mnataka kuharibu urithi wa vizazi vyetu sababu ya matumbo? Hivi Nyerere angechumia tumbo tungepata uhuru? Endeleeni kutetea matumbo yenu, sisi tunatetea watoto na wajukuu zenu. Lakini ipo siku mtajibu. Kama si hapa, basi hata mbinguni.

#BandariYetuUrithiWetu #HatutokiKwenyeReli #ItakuaFundisho

J. Malisa
 
Katika kosa ambalo hatupaswi kufanya ni kukiri TUMESHINDWA.

Hatujashindwa katika kuwawezesha watanzania kujiendeshea mambo yetu.


Nyerere alipoenda UN kuomba uhuru alitoa ushuhuda ya kuwa tuko tayari kujitawala. Sasa tukisema TUMESHINDWA kujitawala basi tunakiri Nyerere alikuwa tapeli wakati siyo ukweli.

Matatizo ya uendeshaji wa nchi tusiyaangalie kijuujuu tu na kuyatafutia majibu yatakayoturudisha kwenye ukoloni mambo leo.

Tukiri yapo matatizo makubwa ya uwajibikaji na yanaanzia kwenye katiba hadi sheria za kawaida.

Katiba yetu inalia na mazingira makubwa ya dhuluma na hayo tuyatambue na kuyashughulikia.

Uchaguzi wa 2020, kwa mfano umezaa uwakilishi haramu ambao hauna uhalali wa wapigakura sasa ukakasi huu majibu siyo kuwakabidhi wageni nchi bali kutambua tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa katiba ya chama kimoja cha siasa bado imejikita kama ni katiba ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Tulianza na Mwadui, tukaja Tanzanite tukawapa wageni, madini yote wageni, hata usambazaji wa maji tuliwapa wageni, hatuko mbali makusanyo ya kodi tutawapa wageni. Hata uzalishaji wa umeme na usambazaji tuliwapa wageni. Mabenki tuliyauza kwa wageni.
Hatuko mbali sanaaaaaaa mbuga zote watakabidhiwa wageni.

Mwishowe hata serikali tutasema tumeshindwa na kuwapigia magoti wakoloni waje watutawale.

Hoja za mraro wa mapato zingekuwa zina mashiko Obama asingewanusuru GM na makampuni makubwa mengine ya USA.

Japan baada ya 2nd world war walikuwa wanapata hasara kwa zaidi ya miaka 40 katika kutengeneza meli. Wajapani walidinda na kuona hasara ndiyo kujifunza na leo hii ni moja ya nchi zinaongoza katika utengenezaji wa meli duniani.

Wachina na wataiwani tulikuwa tunawacheka kwa kutengeneza bidhaa duni lakini KAMWE hawakusema wameshindwa bali waligangamala tu na leo dunia inakiri kweli mchumia juani hulia kivulini.

Kukosea siyo kushindwa bali ni nafasi pana ya kujifunza na kusonga mbele.

Tuamini tunaweza bali mfumo wa sheria ndiyo tatizo. Tusipojiamini tutawaamini wageni ambao watatuwala na wataweka masilahi yao mbele siyo yetu.

Angalia mabenki tu na makampuni tuliyouza lengo lilikuwa yatafanya vizuri zaidi ya sisi kuyaendesha leo hakuna hata moja linaendeshwa vizuri na mengi yamefutwa.

Nchi hii itajengwa na watanzania siyo wageni na mapungufu yetu ambayo ni mengi tunao uwezo wa kuyatatua

Nawakilisha
 
SHERIA YA TUME YA MIPANGO YA TAIFA.


Mapungufu ni kuwa wapishi ndiyo wapangaji.

Wapangaji hawapaswi kuwa watendaji wakuu serikalini.


Rais ndiye mwenyekiti wa Tume tajwa na mawaziri wake waandamizi wamo humo sasa jipya liko wapi?


Mjadala naona ni mrefu lakini matatizo yetu ya kimsingi yaelekea hatuyajua.


Matatizo yetu ni walewale wako kila mahali.

Gwajima anatetea uenyekiti wa Rais eti ni utashi wa kisiasa wakati utashi wa kisiasa siyo lazima utuletee mipango bora.


Kifupi sheria hii inasisitiza uozo uliopo uendelee.
 
Menu
HabariLeo
Tafuta

Home/Biashara/Uchumi
Mkataba Mchuchuma, Liganga kaa la moto
Vicky KimaroFebruary 1, 2023

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imelieleza Bunge kuwa hakuna kazi yoyote inayoendelea kwa mujibu wa Mkataba uliosainiwa katika mradi unganishi wa Chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati leo Februari Mosi, 2023 Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Kihenzile amesema licha ya kusainiwa mikataba katika miradi hiyo lakini inasikitika hakuna kilichofanyika kutokana na sababu za mwekezaji kuhitaji vivutio vya ziada vinavyolenga kumnufaisha zaidi kuliko maslahi ya Taifa letu.

Amesema vivutio vilivyoombwa na Mwekezaji vilikuwa vikikinzana na sheria mbalimbali za nchini. Sheria hizo ni pamoja na Sheria za Kodi, Sheria ya Madini, Sheria ya Rasilimali na Maliasili za Nchi.

Amesema, pia ilibaiinika kuwa Mkataba na Mwekezaji huyo una vipengele kadhaa vyenye mapungufu ambayo yanakinzana na maslahi ya Taifa;

Pia, kucheleweshwa na kuongezeka kwa fidia ya wananchi kutoka Shilingi 11,037,183,020.78 kwa uthamini wa mwaka 2015 hadi Shilingi 15,979,788,649.50 mwaka 2022.

Kihenzile amesema, kiasi hicho kinajumuisha riba itokanayo na kucheleweshwa kwa fidia katika kipindi husika; wakati serikali ikijielekeza katika jitihada za kutafuta mwekezaji mwingine wa kuendeleza mradi, mwekezaji wa awali (SHG) amejitokeza tena na kudai kuwa yupo na ana uwezo wa kutekeleza mradi huo.

“Kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hii takriban miaka 13 kunachelewesha kasi ya maendeleo ya ujenzi wa Viwanda Mama, kushindwa kuongeza thamani ya malighafi za ndani lakini pia kuwakosesha ajira wananchi na kuliingizia Taifa hasara kubwa.”Amesema

Akifafanua suala hilo, Kihenzile amesema mwaka 2011 yalijitokeza Makampuni 48 kutoka nchi mbalimbali duniani kuja kuwekeza katika mradi huo ambapo Kampuni ya Sichuan Hongda Group Corporation (SHG) ilionesha kuwa na teknolojia inayohitajika hususan katika Mradi wa Chuma cha Liganga na kusaini mkataba wa ubia na serikali kupitia shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) t21Septemba 21, 2011 na kuanzisha Kampuni ya Ubia iliyojulikana kama Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL).

Amesema, serikali kupitia NDC inamiliki asilimia 20 na SHG asilimia 80.

“Kamati ilielezwa kuwa asilimia 20 za hisa zinazomilikiwa na Serikali zilipatikana kupitia utaratibu wa ‘Free Carried Interest’ hivyo Serikali haiwajibiki kuwekeza fedha taslim ndani ya mradi ili kumiliki hisa hizo


Amesema, Kamati pia ilielezwa kuwa kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa, miradi hiyo unganishi ina vipengere vitano ambayo ni mgodi wa Chuma wa Liganga wenye uwezo wa kuzalisha Tani Milioni 2.9 kwa mwaka; Kiwanda cha kuzalisha bidhaa za Chuma Liganga chenye uwezo wa kuzalisha Tani Milioni 1.1 kwa mwaka; Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Mchuchuma wenye uwezo wa kuzalisha Tani Milioni tatu kwa mwaka; Kituo cha Kufua Umeme huko Mchuchuma cha Megawati 600 na Msongo wa Umeme wa Kilovoti 220 kati ya Mchuchuma na Liganga na Barabara kutoka Mchuchuma hadi Liganga (shortcut route).

Amesema, kulingana na makadirio ya mwekezaji, uwekezaji katika mradi huo unganishi utakuwa Dola za Marekani Bilioni 3.0, ambapo mtaji wa mwekezaji ni kiasi kisichozidi Dola za Marekani Milioni 600 na mkopo utakuwa Dola za Marekani Bilioni 2.4.

“Kamati ilielezwa kwamba baada ya kusaini mkataba, Kamapuni ya Ubia ilikamilisha hatua za muhimu ili kuanza ujenzi. Hatua hizo ni Uchorongaji na Upembuzi yakinifu, Upatikanaji wa Leseni Maalum za Uchimbaji wa Mkaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakati huo tangu Oktoba 9, 2014.

Pia, utafiti wa athari za mazingira zitakazotokana na utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na njia za kupunguza athari hizo zilifanyika na kupata vyeti vya mazingira vya Mgodi wa Chuma, Kiwanda cha Chuma, Mgodi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma, Kituo cha Kufua Umeme Mchuchuma, na Msongo wa Umeme Kilovoti 220 (Mchuchuma – Liganga).

Amesema vile vile Kampuni imekwishapata vibali vya kutumia Maji kutoka Mito ya Katewaka, Mchuchuma na Lupali.

“Pamoja na hatua hizo inasikitisha kuona kwamba miradi hii hadi taarifa hii inaporipotiwa hakuna kazi yoyote inayoendelea kwa mujibu wa Mkataba uliosainiwa.”Alisisitiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…