Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #8,901
Hakuna fursa tulizozipoteza acha kuongopa.
Tunayo matatizo ya uwezekaji na usimamizi lakini DUBAI PORTS WORLD au mwingine siyo majibu ya utatuzi wa kero tajwa.
Kwanza hakuna mwekezaji atakayewekeza nchini bali yupo wa kukopa kwenye mabenki kwa dhamana yetu na atashindwa marejesho na kutuaachia mzigo wa madeni na riba kibao huku sehemu kubwa ya hela alizozikopa kutoziwekeza hapa nchini bali kuzitumia kujenga hoja nchi nyingine za kupewa fursa za kuendesha bandari zao.
Pili, tuache kujidanganya ya kuwa uwekezaji huu utapunguza urasimu. DP WORLD atakuja na trafiki polisi wake kukomesha rushwa mabarabarani?
Tatu, tuache kupotosha ya kuwa hapatakuwepo msongamano baada ya DP WORLD wakichukua bandari zetu. Kwanza hawatawekeza kama walivyoahidi. Kigugumizi cha ukwasi alichokuwa nacho TISS kinamhusu kwa ukwasi tajwa hana na ndiyo maana hataki kujitia kitanzi cha huo uwekezaji utaanza lini na utakuwa wa namna gani.
Nne, DP WORLD hana sauti juu ya mfumo wa njia zetu za usafirishaji. Itabidi tumpe na TANROADS, TARULA na TRL ili aondoe vikwazo vilivyoko barabarani. Itabidi misururu ya maroli kwenye mizania aidha sheria zitenguliwe au akayakusanye hayo mapato mwenyewe.
Ubovu na ufinyu wa barabara zetu utamkwaza.
Itabidi TRA nayo apewe ili aharakishe makusanyo ya kodi na kuondoa misururu ya malori mipakani. Pia aidha afute kodi zote au kuzipunguza ili kuwavutia watakaozitumia bandari zetu. Vinginevyo, misongamano iko pale pale.
Itabidi pia mizigo yote inayopitia kwake iwe yake kwani wenye mizigo huchelewesha kuikomboa kwa kuilipia na hata wengine kuikacha.
Tunatoa hii mifano kubeza hoja za huyu mpotoshaji.
Kifupi, ili khoja ya huyu mtaalamu itelezeke itabidi DP WORLD watutawale na kuunda serikali, bunge na kusimamia shughuli zote za serikali siyo nchini tu pia na kwa majirani zetu jambo ambalo kamwe halitatokea.
Hatuna matatizo na mizigo inakotokea bali ikifika bandari zetu ndiyo tuna changamoto
Kwa hiyo, kuzungumzia kero ambazo hazipo ni ushuhuda anaongelea mambo ambayo hata hayafahamu na hii hoja yake kuwa amelitumikia TPA kitambo haina mashiko kama upembuzi wenyewe ndiyo huu.