SAFARI YA JERRY SILAA KUUSAKA UNAIBU UWAZIRI YAANZIA HAPA!
Tangia nchi hii ipate uhuru hatujawahi kuwa na mkataba wa nchi na nchi (IGA) ambao kampuni ya umma imechomekewa kwenye mkataba kwa minajili ya kuua ushindani na imegeuzwa kuwa kampuni binafsi kwa minajili ya kupora mali ya nchi nyingine.
Kampuni ya DP WORLD haikupaswa kuchomekezewa kwa kufanya hivyo huu siyo mkataba wa nchi na nchi bali ni mkataba wa Tanzania na DP WORLD inayodhaminiwa na jimbo la Dubai hivyo hauna sifa ya kuitwa IGA.
IGA hutaona kampuni binafsi zinachomekezewa kumeza kampuni za umma za nchi nyingine
Kuingiza DP WORLD kwenye IGA peke yake kunatengua hii IGA kwa sababu yanageuka kuwa makubaliano kati ya kampuni na nchi hivyo kupoteza kabisa maana ya mkataba wa nchi na nchi.
Misingi ya usawa, uwazi, ushindani na ushirikishwaji imesiginwa na huu mkataba pale ambapo kampuni moja imepewa upendeleo bila ya kushindanishwa na kampuni nyinginezo duniani ikiwemo TPA wenyewe?
DP WORLD zabuni yao ni dola 600 Mill na utekelezaji wake haujulikani lakini tunajuaje kuna kampuni nyingine zenye zabuni ya dola bilioni 6 na uwekezaji wa miaka 25 tu? Yaani iko tayari kuwekeza mara 10 ya DP WORLD tena bila sharti hata moja la kuendelea kubebwa na mbeleko za IGA batili kama hii kwenye mipango mingine ya TPA ya uendelezaji wa
Bandari zetu?
Kwa hii IGA kuipa kipaumbele DP WORLD bila ushindani kunatuacha na maswali yasiyo na majibu hivi hakuna mwekezaji mwingine ambaye ana zabuni bora zaidi ya hii.
Ndiyo maana katiba na sheria zetu huhakikisha mali zetu zinalindwa kwa kushinikiza michakato yote kuheshimu misingi ya ushindani, uwazi, usawa, ushirikishwaji na kadhalika wa kadhalika ambayo huu mkataba wa IGA imekiuka.
Ukiona katiba ya nchi na sheria zake zinasiginwa ujue hakuna masilahi ya nchi bali ya viongozi uchwara tu
HUYU DOGO NI MPOTOSHAJI.
Geneva Convention hairuhusu kampuni binafsi au hata ya umma kuwa sehemu ya mkataba kwa sababu inaleta na kuchochea ubaguzi na hivyo dhuluma itashamiri tu.
Pili, Geneva Convention inadai uwazi, ushindani, ushirikishwaji na uwajibikaji kabla zabuni kutolewa. Misingi hii ya utu ilikiukwa katika huu mkataba na hivyo kukosa stahiki ya kuitwa mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi.
Tatu, Geneva Convention inakataza nchi moja kubebeshwa majukumu peke yake na huku mshiriki mwingine wa mkataba kufaidi bila wajibu wowote uliowazi kama kwenye mkataba huu.