Maswali ya kumuuliza Gerson Msigwa
1) Kwanini serikali ilikopa dola milioni 420 benki ya dunia kama haina imani na Uongozi mzima wa TPA?
2) Matatizo yote aliyoyainisha ya TPA ikiwemo wizi, ubadhirifu, kukwepa kulipa kodi na kukosekana kwa mifumo ya kudhibiti Matatizo tajwa kwanini haiwezekani kuyarekebisha ndani ya TPA?
Viongozi wote wa uchukuzi ikiwemo TPA na TRA na TCRA wamo ndani ya uwezo wenu mnakwama wapi kupanga safu za kutatua hizi kero kila mahali?
3) Mapungufu uliyoyainisha TPA hayako kwenye maeneo mengine ya umma?
Serikali kuu na serikali za mitaa hakuna wizi, ubadhirifu, upotevu wa kodi na uzembe? Kwa hiyo, penye kero majawabu ni kuwatimua raia na kuwaleta askari wa mamluki?
4) Lini mtaanza kuibinafsisha Ikulu, serikali za mitaa, mashirika yote ya umma, JWTZ, Polisi, TISS maana ulaji umeshamiri kila mahali?
Au huko waendelee kuiba kwa maana ndiko uhalali wenu wa kutawala ndiko unakotoka?
5) Huoni na mamlaka makubwa ya Rais aliyonayo ni dhahiri aliyeshindwa kuzisimamia bandari zetu ni yeye na anachofanya sasa ni kuwalaumu tu wasaidizi wake?
Kama kuna uwajibikaji si uanzie kwa Madam President halafu na wewe ufuate na wengineo na mkawapisha wenye uwezo wa kuzisimamia taasisi za umma kazi ambazo mmeshindwa?
6) Tunaomba utuonyeshe kwenye mkataba ni wapi hayo matrilioni yametajwa? Kwanini unapotosha umma na taarifa za uongo ambazo hazimo kwenye mkataba?
7) Hivi mliutumia mchakato upi kubaini DP WORLD tu ndiyo inalipa kuuziwa bandari zetu?
Wapi ushahidi wa uwazi, ushindani, ushirikishwaji na uwajibikaji wakati wa mchakato tajwa ili kukidhi mahitaji ya kisheria za nchi hii ambazo ziko kulinda mali za Watanzania?
8) Ni sheria zipi za Geneva Convention zinazoruhusu kampuni binafsi kuingia mkataba na nchi wa aina ya IGA kama huu wetu?
Au inakuwaje kwenye mkataba wa nchi na nchi kampuni binafsi iwe sehemu ya mkataba?
9) Kuna manufaa yapi kwenye mkataba kuipa kipaumbele kampuni ya umma kugeuka ni ya binafsi kama ilivyotendeka kwenye mkataba huu?
Sisi tutanufaika nini kama kampuni ya umma ya Dubai Ports imegeuzwa kuwa ya binafsi kwenye mkataba huu tu?
10) Je utatuhakikishiaje hasara walizozipata Djibouti na Somaliland hata kuwashurutisha kuvunja mikataba yao na DP WORLD haitajirudia kwetu? Wahanga hawa wote wawili wamelalamikia mizigo haikaguliwi, mitambo inazimwa ili kukwepa kodi, mapato yameshuka chini ya yale waliyokuwa wakiyapata kabla ya mwekezaji huyu kuanza kuwapora na uwekezaji waliowaahidi hawajatekeleza hata kiduchu pamoja na miaka mingi ya mkataba kupita?
Wamebaini umuhimu wa kuwatimua DP WORLD ni swala la usalama wa mataifa yao maana malengo yote ya kuwakabidhi bandari zao hakuna hata moja lina mwelekeo wa kutekelezwa?
11) ......tutaendelea na maswali mengine mengi baada ya kujibiwa