New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Nyufa ndani ya Chadema zimezibwa kwa muda na sakata la Bandari lakini kufumuka upya kabla ya uchaguzi.


Kabla ya hili kasheshe la kuuzwa bwerere Bandari zetu nyufa ndani ya Chadema zilikuwa nje nje sasa zimefukiwa kwa muda tu.


Yapo makundi mawili ndani ya Chadema kundi moja laongozwa na Tundu Lissu na la pili liko chini ya Aikael Mbowe.


Ugomvi wa haya makundi mawili ni nani awe mpeperusha bendera ya Urais ujao yaani 2025.


Kundi la Tundu Lissu linaamini mgombea wao ndiye mwenye mvuto na wanaamini alishinda uchaguzi wa 2020 wakati kundi la Mbowe lina mtazamo tofauti na huo wao wanaona ni zamu ya Mwenyekiti wa chama apewe fursa stahiki kama Mwenyekiti wa chama.


Katika hiyo mivutano, kundi la Tundu Lissu limekuwa likibeza jitihada ya Mwenyekiti wao kufikia mwafaka na CCM kwa kudai CCM hawana dhamira ya kweli ya kuwatendea haki wapigakura wa nchi hii.

Pia, Tundu Lissu na kundi lake hawana imani na wajumbe wa hiyo kamati ya mwafaka wakihoji walivyopatikana na wana mwakilisha nani.

Mbowe na wenzake ambao wengi wao ni wachaga wanaona mwafaka na CCM utasaidia kuleta katiba mpya ambayo inabeba matarajio ya wengi ya kufanyika uchaguzi wa huru na haki ukisimamiwa na Tume huru.


Ni dhahiri kwa sasa wamepata gundi ya kufukia hizi tofauti lakini swala tata la bandari haliwezi kuendelea bila ukomo. Tunatarajia mwafaka wa utata na kizungumkuti wa bandari umiliki, uendeshaji wake na mgawanyo wa mapato utapata ufumbuzi kabla ya mwisho wa mwakani na baada ya hapo Chadema itabidi ivalie njuga migawanyiko tajwa kwenye chama chao.
 
Jenerali Ibrahim Babaginda aweka wazi sifa za serikali ya kiraia kupinduliwa


Katika ukurasa wake wa Twitter kaweka wazi hadharani sifa za serikali ya kiraia kupinduliwa.

Moja, uwepo ushahidi wa kutosha palikuwepo na matukio ya wizi wa kura,

Pili, serikali iliyoingia madarakani haina uhalali utokanao na uchaguzi,.


Tatu, wananchi wana malalamiko ambayo wapanga mapinduzi wanaona wataungwa mkono na raia,


Nne, wanao uwezo wa kutekeleza azma yao,

Tano, mahakama zinahalalisha mamlaka haramu.


USHAURI

Kuacha kuiba kura na kutegemea vyombo vya usalama badala ya wananchi kuipa serikali mamlaka ya kutawala ni njia bora ya kuzuia mapinduzi ya kijeshi au machafuko.


 
Nimekutana na swali hili, na haya ndiyo majibu yake.

Swali: Je, DP WORLD ilipatikanaje? Ni vyema kama nchi tuongee lugha moja ili tuelewane.


Majibu:

1. Prof. Mbarawa: Makampuni 7 yalishindanishwa ndipo ikapatikana DP WORLD kwani ilikidhi vigezo vyote.

2. Mohammed Salum, Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Ujenzi: Makampuni hayakushindanishwa bali ilichukuliwa DP WORLD kwa Sheria ya Manunuzi inaruhusu "Single Sourcing".

3. Gerson Msigwa: DP WORLD ilipatikana kwa kufuata taratibu zote na mkataba huu una faida sana kwa nchi yetu.

4. PM Majaliwa: DP WORLD ilipatikana kwenye maonesho ya DUBAI EXPO 2020 yaliyofanyika Dubai mwezi Februari 2022.

5. Mkataba (IGA): Mkataba huu ni matokeo ya mazungumzo kati ya Rais Samia na Kiongozi wa Imarati ya Dubai yaliyofanyika Februari 2022 huko Dubai.

Wewe umeelewa nini?
 
AMINI USIAMINI PANYA ROADS KUWATIMUA SISIEMU MADARAKANI!


Wapinzani wasichojua sisiemu hawatabanduka madarakani kwa njia za kidemokrasia bali kwa vurugu za panya roads.

Neema ya kuwang'oa sisiemu haiko kwenye masanduku ya kura bali siku ambayo panya roads watakapoamua kufanya kweli na hiyo siku haiko mbali.

Wapinzani wanalia na katiba mpya ambayo kamwe sisiemu hawatawapatia. Na hata wapinzani hawajui katiba mpya ikoje hivyo hawajui ni mfumo upi ni sahihi kwa nchi hii

Hata Kenya mageuzi hayakuja kwa kubembelezana yalikuja kwa shari tupu na sisi ndiko tunakoelekea.

Sisiemu wanajidanganya watauza ajira za watanganyika kwa wageni kwa visingizio vya mapato, tekinolojia, wataongeza ajira n.k na kutuponda sisi ni wezi, wavivu, hatujitumi lakini ukweli ni kuwa walioshindwa kazi ni wanasiasa ambao ndiyo wabunifu wa mifumo mibovu na teuzi zao za kifisadi lakini hawako tayari kuwajibika.

La kutushangaza sisi hawatuamini lakini kila kukicha utusihii tuwaamini wao katika harakati zao za kujimilikisha njia kuu za uchumi wa nchi hii!


Uhaba wa ajira siyo katiba mpya ndiyo kaburi la sisiemu.


Vita vya Ukraine kama ilivyokuwa Perestroika ya Gorbachev kule Urusi ndiyo ilifuta mfumo wa chama kimoja na sasa vita hivi kuleta mabadiliko makubwa Afrika na vyama vilivyoleta uhuru kama sisiemu na ANC ya Afrika ya Kusini, MPLA ya Angola na Frelimo ya Msumbiji wataondolewa madarakani kwa umwagaji wa damu ambao haujawahi kuonekana Afrika.


Kadri sisiemu wanasaini mikataba ya kuhamisha utajiri wa nchi na kujimilikisha wenyewe kwa mgongo wa wawekezaji basi tujue polepole wameanza kuwakabidhi nchi wamachinga.


Ajira, ajira narudia ajira ndicho kiama cha sisiemu wala siyo ukosefu wa mfumo mpya wa uendeshaji wa nchi.


Vyombo vya usalama nguvu yake ni vitisho sasa hawa "panya road" watafika mahali hawataogopa kufa na huo ndiyo mwisho wa tisha tisha.


Tatizo la vyombo ya usalama haviwezi kuua kila kijana watakapowaua elfu mbili au tatu wataweka silaha chini na hawa mafisadi wa sisiemu watarokomea kusikojulikana kama mkoloni alivyoishia.


Vita vya Ukraine vinaiondoa Marekani na washirika wake kileleni na sasa ufisadi ambao ndiyo ulikuwa unawaunganisha na viongozi wa nchi fukara kama yetu utakoma na mikataba yote iliyosainiwa tangu tupate uhuru itafutwa bila ya fidia yoyote ile.


Kila mara chunga Urusi mambo yote yanaanzia huko na yataishia huko sisi ni kufuata amri tu.

Yanayotokea Afrika ya Magharibi yanatuhusu sana tusidhani tutapita bila majeraha.

Huwezi karne ya 21 ukaruhusu wageni wamiliki njia kuu za uchumi wa nchi khalafu raia wakae kimya bila ya kukutimua wewe Mtawala na watu wako wote.
 
OUR RULING: TUNDU LISSU NOT PRESIDENTIAL MATERIAL....

And here is our considered reasoning:-


Baada ya kumtafakari sana Mheshimiwa Tundu Lissu imebidi nikiri kutoka sakafu ya moyo wangu huyu atatusaidia sana kwenye kuainisha matatizo yaliko lakini hana majibu yake na haya ni mapungufu makubwa ambayo hatuwezi kuyafumbia macho.

Moja, alijivunia umaarufu kwa kukosoa serikali zote mbili za JK na JPM lakini hakupendekeza nini kifanyike kutibu matatizo aliyoyaona.

Mbili, JK alishangaa watu wanamwamini pamoja ana wapotosha kwenye uhaja wa katiba mpya na hili Lissu alilithibitisha alipounga mkono rasimu ya Warioba ambayo haikuwa na upya wowote zaidi ya kuzigeuza sheria za kawaida kuwa kanuni za kutunga sheria kinyume na matakwa ya kuandika katiba.


Tatu, alihoji Mwendazake kuvunja mikataba lakini hajawahi kutoa mbadala hata mmoja,

Nne, baada ya kovid- 19 kukimbia na ubunge wa viti maalumu Tundu Lissu alikuwa mstari wa mbele kushinikiza wafukuzwe uanachama bila ya kujua alikuwa anakidhoofisha chama chake.

Tano, swala la bandari kajikita katika uonevu wa kihistoria lakini hatujuzi ufumbuzi wake uko wapi. Ni kweli sisiemu imecheza faulo lakini sasa tufanye nini na mikataba wamekwisha kusaini na hawana mpango wa kujitoa.

Sita, angependa tupate katiba mpya lakini hadi leo yeye na wenzie hawajawahi kuandika rasimu yao ili tuweze kuimulika kwenye darubini. Sana sana kavalia njuga mapungufu tu ya katiba iliyopo bila kutupa mbadala na tukielewa hakuna katiba kamilifu. Yaani hata watakapopendekeza kama ipo itakuwa na dosari nyingi tu.

Mwisho, baada ya kumtafakari kwa undani tumefikia kumwona siyo kiongozi wa kutegemewa kuongoza nchi bali ni mhamasishaji mzuri na pia mwanaharakati lakini siyo presidential material atakuja kuwa kama Raila Amolo Odinga tu.
 
Sisiemu kuna matutusa wengi mno

Wanahoji hela za kuzunguka wanatoa wapi kwani na wao wanatoa wapi?


Yaani unajishtaki mwenyewe badala ya kujibu khoja unazozijenga bandari hazijauzwa.

Kama kweli hazijauzwa zimekuwaje?

Pangishwa itabidi utupe mrejesho wa kodi ya pango


Ubia hisa zetu ni ngapi


Binafsishwa = kuuza maana inakuwa mali yake milele na milele amina na bei yake ni hongo mlizopewa au?

Wazanzibara hudai walifanya mapinduzi wakamtimua mwarabu sasa wanaona ganda la muwa la jana chungu kaona ni kivuno.

Kama mwarabu hawafai kwanini sasa mnaona ni jembe kwa watanganyika kama kweli hajawanunua?



 
If you compare these two regimes, The hopeless one under JPM, and this one ,, which one is better now?

To be honest, I do not think I can be fair to JPM because he was a childhood friend, and we were alumni and JKT cadets. Tough to play impartial with childhood buddy, so to speak.

Too personal to give him a fair hearing because I am still hurting for all the lost opportunity. He had the potential to be the greatest of all but miserably fell short on governance and economic management.

The current regime lacks an ideology to unify the citizens, and is ridden with contradictions. At least JPM was a vacuous ideologue though it is within one's ambit to question his sincerity. Looks like there was a yawning gulf between lipservice and actual deeds.

The former made it abundantly clear he cares less about human rights, democracy and the rule of law as a result there was an illegal gag on almost everything.

This regime is hypocritical! And we mince no words for this damning indictment.

On one hand promises sanity but has not changed anything seems to pursue the same policies of wealth transfer to aliens in the name of foreign investment.

So, they look like birds of a feather playing the same old tune of mistrusting citizens while greenlighting economic mercenaries. Both will never hold free and fair elections.

We judge free and fair elections when the nec selection committee is not appointed by the president or by presidential proxies, and the NEC is divorced from local governments in management of our elections.

Also the application of latest technologies in transmission of polling Station forms after elections into the nec portal which is open to public scrutiny.

These are minimum thresholds of a free and fair elections which could have assuaged the clamour and the rhetoric stoking free and fair elections [emoji848]
 
Mbona Tulia Ackson kapaniki hivyo, kulikoni?

Hotuba ya msomi nguli wa sheria imetuacha na maswali mengi hasa mbona anaelekea ana khofu ya kushindwa uchaguzi wa ubunge 2025?

Katika hotuba yake ya leo tumejifunza mambo mengi yakiwemo ufahamu wake wa sheria unatuacha hoi bin taabani.

Kwanza kapendekeza wawekezaji watafutwe na kuongezwa bandari ya Dar-es-Salaam ikimaanisha hata mkataba wa DP World hajausoma na hata kama aliusoma hajauelewa


Mkataba wa DP World umeipa kampuni tajwa uendeshaji wa hiyo bandari ya Dar-es-Salaam bila kuingiliwa na yeyote yule sasa wawekezaji zaidi wa bandari ya Dar-es-Salaam wapi na wapi?

Pili, kaongea kwa niaba ya wana Mbeya lakini hakutueleza ni lini na wapi maana wanambeya wengi wanasema hajawahi hata kukutana nao kwahiyo aache uongo na amwogope Mwenyezi Mungu.


Tatu, taswira yake ilikuwa ya ghadhabu na shari ikiashiria kuna alama za nyakati kesha zisoma hususani za matumizi ya maneno ya ."...... kuna maneno mengi yamepita hapa Mbeya...."

Maneno yapi yamepita Mbeya zaidi ya wapigakura kukujadili utendaji wako mbovu bungeni?

Na ya kuwa, tayari wamepata msitiri anaitwa Msomi Boniface Mwabukusu ambaye sasa ni Mbunge Mtarajiwa wa Mbeya mjini?

Kwa khali tunayoiona huyu mama anaweza kupata kiharusi wakati wowote ule maana hii tafurani siyo ya bure ina jambo linakuja bado lipo jikoni.
 
PARODY: IKULU, BUNGE, TRA, BOT NA TISS KUBINAFSISHWA!


Hoja za kuuzwa kwa bandari kama ni sahihi basi huu ni wakati mwafaka wa kubinafsisha Ikulu, Bunge, TRA na BOT.

HOJA ZA KUUZWA BANDARI.

1) Mapato yataongezeka.

Hoja hizi pia zinashawishi kubinafsisha Ikulu, Bunge, TRA na BOT.

Taasisi tajwa zina matumizi makubwa kwa hiyo tukizibinafsisha tutapunguza nakisi ya bajeti na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeongeza mapato.


2) Tutaokoa fedha zinazopotea kwa wizi na ubadhirifu.

Taasisi zote tajwa kuna wizi na ubadhirifu sasa tukiwapa wageni tutakomeaha hawa viwavi jeshi.


3) Mifumo kutosomana.

Taasisi hizi zote hawasomani kila mmoja hujifanyia atakavyo hivyo mwekezaji atazifanya zisomane maana sisi tumeshindwa.


4) Ajira zitaongezeka.


Ukiwaondoa hawa viwavi jeshi Ikulu, BOT, TRA na bungeni tutaokoa hela nyingi sana na tutatoa mikopo kwa vijana wetu na watajiajiri mamilioni kwa mamilioni.

5) Tutalinda hadhi ya utu wetu.

Kuna utu gani kama sisi ni masikini? Mwekezaji huyu mkubwa atarudishia heshima duniani maana kutakuwa hakuna wezi, wabadhirifu, waongo yaani tutakuwa kama Dubai.

6) Tanzania itakuwa kama Dubai ingawaje wanaoimiliki na mamluki sisi tutakuwa vijijini tunalima kwani kuna shida gani?

Haya hatutafanya kwa sababu pamoja yako sawia na swala la bandari yanaathiri masilahi ya viongozi.


Ukiyagusa masilahi yao watakuja juu na hoja zitabadilika kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…