Tambua ufadhili ndio nyenzo kubwa ya uporaji wa Mali za Africa.
Wakati wa UKOLONI, maliasili za Afrika zilibebwa Kwa lazima.
Baada ya kuondolewa UKOLONI ikawa Sasa wanatumia mbinu mpaka za vita ili mpewe silaha muwapatie dhahabu na chuma na vingine.
Mambo ya vita yalipoisha, wakaona njia rahisi no kupata njia ya kupata viongozi puppets Kwa kuwapa fedha ya Rushwa ya uchaguzi.
Democrasia ya Sasa ya kununua kura imewapa njia Bora ya kutafuta viongozi wasio na akili ya UBUNIFU. Wanachofanya ni kuhamisha Mali za Afrika kupeleka ulaya na Kwa Sasa wametumia njianile ya waarabu kama zamani ili makampuni ya kiarabu yenye hisa kubwa toka magharibi yaendelee KUPORA Mali za Afrika.
Misaada ni lazima. Ukikataa misaada kifo kinakusubiri kama JPM.
KIBAYA ZAIDI ulichukua msaada Leo, kesho wanabadiri thamani ya Dola dhidi ya fedha zako.
Kwahiyo unajikuta ili upate Dola ya kulipa deni utapashwa kuuza bidhaa nje zenye themani kubwa ili kuziba pengo la Dola iliyochezewa kinamna.
Kwahiyo, ni ukombozi wankijeshi utakaotutoa huko au basi kubadiri namna ya democrasia ya uchaguzi.
Maana Kwa Sasa bila kupata fedha ya wafadhili huwezi kushinda uchaguzi.
Tumesikia DPW imeahidi baadhi ya watu kupewa fedha ya uchaguzi. Sasa viongozi makini na wenye uchungua na maliasili za nchi utawapataje.
African isiporudi kwenye DRAWING BOARD juu ya hii democrasia ya VYAMA VINGI na namna ya kuepuka fedha ya nje kwenye uchaguzi, sahau juu ya Afrika kujikomboa na kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa fedha za misaada.
Na actually, hakuna misaada. Ni mikopo, madeni na ndoana za kuzimeza na lazima uzitapike.
TUNAKUPA Hela ya uchaguzi, sisi unatupa bandari zako zote au tupe tuchimbe madini yako ya uranium Kwa bei tuipendayo.
Maana ukipewa Hela ya uchaguzi, utairudishaje. Ndoana. Lazima uiteme. Itoke na mapafu, au ichukue roho. Hilo utajua wewe.
Kwahiyo sio kama MAKANISA. Kwa nchinza magharibi misaada ni SHAMBA ambalo wakiliacha watashindwa kuzihudumia nchi na watu wao.
Ndio maana marekani haina uzalishaji wa maana, ila Kwa kutoa mikopo, kucheza na Dola, Hela na Mali za wizi toka Afrika, vita na uuzwaji wa Silaha, suala la SWIFT CORD, ndo utajiri huo ambao wanatamba nao Kila siku