New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Mara tu alipotinga Magogoni alikiri anajua umuhimu wa katiba mpya baada ya kukikalia kitebe sasa haoni umuhimu wake.

Namwona Mwendazake kama karudi rasmi.
 

Attachments

  • PSX_20230911_190759.jpg
    PSX_20230911_190759.jpg
    140 KB · Views: 3
Shall we be around in 2030?It is very doubtful,because the Globalists want by 2030 to have completed their Depopulation agenda and start initiating the Great Reset.Let us hope that somehow by whatever reason, their plans will be delayed.
We believe there is God in heaven who commanded us to multiply and fill the world.

We know His commandments are the gospel truth

We shall be around to begin the onerous task of dismantling the globalists feats on this beautiful nation.

All big miners shall be SHOWN THE EXIT DOOR and be swiftly handed to whoever is interested in mining.

DP WORLD will also pack their bags as fast as their feet can take them out


Thereafter the locals will jovially take over.

It is a dream we must cling on.
 
We believe there is God in heaven who commanded us to multiply and fill the world.

We know His commandments are the gospel truth

We shall be around to begin the onerous task of dismantling the globalists feats on this beautiful nation.

All big miners shall be SHOWN THE EXIT DOOR and be swiftly handed to whoever is interested in mining.

DP WORLD will also pack their bags as fast as their feet can take them out


Thereafter the locals will jovially take over.

It is a dream we must cling on.
Rutashubanyuma read the Book of Revelation to get the truth,your idea is not based on Bible truth.
 
Baada ya hii ajira maswali yameibuka ni nani mmiliki wa hii radio hata kuwa na ubavu wa kumlipa huyu gwiji wa habari?

Hatuna majibu, tunakiri!

TUONAVYO

Alikuwa mgeni mwalikwa. Hii radio haina musuli wa kumwajiri.
 

Attachments

  • 3b347037d2b54d2c943a276f47e62260_44492128_765419242008674_2228965515952511979_n.mp4
    2.8 MB
Rutashubanyuma read the Book of Revelation to get the truth,your idea is not based on Bible truth.
My considered view was guided by the Book of Genesis.

Revelation evolves around end times hopefully not yet there to be bogged down, do we?
 
Tunasema sheria za uchaguzi zina mushkeli zirekebishwe kabla ya chaguzi za 2024
 
Khoja ya kuwa kwa vile wengi hawaijui katiba ndiyo sababu tusirekebishe vifungu vya katiba zenye ukakasi haina mashiko
 
Kutumia katiba kama kigezo cha kwenda kwenye chaguzi wakati kuna mapungufu makubwa ya kisheria na kanuni za uchaguzi siyo haki mbele ya Mwenyezi Mungu
 
Kiu ya wapigakura ni kuwa na sauti ya kuwachagua viongozi wao itulizwe siyo iendelee kuporwa
 
Uchaguzi wa 2020 umethibitisha yapo matatizo ya wizi wa kura unaofanywa na taasisi za umma
 
MATATIZO YA UZALISHAJI WA UMEME NI MIPANGO MIBOVU TU!

At last wameacha kuongopa. Mwanzoni walidai matengenezo sasa imebidi wawe wazi muda wake hauwezi kuwa mrefu sana kuendelea na danadana.

Ukweli ni kuwa uzalishaji kiduchu na hili ni uzembe mtupu. Tumewashauri zaidi ya miaka 20 sasa vipaumbele ni gesi na makaa ya mawe siyo maji kuzalisha umeme wakaweka pamba masikioni.

Haiwezekani utegemee mvua kuzalisha umeme wakati una mibadala ya nguvu.


SHIRIKA LA UMEME TANZANIA-TANESCO

TAARIFA YA KUKOSEKANA UMEME TAREHE 13 SEP 2023,JUMATANO.


Shirika la umeme TANESCO Arusha linawawataarifu wateja wake hakutakuwa na huduma ya umeme siku JUMATANO na kupelekea baadhi ya maeneo mkoa wa Arusha kukosa huduma ya umeme.

ASUBUHI

SIKU
- JUMATANO

TAREHE - 13-09-2023

MUDA 2:00 ASUBUHI HADI 12:00 JIONI.

SABABU Ukame na Ukosefu wa Mvua uliosababisha upungufu wa maji na kuathiri uzalishaji Umeme.

Laini na maeneo yanayokosa umeme

SINONI
Uswahilini,kwa mrombo yote,baadhi ya maeneo ya Mbauda,Murriet yote,baadhi ya maeneo ya olasiti,mlima CCM,nadosoito,olkungu,njiro ndogo,oljoro yote,mbuyuni,bwawani,mirongoinne,songambele,kwa shehe,custum,kinana na baadhi ya maeneo ya wilaya ya simanjiro.

M5
Sekei yote, olgilai,ngiresi,bangata,midawe,engokareti,kwa mbotela,songota.

NGORONGORO
Sabato, Bashay, Njia Panda, Ngorongoro,Changarawe,Oldean,Endashangwet, Mng'ola juu, Midabini, Kambi ya Simber, Mang'ola juu, Midabini, Kambi ya Simba,Mang'ola Magorofani, Mang'ola barazani,Mang'ola mbuga nyekundu, mang'ola kisiri, Mang'ola malekchad.

MERERANI
Baadhi ya maeneo ya wilaya ya Mererani.

USA M/MERU
Kimandolu,Kwa mrefu,shangarai,oldadai,ngulelo,sasi,snow crest hotel,moivaro,kijenge juu,kwa shabani,Ambureni.F2Esso, Mbauda,TFA.Majengo,shamsi,ngarenaro,Tanfoam,TANAPA,Airport,Magereza,Matevesi,Ngaramtoni ya chini,Visima vya maji vya A-Z,Country Coffee,Sombetini,Njia ya Ng`ombe ya pili.

MANYARA M/MBU
NMC, Mangafi, Gibbs, Endoro, Marera, Ayalabe, Rhotia, kilima tembo, Mbulumbulu, Manyara kinaoni, Chemchem, Mto wa Mbu, Selela, Engaruka, JKT Makuyuni, Kwa Laiboni, Makuyuni.

USA KIA
Wilaya yote ya Usa River

JIONI

SIKU
- JUMATANO

TAREHE - 13-09-2023

MUDA 12:00 JIONI HADI 5:00 USIKU.

SABABU Ukame na Ukosefu wa Mvua uliosababisha upungufu wa maji na kuathiri uzalishaji Umeme.

Laini na maeneo yanayokosa Umeme.

M3
Soweto,white rose,kibanda maziwa,sakina,masai land,kiranyi,olosiva,freedom lodge,siwandeti,majengo, Lush garden.

AIRPORT
Sable square,balton,ngaramtoni ya chini,texas,kisima cha maji cha monduli,kendown,kibao cha Dodoma,mringa estate,burka,TPRI,Agha knan,likamna ya mwanzoni.

MONDULI –LBS
Olasiti yote, burka, mateves, kisongo yote, aim mall majengo, na wilaya yote ya Monduli.

SANAWARI
Sanawari, naura spring, mianzini. Ilboru safari lodger, ilboru secondary, oltroto, kioga, mula, visima vya maji vya sanawari.

INDUSTRIAL 3
PPF,Banana,Olorieni,AICC Kijenge,Suye,Pentagoni,Mashine,Kwa Sayore,Moshono yote,Chekereni,Meat king.

LONGIDO
Namanga,lengijave,oldonyosambu,mbuga nyeupe,longido yote,lesinoni,olkokora,wilaya ya loliondo

THEMI 1
Nanenane,Njiro SDA, Chuo cha uhasibu,ESAMI,Njiro kwa tondi,Double B,Kikwakaru A,Sunflag quarters,jeshini,Njiro complex,kambini,World Vision,TBC,FFU


Shirika linaendelea kuomba radhi na uvumilivu kwa usumbufu unaendelea kujitokeza kwa wateja.

NB: TAARIFA HII INAWEZA KUBADILIKA WAKATI WOWOTE KULINGANA NA HALI YA UZALISHAJI UMEME ITAKAVYOKUWA

Kwa mawasiliano tupigie kupitia 0748550000.

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja
TANESCO ARUSHA

12/09/2023.
 
HATUWEZI KWENDA UCHAGUZI WA 2024 NA 2025 BILA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA UCHAGUZI.

Watawala wamekuja na mbinu ya medani wengi hawaijui katiba iliyopo, vyama vya siasa siyo wamiliki wa Katiba na ubora wa katiba siyo lazima haki ikatendeka.

Hivi ni visingizio vya kukwepa kurekebisha mfumo wa uchaguzi na kutushinikiza tuendelee na dhuluma ambazo kwa kiwango kikubwa zimechangiwa na sheria za uchaguzi.

Maeneo yafuatayo ni vyema yakarekebishwa kwenye sheria za uchaguzi ili kulinda haki za mpigakura:-


Sheria inayowapa wakurugenzi wa halmashauri za majiji/ manispaa na wilaya kusimamia chaguzi zetu zifutwe na Tume ya Uchaguzi iajiri watendaji wake na kuwa na ofisi za wasimamizi wa uchaguzi kwenye kila jimbo.

Kanuni za uchaguzi zinazowataka wagombea wajaze fomu za kugombea baada ya kuteuliwa na vyama vyao vya siasa vilivyosajiliwa zifutwe. Makatibu wa vyama vya siasa tu wawe ndiyo wanawakilisha orodha ya majina ya wagombea wao katika nafasi zote nchi nzima. Hii itaondoa wimbi la vyombo vya dola kuwapora wagombea wa vyama vya upinzani fomu tajwa au wasimamizi kuzitumia fomu tajwa kuwaengua kwa sababu za kukosekana kwa picha au muhuri au dosari za kiapo au sahihi. Kwa kuwa vyama vya siasa vimesajiliwa hakuna uhaja ya wagombea kujaza fomu. Urasimu huu lengo lake ni kujenga mazingira haramu ya kuwavua wagombea wa upinzani haki yao ya kimsingi ya ushiriki wa kuchaguliwa. Pia wapigakura huporwa haki yao ya kuwachagua wagombea wafaao pale ambapo idadi ya wagombea inapunguzwa na warasimu na hata warasimu kufikia hatua ya kuwachagulia viongozi wasiowahitaji.

Tume ya uchaguzi kupitia waajiriwa wao kwenye majimbo ya uchaguzi ndiyo watawapa barua za mawakala wa vyama vya siasa badala ya wakurugenzi tajwa kufanya kazi hiyo. Uzoefu tulionao unaonyesha wakurugenzi tajwa hutumia madaraka yao haramu vibaya kwa sababu wengi wao ni makada wa CCM na pia wana mashinikizo ya mwajiri wao ambaye ana masilahi mazito kwenye chaguzi zetu kupindisha haki. Utaratibu ulivyo sasa unatoa mianya kwa wakurugenzi tajwa kugoma kutoa barua za mawakala na kwa kufanya hivyo kuharamisha chaguzi zetu kwa kutokuwa huru na za haki.

Vituo vya uchaguzi ambavyo mawakala wa chama chochote watazuiwa kushiriki na kuhakiki zoezi la kupiga kura basi chaguzi za kituo husika yatatenguliwa na uchaguzi wa vituo vilivyoathiriwa utarudiwa.

Tekinolojia ya kisasa itatumika katika kuyatuma matokeo kwenye tovuti ya Tume tajwa ambayo itakuwa wazi nyakati zote ikionyesha fomu za uchaguzi za kila kituo na jumla ya kura kwa kila jimbo yaliyotokana na yale ya kila kituo.

Majumlisho ya kura za kila jimbo yasiyoambatanishwa na matokeo kwenye fomu za kila kituo yatabatilishwa. Hili ni muhimu kwa sababu matamko mengi ya chaguzi za urais na wabunge yameonyesha hayana uhusiano wowote ule na yaliyomo kwenye fomu za vituoni. Kinachojitokeza wakurugenzi tajwa hutamka matokeo ya majimbo watakavyo kulingana na mashinikizo ya wale waliowateua kuzishika hizo nyadhifa.

Usafirishaji wa matokeo kutoka vituoni kwenda tovuti ya Tume ya uchaguzi yatumwe kwa tekinolojia ya kisasa badala kwa mikono ambako uzoefu umeonyesha ubadilishaji wa matokeo kwenye fomu za vituoni hufanywa na vyombo vya usalama ili kuhalalisha kutengua matakwa ya wapigakura yaliyojumuishwa kwenye fomu za kila kituo. Baada ya kuwaibia kura wagombea wa CCM kwa kubadilisha fomu za vituo vya uchaguzi wasimamizi wa majimbo hufanya majumuisho haramu yake na kutamka ya majimbo kinyume na matakwa ya wapigakura.

Matokeo yote ya uchaguzi yatangazwe ndani ya siku 7 ili kuondoa hisia za upangaji wa matokeo.

Mabadiliko ya uteuzi wa makamishina wa Tume ya uchaguzi inaweza kusubiri marekebisho ya katiba ili kuongeza sauti ya wapigakura kwenye utendaji wa Tume ya uchaguzi
 
A photo speaking volume of words but we leave it to your fertile imagination to sort it out without being encumbered by our intrusive yet comandeering innuendos.

Enjoy.
 

Attachments

  • Screenshot_2023-09-13_004736.jpg
    Screenshot_2023-09-13_004736.jpg
    75.5 KB · Views: 3

View: https://x.com/iamartin_/status/1701902514747023578?s=48&t=4upxWgiXhM6_ngO5WuEUWQ

MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAFAO YA VIONGOZI WA KITAIFA KUCHOCHEA MATABAKA MIONGONI MWA WATUMISHI WA UMMA.


With all due respect, siyo sahihi kutabiri katiba mpya itayaondoa haya yote. Inaweza ikazidisha zaidi ya hata ya haya. Katiba ambayo hata Chadema walishiriki kuiandika ya Warioba kama ingelikuwa sheria ingelikuwa na haya yote maana yaliwekwa.

Pili, anakosea kuingiza masilahi ya wabunge na ya rais kwani ya wabunge hata wa chadema wanapata pia.

Mbaya zaidi, ubunge ni ajira huyu mama na mtoto wake waligombea kama walivyogombea wengine sasa inahusika vipi na ya wake na familia za wastaafu.

Tatizo la hiyo sheria inakoleza UBAGUZI miongoni mwa watumishi wa umma.

Ilipaswa watumishi wa umma wawe na kikotoo kimoja ili kuimarisha usawa.

Kukosekana kwa kikotoo kimoja ndiyo masilahi ya watumishi wengine wasiyo wa kitaifa kama hawa hulipwa kiduchu na wamewekewa masharti magumu ili kwenye uhai wao walipwe kidogo sana.

Mwandishi alikuwa na mada nzuri ila kaiharibu kwa kuchanganya ajira binafsi za ubunge na za mwenza wake.
 
MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAFAO YA VIONGOZI WA KITAIFA NI UKIUKWAJI WA KATIBA YA NCHI HII!

Kuna sheria iko jikoni yenye kulenga kuboresha mafao ya viongozi wa kitaifa na kuhakikisha wenza wa viongozi hao kulipwa 25% kama mafao ya kustaafu. Pia familia zao kuvuna 60% ya mshahara mara baada ya viongozi wa kitaifa kufariki dunia.

La ajabu, huu muswada pamoja na kuchochewa na mapendekezo ya mbunge na mke wa Rais mstaafu mama Salma Kikwete aliyoyatoa bungeni tarehe ya April 22, 2022 katika Bajeti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (2022/23) lakini baadhi yake pia yamo kwenye Rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalumu la katiba.

Yapo matatizo mengi kama hili bunge litapitisha muswada huo. Tatizo kuu mafao ya viongozi wa kitaifa wastaafu ni ya kikatiba na bunge halina mamlaka ya kuyaboresha bila ya kurekebisha katiba!

Tatizo kubwa ni kupanua nyufa ambazo zinatokana na viongozi wa kitaifa kuyatumia madaraka yao vibaya ya kujipendelea wao wenyewe kila kukicha.

Sheria tajwa inalenga kuimarisha matabaka ya wanaotawala na watawaliwa kwa sababu inapokuja watumishi wa umma wasiyo wa kitaifa utaona bunge hilo hilo hukaza buti kudhoofisha haki za wafanyakazi wa ngazi za chini na kuwaongezea ufukara mara wanapostaafu.

Aidha bunge limeweka ukomo wa umri wa kulipwa haki za kustaafu kwa watumishi wa kawaida na kuwa miaka 60 wakati kabla ya hapo ulikuwa miaka 50-55. Bunge halijali mtumishi akistaafu hana kipato na kumnyima mafao ya kustaafu hadi afikishe miaka 60 ni kumwongezea umasikini.

Pili, bunge hilo hilo limejenga matabaka wako watumishi wa umma wa kitaifa na wasiyo wa kitaifa huku wa kitaifa wanacho kikotoo tofauti na wale wasiyo wa kitaifa. Kikotoo cha viongozi wa kitaifa ni asilimia ya mshahara wa sasa wa cheo kilekile alichoondokea wakati wale wasiyo wa kitaifa msingi wake kwanza haujulikani na pia hujikita zaidi kwenye majumlisho ya mishahara ya mtumishi husika aliyolipwa wakati wa utumishi wake na wala siyo asilimia ya cheo alichoondokea nacho.

Kigezo cha kikotoo hiki ni kumbana mfanyakazi alipwe mafao kiduchu kwani sote tunajua mfumuko wa bei na mapato utaleta m'mom'monyoko wa mafao husika na kutomwezesha mstaafu kumudu gharama za maisha lakini kwa viongozi wa kitaifa mambo ya mafao ya kustaafu ni murua kabisa.

Tatizo ni kuwa Kikotoo cha viongozi wa kitaifa kigezo chake kikuu ni kumlinda mstaafu dhidi ya mfumuko wa bei na mapato. Wakati cha watumishi wasiyo viongozi wa kitaifa kikotoo chao kinalenga kudidimiza mafao ya kustaafu kwa kuhakikisha hakuna uhusiano wowote ule na mfumuko wa bei na mapato!

Hili ni tatizo kubwa la kwanini hakuna kikotoo kimoja kwa watumishi wote wa umma? Lengo la kujitawala lilikuwa kuamini dhana ya kuwa kwa kuwa viongozi wanatoka miongoni mwetu basi watafanya maamuzi yanaboresha masilahi ya wote lakini hali halisi ni kinyume chake.

La kusikitisha sasa hata wenza na familia za wastaafu sasa kulipwa mafao endapo viongozi wa kitaifa watakuwa wamefariki dunia na wenza wao kulipwa pia na hivyo kulipwa mara mbili mbili!!!!

Tuna maswali mengi ya kujiuliza. Mwajiriwa wa umma ni nani haswa? Tunapomwajiri kiongozi wa kitaifa huwa tunaajiri na familia yake pia? Ni wapi kwenye katiba inasema hivyo?

Katiba yetu haitambui wenza na familia za viongozi wa kitaifa kama ni waajiriwa wa umma na kutunga sheria ya mafao ya wenza wa marehemu waliokuwa viongozi wa kitaifa ambao haki zao ni za kikatiba ni ukiukwaji wa katiba. Inabidi kwanza katiba iwatambue wenza wa viongozi wa kitaifa na familia zao ni watumishi wa umma ndipo hapo haki za kustaafu zitawahusu. Bunge haliwezi kuajiri familia ya wastaafu wa viongozi wa kitaifa na kuwalipa mafao ya kustaafu wakati katiba haiwatambui. Na maelezo yanahitajika kwanini watumishi wengine wasio wa kitaifa familia zao nazo siyo sehemu ya ajira wa umma? Zoezi zima lina mwelekeo wa kuondoa misingi ya usawa na kuchochea matabaka.

Kama bunge linataka kuongeza nyufa za matabaka miongoni mwa watumishi wa umma basi warekebishe katiba kama rasimu ya marekebisho ya katiba iliyopitishwa na bunge haramu la katiba.

Bunge likifanya hivyo litakuwa halijakiuka katiba bali litakuwa limewabagua watumishi wengine wa umma ambao siyo viongozi wa kitaifa ambao wenza wao na familia zao hawatalipwa baada ya wao kuaaga dunia.

USHAURI.

Hili bunge ni kinara sana wa kupitisha maazimio na sheria zinazokinzana na katiba ni vyema sasa mkaanza kurudi kwenye mstari na kuikataa hii sheria ya mafao ya wenza na familia za viongozi wa kitaifa waliofariki dunia.
 
This world is OVER!

People are now too narcissistic
 

Attachments

  • IMG-20230914-WA0002.jpg
    IMG-20230914-WA0002.jpg
    66.9 KB · Views: 1
Viongozi wa kitaifa wa Tanzania wanalipwa zaidi ya Viongozi wa kitaifa wa Marekani!
 
Back
Top Bottom