MADEREVA WA WABUNGE WANALIA MACHOZI.
Na Thadei Ole Mushi.
Baada ya kufichua marupurupu ya Mbunge pamoja na Mshahara wao madereva wa wabunge wameomba watanzania wawafikishie kilio Chao Kwa Spika.
1. Wanadai kuwa hakuna Dereva ambaye ana Mkataba hata mmoja wa Kazi yake hivyo KUISHI Kwa wasiwasi kuwa Mbunge anaweza kuamka asubuhi na kumtimua kazi. Hivyo wanaomba watambuliwe kisheria na wapewe mikataba ili wafanye Kazi yao kwa weledi na bila hofu. Wanadai kila mara ukimchukiza Mbunge tu Kwa kuwa huna Mkataba hukufukuza na Stahiki zako zote hupotea.
2. Wamesema Kwa siku Mbunge akiwa Dodoma Dereva hulipwa Shilingi 70,000 kama Posho. Kwa maana hiyo katika kipindi chote Cha Bunge la budget siku 97 wanapaswa kulipwa Shilingi 6,790,000 lakini wanadai Fedha hizi wabunge husaini lakini hazifiki kwao wabunge wanabaki Nazo.
3. Wanaomba Mishahara yao upitie kwenye Account zao Moja kwa Moja badala ya kupitia kwenye account ya Mbunge. Wanadai Kwa kuwa hawana Mkataba na Mbunge ni Bosi wake hawathubutu Kuwadai Mishahara na badala yake mara nyingine hawalipwi huishia kununulia Nyama choma biashara inaisha.
4. Wanadai kuwa Spika aangalie uwezekano wa kuwaongezea mshahara toka 170,000 kwenda laki Tano Kwa kuwa nao Wana familia zinazowategemea. Wanadai ukichukua mshahara wanaolipwa Sasa hivi ni sawa na Kwa Siku analipwa Shilingi 5,000 mshahara huu hata kibarua wa fundi ujenzi huwezi mlipa huko mtaani.
Wabeba Roho za waheshimiwa ni sahihi kufanyiwa hivi?
Share Hadi imfikie Dereva unayemjua.
Ole Mushi
0712702602