Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #6,421
Drugs no match to intravenous intervention
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukimtunuku mtumishi cheo kwa utumishi bora huwezi kurudi na kumpora kuwa hajasomea.
Zipo njia nyingi za kuwapandisha vyeo watumishi zikiwemo darasa, utumishi wa kutukuka na wa muda mrefu.
Huwezi kumpandisha cheo kwa utumishi wa kutukuka wa uaminifu wa kukataa kuhongwa burungutu la pesa halafu baada ya miaka miwili uje na hoja ulikuwa uteuzi wenye masharti ya kuhenyea!
Uaminifu hausomewi unatuzwa na Mungu. Huwezi kujifunza kuwa mwaminifu kwa hiyo huwezi kumwadhibu mwaminifu kwa kutokwenda kusomea cheo ambacho umemuenzi kwa kulipa sifa na hadhi jeshi la polisi ambayo mhitimu wa hayo mafunzo kamwe hatainua hadhi ya jeshi la polisi kama huyu mtumishi mwaminifu. Sisi makabwela tuliwashtukia kuona mnaenzi maadili kumbe tulikuwa sahihi: Huwezi kuitukuza sifa ambayo huna.
Kumvua cheo baada ya kumfungulia mashtaka inadhihirisha uongozi mzima wa jeshi la polisi unakerwa na watumishi waaminifu ndani ya jeshi hilo hata kufikia hatua ya kuwaburuza mahakama ya kipolisi kwa kosa la kukubali kutunukiwa cheo bila masharti yoyote yale.
Alipopewa cheo hakupewa masharti haya mapya. Swali la kujiuliza uongozi wa jeshi la polisi kwa nini mnavunja masharti ya mkataba huu wa upandishwaji cheo? Kigugumizi hiki kimetokea wapi, kinasukumwa na nini na kimeanza lini? Kuweni wa kweli Mungu anawaona.
Kama cheo cha utumishi bora kina masharti ya kukisomea sasa mlimpea cha nini? Utumishi wa kutukuka ni wa kutukuka tu hauwezi kubezwa na sifa za darasa. Utumishi wa darasa ni wa darasa na wa kutukuka ni wa kutukuka tu na hakuna uhusiano wowote baina yao.
Sijui mahakama ya kipolisi ikoje lakini yaelekea hutimiza majukumu yake kisiasa kwa kuufurahisha uongozi wa jeshi la polisi na hivyo haiwezi kutenda haki. Hii inajibu vilivyo khoja ya kwanini hakukata rufaa. Hakukata rufaa kwa sababu hana imani na mahakama ya kipolisi ambayo ni dhahiri haiko huru hata kuhoji mambo ya kimsingi tu kama barua ya kupandishwa cheo inasemaje kuhusu sharti la kuhenyea cheo. Kama barua iko kimya basi mahakama ya kipolisi ilipaswa kuutupilia mbali mgogoro mzima na kumrejeshea mtuhumiwa haki zake zote za cheo husika.
Inakuwaje utumishi bobea ambao tayari umeenziwa kwa kupandishwa cheo uonekane una dosari za kupungukiwa sifa za darasa? Kama utumishi bora haujakamilika bila kuusomea sasa IGP alimpandishaje cheo ambaye wakati anampandisha cheo alitamba anayo mamlaka sasa mahakama ya kipolisi inasema hana kama mtunukiwa hana sifa za darasa!
Mtazamo wetu.
Mrudishieni cheo chake maana alikihenyea pale alipokataa rushwa ya Tshs 10.mill. Anawazidi polisi wote wenye shule huku siyo waaminifu.
Na hivyo vitisho vya makalipio makali kwa kudai haki aliyopokonywa isivyo halali na kinyume cha sheria vikome na ahadi za IGP kumwonyesha kazi nazo azisitishe mara moja kwa sababu moja tu mtu wa kawaida ataona hili ni bifu dhidi ya watumishi waaminifu maana mabosi siyo waaminifu ni viwavi jeshi.
Sasa huyu malaika wa Mungu anasulubiwa kwa kukemea vitendo vya ukosefu wa uaminifu ndani ya jeshi hilo yaani aliwaumbua mabosi wake kwa kukataa kukata kidali aliyodoboshwa nayo.
Hawa mabosi wana kinyongo sana maana hata hela ya sare ya polisi iliyomo kwenye bajeti wanaitafuna kulingana na taarifa ya CAG sasa wanapata ukakasi kuona ndani ya jeshi hilohilo wako ambao wanakhofu kubwa ya Mungu hawapokei pesa chafu. Wako tayari polisi wa kawaida atumie kamshahara kake kujinunulia sare kulikoni kutumia fedha za wavuja jasho kuwapunguzia zigo zito la kujivalisha sare za kazi.
Ni kwa vile nchi haina maadili ndiyo maana hawa vibosile waliotenda huu unyama hawatawajibishwa kwa sababu za kisiasa tu siyo za kiutendaji.