"Tulitoa ajira za Askari 700 na wote wakapandishwa vyeo na Mimi ndio mpandisha vyeo, haina maana Mtu akipandishwa cheo asifanye kazi, warudi wakasimamie Wafungwa, hatuwezi kuajiri kila mwaka, kama una cheo au hauna cheo na hauna kazi ya kufanya ofisini rudi field ukafanye kazi, cheo chako utabaki nacho wala hakiondoki hata kama unasimamia Wafungwa"
"Msitulazimishe kuajiri Watu wapya kwasababu Watu wengi wamepanda vyeo, mtanifanya sasa nisipandishe vyeo kwasababu nikipandisha mnakuwa hamfanyi kazi"
"Kwahiyo hili la ajira sitotoa nimezungumza siri na Kamishna Mkuu wa Magereza, sio siri tena ameniomba niajiri Askari wengine ameniambia nipe tu hata wa darasa la saba niruhusu tu niajiri wakasimamie Wafungwa"
"Kusimamia Wafungwa kunataka uzoefu na Mtu aliyefunzwa vizuri sasa ukiniambia nikupe tu hata darasa la saba hata kama utawafunza kwa miezi mitatu, wale niliowapandisha vyeo ni wazoefu zaidi warudi wakasimamie Wafungwa na sitotoa kwa sasa ajira mpya"——— Rais Samia akizindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Magereza, Dodoma leo
#MillardayoUPDATES