New Age Paganism

Hapo kwenye ilimradi usivunje sheria ndipo penye msingi, fanya yote lakini usivuke mipaka na kufanya yale aliyo kataza Mungu wako.
 
Pia mtu akijitambulisha kama mpagani basi anakuwa mtu ambaye hana misingi ya kiimani na haieleweki katika jamii zetu
Huo unaoitwa upagani ndiyo misingi halisi ya imani katika jamii zetu.

Kabla ya kuja Uislamu na Ukristo miaka mia chache iliyopita, huo unaoitwa upagani ulikuwepo.
 
Hiyo riziki ambayo vijana wanatafuta, Inatoka kwa Mungu na hakuna anaye pata kwa ujanja wake pasipo na kibali kutoka kwa aliye juu.
Ndio Mungu kawapa riziki acha vijana wafurahie wanavotaka wao kama watatumia kungonokea, kumchangia Lisu, kubetia, kulewea hiyo ni wao...wewe sio wakili wa Mungu mpaka uite watu wapagani
 
Huo unaoitwa upagani ndiyo misingi halisi ya imani katika jamii zetu.

Kabla ya kuja Uislamu na Ukristo miaka mia chache iliyopita, huo unaoitwa upagani ulikuwepo.
Kweli ulikuwepo, na haikuwa njia sahihi ndipo wakaja watu na habari njema za njia ya kweli kutufikisha neno la Mungu.
 
Tokeni, mmedanganya sana waafrika kwa kipindi kirefu na hizo dini zenu za kishenzi, hakuna kitu kinaitwa upagani, hilo neno limeletwa na hao wazungu&waarabu kuwaaminisha wasiofuata dini zao ni wapagani, kumbe si kweli.

Kwa bahati mbaya kizazi cha sasa ni vijana waliostaarabika sana ndiomaana hawadanganyiki tena na hizo dini zenu mlizotumia kuwaharibu akili babu na baba zetu.

Na kwa taarifa yenu weka akilini hili jambo, miaka 10- 15 ijayo katika dini zenu mtabaki na magofu matupu au waumini wachache sana ambao nao wazee watupu maana kizazi cha sasa kimeamka kimeanza kuhoji undani wa hizo imani za akina Yesu wa mchongo na Allah wa mchongo, tunawauliza maswali mazito ambayo hata mashekhe&maaskofu wenu hawana majibu zaidi ya vitisho ya motoni na stories za kutungwa.

Acha watu waisi wanavyojua wao, zama za kutishana na upuuzi wa Miungu ya watu weupe zimepitwa na wakati.
 
Kweli ulikuwepo, na haikuwa njia sahihi ndipo wakaja watu na habari njema za njia ya kweli kutufikisha neno la Mungu.
Mungu hayupo na hizo habari njema ukizichambua zina matatizo mengi sana.

Mmeondoka kwenye matatizo ya upagani wenu, mkaja kuchukua upagani wa wageni.

Nikikuwekea contradictions za kwenye Biblia huwezi kuzitatua.
 
Zamani watu walikua wastahimilivu sana na walikua na vifua sana mtu anafarijiwa kanisani/msikitini lkn hamna cha maana anachopata na haoni kama ni shida, ila vijana wa saivi maisha yamekua magumu umletee porojo za utakua billionea kwa maombi?
Yaan unakwenda kanisani/msikitini ili ufajiriwe? Acha tu hayo majumba yenu ya ibada yabaki matupu maana kwa maandiko ya vitabu vya dini haswa ukristo, kanisa ni mtu mwenyewe sasa anayekwenda kwenye hayo mamikutano na makusanyiko sijui anatumia maandiko yapi tena zaidi ya janja janja za wachungaji kuwadanganya watu wazidi kwenda makanisan kupitia vifungu vya bible ambavyo navyo havisapoti huo uhuni.

Miaka ijayo hayo makanisa yatakuwa magofu ya maonesho, hakuna kijana mwenye akili timamu atapoteza muda kwenda kusalia Miungu ya wazungu
 
Dini tuliletewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…