rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 456
Ooh! Kumbe huko ndiko unakotaka kuelekea.
Yaani nitoe MCHANGO ILI NAMI NIWE MIONGONI WALIOCHANGIA KUWATUKANA WAISLAM, UISLAM NA MTUME WAKE?
Rafiki yangu X-Paster usitoe kisingizio cha kutotoa mchango wako kuisaidia JF kuwa utakuwa unachangia dini yako na mtume wako kutukanwa. Hivi sasa una zaidi ya post 2000 na tukiangalia nyingi zaidi ni za kutetea dini yako. Sasa je kwahilo hustahili kutoa mchangio wako? Mbali na hilo kuna mangapi umeyafahamu kupitia JF? Kuna watu wangapi wamefikiwa na ujumbe wako ulioutoa hapa? Kwani hayo hayahitaji mchango wako? Ukisema dini yako inatukanwa mbona hata wewe umetukana dini za wenzako? Wewe unaangalia upande mmoja tu! Acha visingizio wasiliana na Maxence utoe mchango wako ili JF iendelee kuwa hewani. Sawa rafiki yangu?