Nafahamu kuwa hapa JF ni mahali palipojaa watu wenye upeo wa hali ya juu kuhusu matumizi ya kompyuta.Ndio maana huwa ninakimbilia hapa mara nyingi japo wakati mwingine siyo mahali pake.Nina imani kwa undugu uliojengwa na JF,mtanisaidia.
Ni kwamba tumeanzisha ICT laboratory.Na ili computer zetu zidumu muda mrefu na kuwe na matumizi sahihi nimepatiwa kazi ya kudesign posters za kuhamasisha na kukumbusha watumiaji.Ninachoomba ni mchango wa mawazo.Itakuwa vizuri ikiwa mtanisaidia ideas juu ya hizo posters.Sina pa kuanzia.