New Targets: Slaa na Raia Mwema



Mimi nawashauri CHADEMA kuwa wasiweke mgombea urais mwaka 2010 kwani Slaa na Zitto ni wachanga sana na hawaTOSHI wanahitaji muda sana kukomaa.
 
Kwa vigezo gani umetumia kusema ni kiongozi makini kuliko wote Tanzania?? Ushabiki mwingine bana..hadi unakuwa kipofu..Slaa ni kiongozi mlalamikaji mzuri sana Tanzania...(I will fight abakie upinzani milele)
 
Upinzani ni muhimu utilie mkazo kuelimisha wananchi hasa wa vijijini bila ivyo haya majambazi yataendelea kupora labda tuamue kutafuta machine gun

kwa Bahati mbaya sana wengi wetu huwa tunakariri propaganda za CCM nsa kuamini kwamba ndiyo ukweli wenyewe. upinzani sasa hivi una nguvu zaidi maeneo ya Vijijini kuliko mijini.

vyama vingine vimeanza kupata kura nyingi zaidi vijijini kuliko mijini. wakati sehemu nyingine za Tanzania CHADEMA imepata viti vingi kwenye serikali za mitaa,lakini imeambulia viti vinne tu kwenye jiji la Dar es salaam!!

hoja hii ya kuelimisha wanavijiji ni sawa na ile inayosema vyama vingine viungane ili kuitoa CCM. inawezekana kweli timu nyingine ziungane ili ziitoe Simba kileleni? ili nani awe mshindi kati yao?
 

Mkuu Mwanakijiji,
Kuna kipengele kimoja ambacho CCM watakitumia kumpaka Slaa kama itakuwa JK vs Slaa. Ili kisiwe na uzito, ingefaa Slaa amshawishi Prof. Lipumba awe mgombea mwenza na hapo wata-neutralize hiyo ngebe.
 
Dr. Slaa anauwezo mzuri na anauzika kwa wapiga kura kuliko Bwana Mbowe. Lakini Dr. Slaa anajulikana zaidi mijini kuliko vijijini na katika uchaguzi wa urais watu wa vijijini ndiyo hasa wapiga kura, hivyo bado JK anaendelea kuongoza nchi.
 
Mkuu Mwanakijiji,
Kuna kipengele kimoja ambacho CCM watakitumia kumpaka Slaa kama itakuwa JK vs Slaa. Ili kisiwe na uzito, ingefaa Slaa amshawishi Prof. Lipumba awe mgombea mwenza na hapo wata-neutralize hiyo ngebe.

Du!! kumchanganya na Lipumba!!! watamninginiza kama walivyo mfanya Mbowe Tarime!! CHADEMA wasimame wenyewe kwa bara wanaweza JK hamwingii Slaa.
 
Mimi nawashauri CHADEMA kuwa wasiweke mgombea urais mwaka 2010 kwani Slaa na Zitto ni wachanga sana na hawaTOSHI wanahitaji muda sana kukomaa.

Tunaposema mtu bado yuko mchanga sana kisiasa tunamaanisha nini hasa!! Je JK ambaye tulimuona kakomaa kisiasa (kakulia kwenye siasa) anatusaidiaje? kuuza nchi na kukumbatia ufisadi ndo kukomaa kisiasa tunakohitaji? Au tunataka mkomavu kisasa ili atakapo pewa nafasi aweke mafisadi wenzake na kuwalinda naye kujijengea mahekalu? Mtazamo wangu hapa tulipo tunahitaji kiongozi mwenye kusbutu kuchukua maamzi magumu kwa faida ya nchi na si kwa maslahi kwa mafisadi kwa mgongo wa kulinda wawekezaji.
 
Dr. Wilbroad Slaa ndio kiongozi anaefaa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2010, yuko makini katika utendaji wa kazi na matokeo yake tumeshaoyaona katika vita yake dhidi ya UFISADI. Kama Dr. Slaa atagombea mimi nitarudi bongo na kuwashawishi wengine wa ughaibuni kufanya hivyo ili tupige kura zetu kwa sababu tunajua haitokuwa kula kwa Chama Cha Majambazi na Mafisadi (CCM)
 
Slaa anakubarika
Je Mbowe atakubari kuachia nafasi hiyo?
Slaa Rais
Zitto waziri mkuu
Mbowe hatumtaki fisadi
 


Umesema vyema sana . Watu wengi hasa hapa JF wanakuja na theories na stories uhalisia wa maisha hawaujui . Mimi nasema wana JF transform kutoka kuandika na kuonyesha kwamba unajua hadi kwenye vitendo .Elimu hii si vyama pekee hata wewe una wajibu . Kanisa limeamua kutoa Elimu hiyo leo CCM inalia .Chadema na upinzani unafahamika sana huko vijijini kuliko Dar .
 
Jamani Slaa akigombea urais. tujiandikishe na tukapige kula tuache porojo tu za maneno kwani huwa hatupigi kula na ni wa kwanza kulalamika. kwa kweli tutaleta mabadiliko yanayotakiwa. sina wasiwasi kwani wote hamtakubali kuhongwa pilau
 
Dr. Slaa anauwezo mzuri na anauzika kwa wapiga kura kuliko Bwana Mbowe. Lakini Dr. Slaa anajulikana zaidi mijini kuliko vijijini na katika uchaguzi wa urais watu wa vijijini ndiyo hasa wapiga kura, hivyo bado JK anaendelea kuongoza nchi.


Huu ni uongo Chadema ikifahamika Kijijini basi ujue Dk.Slaa anajulikana zaidi .wanaona TV wanaenda mijini na wanasoma magazeti
again fanya research
 
Dr Slaa akiwa Rais (Mungu apishie mbali) nahamia Cambodia. Slaa huyu huyu alienunua nyumba kwa kutumia pesa za mayatima akiwa Padri, Slaa huyu huyu ambae ndie msimamimizi mkuu wa pesa za Chadema anamuachia Mbowe anakwapua mapesa ya ruzuku kwa kisingizio cha kujilipa madeni hewa.

Dr Slaa yupo Bungeni miaka 15 sasa hana lolote la kuwaonyesha wananchi wa Karatu za kelele za Mwembeyanga.

Dr Slaa? NO thank you!
 


Majungu mbali na ukweli mbali .Weka ukwelo hapa wa madai yako . Na wewe wa karatu huwezi kuwasemea watu wa karatu.Ukitaka kujua kafanya nini Muulize Makamba wako aliweka camp kule na kaishia kupata mitaa 6 Jimbo zima . Ndiyo kipimo na anapimwa na watu wake si wewe hapa .

Madai mengine haya 2 tafadhali weka ushahidi hapa otherwise ni nyimbo zenu zile zile za CCM .
 

Ahsante sana mkuu kwa mawazo yako. Tuwakee na wasifu wa wagombea wengine basi, ukianzia na Mwenyeketi wetu wa chama tawala!
 


Dr Slaa ana uwezo mkubwa sana ukimlinganisha na Rais wa sasa. Labda wewe humjui vizuri. Tunahitaji rais anayeweza kukemea uovu, hasa ufisadi, na mwenye uchungu na nchi yake. Sifa hizi Slaa anazo na JK hana!
 

Utahamia cambodia mara ngapi?

Mbona uko Cambodia kwa muda sasa. Of all things u can say bado ni hili tu ndilo unakuja nalo - la mayatima? wapi hao?

Na Kikwete aliyekaa bungeni na serikali kwa miongo mitatu ana nini cha kuonesha wananchi zaidi ya IPTL, richmond, EPA, buzwagi, dowans, TRL, ufisadi bandarini, utumiaji wa pesa za serikali bila record, kufuta surplus ya pesa za kigeni iliyoachwa na Mkapa, etc etc etc
 


This is very cheap! Kama ni kuhamia Cambodia ungehamia sasa ambapo kiongozi wa nchi anakumbatia mafisadi na kuipeleka nchi pabaya. Hakuna utawala wa sheria, Mafisadi wanazidi kuimaliza nchi huku yeye akiwachekea. Tunahitaji wanamapinduzi wa kweli 2010. Kwa kuanzia tunamuona Dr Slaa. Na sio lazima agombee kupitia Chadema. Sisi wenye nchi tunaweza kuamua kuanzisha chama kikubwa cha upinzani chenye nguvu ya wananchi wengi wanaoumizwa na ufisadi huu wa sasa.
 
Dr Slaa ana uwezo mkubwa sana ukimlinganisha na Rais wa sasa. Labda wewe humjui vizuri. Tunahitaji rais anayeweza kukemea uovu, hasa ufisadi, na mwenye uchungu na nchi yake. Sifa hizi Slaa anazo na JK hana!


Jana kuna mtu aliniuliza kwamba ni kwa nini Mbowe amekiri kuwa atagombea ubunge? Sikuwa na jibu la moja kwa moja wakati huo.

Ila sasa nitamtafuta nimpatie jibu kwani sasa "Sauti iliayo nyikani" imenifikia. Hakika Tanzania inaweza kuwa kitu kingine kabisa katika sayari kuanzia Oktoba 2010.
 
..... beg to differ, itakuwa kama kumsukuma mlevi!
This si coming from the horse's mouth. Personal secretary wa Makame kanena someni btn the lines.



unaweza kuweka hata ushahidi wa kimazingira?
Ulipong'ang'ania TANESCO inunue mitambo chakavu ya DOWANS

Mods hawezi kukusaidia kamwambie mkuu wa nji mwenyewe

Mkuu, usitutie hasira saa hizi... mnataka kuwa watawala siyo viongozi... hii si ufalme, ni demokrasia, kama mkuu wa nchi hajiheshimu na sisi hatutamheshimu, Ebo! Usitutishe, kama una la kusema na la kumtetea useme, siyo kuleta vitisho hapa!
Msamehe anasiku mbili humu

Nakubaliana na Mchukia Fisadi, sehemu pekee inayokufaa ni Mirembe. Mwenye akili timamu hawezi kusema kitu kama hicho hapo juu akisahau kuwa dakika mbili kabla alisema hicho nilicho quote hapo chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…