New telecom Bill sends shockwaves to investors


Hii sio kweli! Nchi gani ya hiyo inayokulazimisha kulist kwenye stock exchange yao?

Na sioni ni jinsi gani exactly watu watafaidika kwa hii sheria, kuwa na shares za Voda haina maana kuwa lazima ufaidike wakipata faida, kampuni yenyewe ndo inaamua kama itatoa dividends.

Kwenye shares kuna risk, watu wakiingia hasara watakuja kulalamika humu kuwa wameibiwa!
 

Wamelazimishwa kwa sababu walikuwa hawataki Watanzania nao wafaidike na hizo faida kubwa wanazovuna. Hata siku moja huwezi kusikia kampuni kubwa ya Japan ambayo inataka kuinvest US isione umuhimu wa kulist hisa zao katika NYSE.

Ni kweli kwamba hisi pia hupoteza thamani (depreciation in value) lakini mara nyingi hisa huongeza thamani. Pia siyo kweli kwamba ili kufaidika ni lazima kampuni itangaze kugawa dividends. Shareholders wanaweza pia kufaidika kama thamani ya shares zao imeongezeka na kuamua kuziuza. Kwa mfano hata kama kampuni haijatangaza dividend shareholder aliyenunua shares kwa U$4 na zikaongezeka hadi kufikia labda U$30 akiamua kuuza hapo faida yake ni $26 kwa kila share atakayoamua kuiuza ukiondoa capita gains tax ambayo hutozwa katika nchi nyingi za magharibi.

Kuna kampuni ambayo watu walinunua share moja kwa $3 na baada ya miaka michache ziliongezeka thamani hadi kufikia juu kidogo ya $400. Wengi waliamua kuziuza shares zao kwa wingi na kupata faida kubwa sana na wengine kuamua hata kuretire kitu ambacho hawakudhani kama wangeweza kukifanya katika muda mfupi ujao. Na hii kampuni ilikuwa bado haijagawa dividends kwa shareholders wake.

Kwa maoni yangu huu ni ubaguzi tu wa haya makampuni makubwa kukataa shares zao kuwa listed katika DSE kitu ambacho hawawezi kukifanya NYSE au London Stock exchange maana kwa kuuza shares zao wanaongeza pia pato lao na hivyo kuweza kuexpand zaidi au kuongeza ubora wa bidhaa zao.
 
Sijasema kwamba tunahitaji kufanya investor awe happy bali tunahitaji kutengeneza mazingira ambayo yenyewe yatachochea uwekezaji. Hapo nyuma nimesisitiza tu kwamba hapo wanayaandalia mabenki na mifuko ya pensheni namna ya kuwekeza mitaji yao na si wananchi wa kawaida.
Haya makampuni yanaamua kulist na yapo controlled kutoka nje. Ghafla unatokea mtikisiko unadhani nini kitafuata kama si hasara isiyo na mathili? Unakumbuka wale jamaa wa TV. Baada ya headquarter yao kutangaza kufilisika na Tanzania hali ilikuwaje. Tujijengee uwezo wananchi waanzishe makampuni Tanzania na wao wenyewe waone haja ya kulist kabla ya kuwang'ang'ania foreigners walist. Tena wananchi wakiwa na uwezo foreigners wenyewe watataka kujiunga. Mf Ernst n Young na Massawe etc.
Huko Asia investment strategies zao zimebadilika saana yaani wamerelax saana sheria zao.
 

Kwanini Watanzania binafsi ambao wana uwezo wa kununua hisa za makampuni hayo wasiruhusiwe kufanya hivyo?
 
BAK hapo umenena maana kampuni yenyewe ndiyo inatakiwa ione umuhimu na lengo kubwa zaidi ni kupunguza exposure inayotokana na currency fluctuation na pia wanakuwa wanahitaji capital ili waexpand operations zao.
Watu wanakariri kwamba mara nyingi hisa huongezeka value basi wasingekuwepo investment managers. Kuinvest ni kama kugamble na kama ilivyo biashara nyingine unaweza ukapata faida au hasara. Huo ni mfano wako mmoja wa faida ipo mifano mingi ya hasara. Hebu fuatilia performance S&P 500 from 2000 t0 2010 utaona nini kilitokea. Ila ukianzia 1950 utaona faida. Kwahiyo issue ya faida huwezi kuiita mara nyingi. Kwa tanzania waulize watu wa TOL.
Ubaguzi upi hapo au policy ya nchi yetu mbovu? Hebu angalia inflation, exchange rate risks etc. Hivi unadhani mitaji yao ilipatikana kwa kukopa Tshs. Watengeneze sound fiscal and monetary policy ndiotuendelee. Otherwise mkiendelea kulazimisha watu wataondoka, mtapoteza ajira na hamna mtaji wa kutosha kuinvest basi ni balaa
 
Kwanini Watanzania binafsi ambao wana uwezo wa kununua hisa za makampuni hayo wasiruhusiwe kufanya hivyo?
Nami pia nimeuliza swali langu hapo. Hivi makampuni yote ya Tanzania yana capital ya kutosha hadi tulazimishe makampuni ya simu? Kwanini tusiwawezeshe hawa walist kwa kutengeneza sheria zinazofanana na hali yetu?
Sina tatizo na Watanzania kununua share lakini iwe ni kwahiari ya wenye kampuni. Yaani unadesign idea mpaka inakuwa successfull, unajiona hufikirii expansion mtu anatokeza analazimisha ubia. Haingii akilini
 

Nimesema ni ubaguzi kwa sababu pamoja na kuwa hizi kampuni zinapata faida kubwa sana nchini kupitia huduma zao za simu kwa Watanzania lakini wakati huo huo hawataki kuona Watanzania hao wanafaidika kupitia makampuni hayo kwa kuweza kununua hisa kirahisi kama zikiwa listed katika DSE, na hivyo kufaidika kwa kupata dividends kama makampuni hayo katika siku za usoni wataamua kutangaza ugawaji wa faida au kuziuza shares zao kama zimeongezeka thamani na hivyo kupata faida ambayo itawaletea maendelea Watanzania hao katika nyanja mbali mbali za maisha yao na Taifa kwa ujumla.

Waje wainvest nchini mwetu lakini wakati huo huo wasione umuhimu wa Watanzania kuwa shareholders katika makampuni yao bali wanataka shareholders wao watoke katika nchi za magharibi! Huu kwangu ni ubaguzi na hili haliingii akilini kabisa kwa sababu makampuni haya nayo yatafaidika kutokana na Watanzania kununua shares zao maana hii ni njia nyingine ya kujiongezea mapato katika kampuni hizo.
 

Ni kweli kuwa share value inaweza kuongezeka, lakini inaweza kupungua pia, lazima uangalie pande zote mbili kabla ya kufanya investment. Kuna watu wengi wamepoteza life savings zao kwenye stock exchange.

Juzi juzi tu watu walikuwa wanalalamika humu kuwa shares zao zimepungua thamani, nadhani zilikuwa za NMB sikumbuki vizuri.

Kampuni zinalist kwenye stock exchange ili kupata capital, yaani ni business decision inayoiletea kampuni manufaa, hawajalazimishwa.

Sasa tukianza kulazimisha tunaondoa process nzima ya maamuzi ya kibiashara, kuna kampuni zengine za simu utakuta hazipo fit kulist kwenye DSE, zikifilisika mtawaambia nini wawekezaji?
 
Ni kweli kuwa share value inaweza kuongezeka, lakini inaweza kupungua pia, lazima uangalie pande zote mbili kabla ya kufanya investment. Kuna watu wengi wamepoteza life savings zao kwenye stock exchange.

Mkuu Kang, ndiyo maana ya kuinvest siyo siku zote unapofanya uamuzi wa kuinvest mahali kuna kuwa na faida tu wakati mwingine kunakuwa pia na hasara.

Juzi juzi tu watu walikuwa wanalalamika humu kuwa shares zao zimepungua thamani, nadhani zilikuwa za NMB sikumbuki vizuri..

Hili hutokea kabisa na ndiyo maana kama unaamua kuinvest basi ni vizuti ukafanya hivyo ukiwa na lonterm vision badala ya short vision ambayo mara nyingi huwa ni hasara au faida ndogo sana

Kampuni zinalist kwenye stock exchange ili kupata capital, yaani ni business decision inayoiletea kampuni manufaa, hawajalazimishwa.

Hili pia ni kweli kabisa, lakini hapa Serikali imewalaizimisha hawa baada ya kutoona kuwa pamoja na kuwa wako nchini kwa muda sasa lakini hawana mpango wa kuwa listed katika DSE. Serikali katika uamuzi wake imeangalia zaidi maslahi ya Watanzania badala ya yale ya kampuni, kitu ambcho mimi nakiunga mkono.

Sasa tukianza kulazimisha tunaondoa process nzima ya maamuzi ya kibiashara, kuna kampuni zengine za simu utakuta hazipo fit kulist kwenye DSE, zikifilisika mtawaambia nini wawekezaji?

Kufilisika kwa kampuni hutokea hata katika nchi za magharibi na investors wamepoteza bilions of their hard earned money. Fuatilia stories za makampuni kama Enron, Nortel na juzi juzi kulikuwa na ya Madoff, lakini pamoja na hayo kwa maoni yangu hii si sababu yenye uzito mkubwa kwa nini makampuni haya ambayo yanavuna faida kubwa sana nchini mwetu yasirahisishe upatikanaji wa hisa zao kwa Watanzania kupitia DSE.
 
It is not true kwamba tunawahitaji foreign investors sana kuliko investor wa ndani nchini mwetu. Kama kampuni ni public company kama Vodaphone etc kwa nini wanawaogopa investors wazawa? Hapa inaashiria kitu kimoja. Kuna ulaji mkubwa wa kutisha na wanaogopa watafichuliwa maovu yao. Mbona mambo yako poa tu huko western countries kwenye maswala ya public companies.

Hoja ya bei kupanda na kushuka hilo ni swala la investor halimuhusu mtu asiyeweka investment yake.
 
Tunaendelea kuonekana laughing stock

Tanzania: Local Mobile Firms Shocked By New Bill

4 February 2010

Tanzania's parliament yesterday passed a bill that will make it compulsory for mobile firms to be listed on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).

The Citizen reports many members of parliament, before passing the bill, accused mobile phone companies of treating customers unfairly and denying the government billions of shillings in taxes.

Godwin Ngwilimi, legal and regulatory affairs head of Vodacom Tanzania Limited, said the new legislation takes the country back to the era of nationalisation when individuals were forced to sell their companies or shares to the government.

Minister for Communication, Science and Technology, Prof Peter Msola, said the Electronic and Postal Communication Bill 2009 is aimed at establishing a legal framework for providing regulations to electronic communication service providers.

Once the bill becomes a law, telecommunications firms will be required to offer shares to the public. They will also be required to list with the DSE within three years after the Act comes into force.
 

Sijui criteria gani ilitumika kuamua "within three years" instead of 12 or 18 months.
 
Sijui criteria gani ilitumika kuamua "within three years" instead of 12 or 18 months.

Bongo we huwajui, watu wanaweza ku pluck a number out of thin air with no research, precedent or justification.

Yaani hapa tunachekesha tunachekesha tunachekesha. Tunatoa mixed signals kuhusu commitment yetu kuhusu free trade, on the one hand Kikwete anazurura dunia nzima kuwaambia wawekezaji kwamba Tanzania inahitaji wawekezaji na ina an investor friendly environment, on the other hand tuna fanya moves za kikomunisti kama hizi za kulazimisha watu ku float shares zao kwenye market, investors walivyo jumpy watajiuliza kama hawa watu wana balls za kufanya kitu ridiculous kama hiki what is next? Outright nationalization?

Mtu yeyote anayejua umuhimu wa PR na potential ya umuhimu wa kulazimisha investors wa float shares zao, atajua kwamba hii bad publicity iko more costly kuliko faida za hayo makampuni ku float shares zao.

Kama serikali inatafuta njia za kuimarisha masoko ya mitaji kunanjia nyingi sana za kufanya hivyo, lakini kulazimisha investors ku float shares ni uvivu wa kufikiri unaoweza kuwa na grave economic consequences.Tayari nategemea hili kutushusha point katika indexes za business friendliness, na investors wana options nyingi tu kwenda nchi nyingine.

On principle, dunia ya leo huwezi kumlazimisha investor a float shares, kama walitaka kufanya hivyo wangeiweka hiyo kama clause wakati investors wanakuja nchini ili mtu ajue from day one. Ingawa hata hiyo ingekuwa totalitalian, lakini watu wasingeweza kusema kwamba tunabadilisha goalposts in the middle of the game which is a very serious charge in the investment world.

Sijui kama bureaucrats wetu wanaelewa hili.

Worse still, wanaweza kulazimisha investors wa float shares at a very high price in terms of the country's PR bila ya kupata chochote in therms of ROI kwa sababu wananchi wenyewe hawako ytayari kununua shares at that level.

Balderdash!
 
I'm in support of the bill, but very baffled by the timeframe... why wait 3 years?? 18 months is more than adequate time for a company to formalize listing.
Next stop should be with the mining firms... Matter of fact with these guys, the legislation to the same effect should be fast tracked.
 

Hilo ndio neno maana tunapoelekea hapaeleweki. Late December 2009, Chavez naye aliwapiga mkwara carmakers industry kabla ya hapo alifanya nationalisation ya hali ya juu. Akadevalue currency. Zote hizi ni Nationalisation. Hili ni tatizo I wish Rais asisaini hii bill. Inapeleka signal mbaya saana on investors protection. We wait and see kwenye INDEX maana itakuwa kituko
 
Sijui criteria gani ilitumika kuamua "within three years" instead of 12 or 18 months.
Nadhani ndani ya miaka hiyo 3, investors wengi watachomoa. Nadhani Zain wanaweza kuwa wa kwanza. Yaani wakati nchi nyingine inaencourage investors siye tunakaa na kuweka vikwazo. Msisitizo wangu ni ule-ule. kwanini wasiwawezeshe watanzania kulist makampuni yao?
 
Hii hypothetical thinking ndiyo iliyofanya watu wapitishe mswada. Kila nchi inawahitaji investors. Hatujajitosheleza kabisa na ndio maana tuna import saana na makampuni ya kigeni yamekuwa mengi. Hivi wakiondoka investors hali itakuwaje? Vodaphone wameweze kulist kutokana na mazingira ya soko husika ila kwa soko la tanzania kulist ni ngumu saana hebu angalia turnover ya soko lenyewe.
 

Technically, wamewapa avenue nyingine ya kuendelea 'kuwaibia' watanzania! Ni uamuzi wa kishabiki zaidi kuliko maslahi ya taifa, Yaani kwa kifupi sheria hii, inawazuia investors kuleta capital kutoka nje na badala yake waitafute kutoka ndani!
 
bahati mbaya sijasoma post zote hivyo kama nita kuwa narudia, napenda kusema samahani.
Sasa nikija kwenye mada inayoongelewa , naona kuna tatizo linalo jirudia, nalo ni kwa serikali kutokuweka vipengele muhimu kwenye mikataba, hivyo wanapokuja na mabadiliko wanapata upinzani, na serikali kuonekana hamnazo.
na kama ni biashara mpya ambao watawala wanapenda kusema ilikuwa ni mara ya kwanza, hatuna ujuzi nayo na uongo mwingine, basi nenda na mkataba wa muda mfupi na hata ukiweka wa muda mrefu unaweka na masharti yako, kwamba hali ikiwa tofauti, basi unayo haki ya kubadilisha mkataba au vipengele vya mkataba..
Mfano John Terry alipo saini mkataba wake na Chelsea, aliweka kipengele kwamba yeye ndio atakuwa highest paid player, hivyo leo hii mtu mwingine akisajiliwa kwa sema 150,000, basi mshahara wa John Kahaba utakuwa adjusted . Sasa Joni akiwa anaakili hiyo, je linchi likubwa kama Tanzania hatuna akili hiyo? Hata mtu akisema oh Joni anawashauri/meneja/wakili nk, je linchi letu halina watu hao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…