Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Happy Monday!
Popote ulipo mdau, kama una fursa ya kupata chanjo ya Corona, fanya hima uipate.
Kwa siku zijazo, itakurahisishia sana mambo mengi, ikiwemo safari za kimataifa.
Mimi nimechanjwa licha ya kwamba si mgonjwa.
Sikupatwa na mzio wowote ule kutokana na chanjo hiyo zaidi ya bega kuuma tu kidogo kwa siku kama mbili hivi.
Ukishadungwa, kwa pande hizi nilipo, wanakupa hako ka kadi kama uthibitisho wa kuchanjwa. Halafu ni bure kabisa!!
Chanjweni ili msije kupata usumbufu hapo baadaye.
Shime!