KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwa mtindo wa uandishi, sitashangaa kama wewe ndiye 'Pascal' mwenyewe!Pascal si mtu wa kujipendekeza
Na kama sio yeye, basi tabia zenu zinashabihiana sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mtindo wa uandishi, sitashangaa kama wewe ndiye 'Pascal' mwenyewe!Pascal si mtu wa kujipendekeza
Angalia tofauti ya nukta na koma utagundua siyeKwa mtindo wa uandishi, sitashangaa kama wewe ndiye 'Pascal' mwenyewe!
Na kama sio yeye, basi tabia zenu zinashabihiana sana.
Bwashee nalaani wizi kama upigaji wapige wote,kama ni mkanda wafunge wote.Mkuu 'Kalunya', sasa nimekuelewa unachosema, lakini sikubaliani na msimamo wako.
Kwa hiyo, kwa maoni yako, kwa vile wakubwa 'wanapiga' na hawa wengine wote pamoja na uzalendo wao unataka na wao wageuke wawe wapigaji?
Mantiki ya namna hii uliiona wapi?
Unahimiza kila mtumishi aliye na nafasi, asitekeleze majukumu yake kwa uaminifu, kwa vile wakubwa wanapiga?
Unataka kila mwenye nafasi inayomwezesha kupiga, afanye hivyo, kwa sababu asipofanya hivyo, atastaafu akiwa maskini, na watu kama wewe mtakuwa mkimcheka kwa vile hakutumia nafasi yake kwa manufaa yake mwenyewe?
Haya ni mawazo ya kipuuzi kabisa.
Kama uovu unaofanywa na hawa viongozi juu ya nchi hii unakuumiza kama waTanzania wengine wote, huwezi kuja hapa na kushangilia maovu hayo hata kama ni kwa aina ya kukata tamaa kama unavyoonyesha wewe hapa.
Haya mambo ya uandishi wa kuzungukazunguka, ukionekana kushangilia uovu, kumbe nia yako ni kuumia kwa uovu huo, ni uandishi mbovu.
Sema wazi unachotaka kusema, usizunguke kama kusifu kumbe una maana ya kulaani.
Sasa unamulaumu nini huyo bosi hapo juu ambaye hata baiskeli hana, lakini analinda heshima yake na heshima ya nchi yake.
Wewe ni mmoja wa wapuuzi, na nimekuweka kwenye orodha hiyo hapa JF.
"KALUNYA", ni mpuuzi.
Bure kabisa.
Wanabodi,
Niko Standby kuwaletea link ya uzinduzi huu.
====
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo ashiriki kwenye uzinduzi wa makala maalumu iitwayo ‘Royal Tour’ jijini New York nchini Marekani.
Makala hayo maalumu ambayo mchakato wake umefanyika kwa takribani mwaka mzima umemshirikisha moja kwa moja Rais Samia akiwa katika vivutio mbalimbali vya utalii nchini Tanzania kwa lengo la kuongeza watalii na kuvutia wawekezaji.
Uzinduzi huo wa aina yake unahudhuriwa na takribani watu 400 unafanyika kwenye Jumba Mashuhuri la Makumbusho liitwalo Guggenheim kuanzia saa moja na nusu za usiku za Marekani, sawa na saa nane na nusu usiku kwa Afrika Mashariki.
Miongoni mwa washiriki ni pamoja na wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, viongozi wa kisiasa, mashirika ya kimataifa, waandishi wa habari na Watanzania waishio Marekani.
Pia wafadhili na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za uhifadhi kama TANAPA, NCAA, TTB, TAWA, TFS na makundi ya wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania wakiwakilishwa na CTI, TBA, TPSF, TATO na CEOrt wahudhuria.
Shughuli hiyo inaoneshwa mubashara kupitia televisheni za Marekani kwenye mfumo wa utangazaji wa umma (PBS) kupitia kituo cha televisheni cha WTTS yenye watazamaji takribani milioni 3.5 na baadaye makala hayo itaoneshwa kwenye zaidi ya chaneli 300 zinazowafikia takribani asilimia 86 ya Wamarekani.
Makala hayo yatazinduliwa pia jijini Los Angeles, Aprili 21, mwaka huu na baada ya matukio hayo mawili, filamu hiyo pia itarushwa kwenye mtandao wa kidijitali wa Amazon na Apple TV.
Kwa Tanzania, filamu hiyo itazinduliwa kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili na baadaye visiwani Zanzibar tarehe 7 Mei.
Taarifa zaidi soma;
Uzinduzi wafanyika New York
Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour umefanyika usiku wa kuamkia leo Aprili 19, 2022 Jijini New York Nchini Marekani na kuhudhuriwa na watu wengi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.
Filamu hiyo maalumu ilitengenezwa kwa mwaka mzima ikimshirikisha Rais Samia kama mhusika mkuu akiwa katika vivutio mbalimbali vya utalii #Tanzania kwa lengo la kuongeza watalii na kuvutia wawekezaji.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na zaidi ya watu 400 katika Jumba la Makumbusho la Guggenheim, baadhi ya waliohudhuria ni wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, wanasiasa, mashirika ya kimataifa.
View attachment 2192524View attachment 2192525View attachment 2192528
View attachment 2192538
Paskali
DSM
Tanzania
Lina umuhimu gani hili tukio? Unataka kuniambia mpaka karne hii hakuna juhudi zozote zilizofanywa kutangaza utalii wetu? Kama vivutio vyetu havijulikani Marekani mpaka karne hii! Hili ni la kushangaza.No sio kuhamasika bali hili ni tukio muhimu sana kwa taifa Letu. Kama huwa tunaletewa live za matukio less important, why not this very important?.
P
Samia kafungua nchi tayari, wapigaji wameshika hatamu, yaani wale wezi wa mali za umma na wahujumu uchumi wanakomba kwa raha zao. Mama anaendeleza yale ya Jakaya,ama kweli hizi ni zama zaoMkuu Kambi ya Fisi , kila zama na zama zake, JPM sio tuu hakusafiri, bali pia alizuia wengine wasisafiri kwa lengo la kubana matumizi. Inawezekana kwake na kwako kusafiri ni kuzurura ovyo hivi Mama anavyo piga ma trips mnamuona kama ni kama anazurura ovyo!. No!. Kwanza kusafiri sio kuzurura, kuzurura ni kufanya safari zisizo na malengo, JPM alikuwa ni Inward person, hapendi kusafiri na kujichanganya na wenzake. Anapenda kujifungia ndani tuu.
Samia ni Outward person, outgoing kama JK, ni mtu wa kujichanganya na wenzake kubadilishana mawazo, uzoefu na kupata exposure.
Matokeo ya JPM kujifungia ndani, aliifunga na nchi, hakuwa na exposure hivyo kuna mambo alifanya kishamba. Sasa Samia anafungua nchi. Matokeo utayaona.
P
Ulishaona wapi kitu kama hicho kinafanyika!Bwashee nalaani wizi kama upigaji wapige wote,kama ni mkanda wafunge wote.
Sio wachache wafunge mkanda juu washindane kulegeza,then fainali uzeeni nani atachekwa.
So wafaao ni wapigaji,au kwa sababu Hakuna sheria iwezayo mfunga fisadi, maana tunajua jela ni kwa ajili ya watu masikini walioiba kuku sababu hawana ya kumuhonga hakimu.Ulishaona wapi kitu kama hicho kinafanyika!
Typical 'Pascal Mayala' approach; popo si mnyama wala si ndege!
Watu wa aina yenu hamfai kwa lolote.
Naona tunazungushana bure 'mkuu wangu 'Kalunya'.So wafaao ni wapigaji,au kwa sababu Hakuna sheria iwezayo mfunga fisadi, maana tunajua jela ni kwa ajili ya watu masikini walioiba kuku sababu hawana ya kumuhonga hakimu.
Ndugu Mimi binafsi sijapata Neema hio tu ya kuzikwapua, maana huu ni upumbavu unakusanya vipi Ili zikaliwe na wajanja juu,KILA mtu ale kwa urefu wa kamba.
Kama taifa limeamua kuwa la wapigaji ifahamike hivyo KILA mtu na apige kulingana na fimbo yake.
Yeye kama atumii nafasi yake vizuri bahati haiji mara mbili wala Hakuna ujira au kuja kuzikwa na tuzo ya uadilifu wa uzalendo ajiandae tu na fedheha siku mfumo utakapo mtupa jongoo na uadilifu wake.Naona tunazungushana bure 'mkuu wangu 'Kalunya'.
Nionavyo mimi, ni kama na wewe inakuumiza sana kuona hali mbovu iliyopo, lakini badala ya kuilaani moja kwa moja, inakuwa kama umekata tamaa, au ungependa na wewe uwe upande wa pili ili ufaidi?
Hayo mapapa yanayotunyonga hayastahiri hata kwa sekunde moja kusifiwa hapa, au kuonekana kuwa sisi tusiokuwa na nafasi hizo tutamani kuwa kama wao. Hawa ni watu wa kulaani, na katika kitabu changu ningependa kabisa pawepo na sheria ya kuyanyonga/kuyapiga risasi hadharani.
Sina chochote cha kutamani kutokana na vitendo vya wahujumu hawa wa taifa letu; na kamwe, siwezi kumlaumu mtu kama "lile li bosi linalopanda daladala" kwa kutotumia nafasi yake ili na yeye aendeshe gari zuri.
Hapa ndipo ninapoachana nawe kabisa.