New York: Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Tanzania - Starring Samia Suluhu Hassan, President of The United Republic of Tanzania

Bwashee nalaani wizi kama upigaji wapige wote,kama ni mkanda wafunge wote.
Sio wachache wafunge mkanda juu washindane kulegeza,then fainali uzeeni nani atachekwa.
 
Mbuga zipo Tanzania au Marekani? mambo ya hovyo kabisa
 
No sio kuhamasika bali hili ni tukio muhimu sana kwa taifa Letu. Kama huwa tunaletewa live za matukio less important, why not this very important?.
P
Lina umuhimu gani hili tukio? Unataka kuniambia mpaka karne hii hakuna juhudi zozote zilizofanywa kutangaza utalii wetu? Kama vivutio vyetu havijulikani Marekani mpaka karne hii! Hili ni la kushangaza.

Mara kadhaa mbuga ya Serengeti imeongoza kwa kuwa Mbuga bora ikishindanishwa na Mbuga nyingine, hili halikuvutia Watalii? kuna Channel kadhaa za Kimataifa zinaonesha Mbuga zetu tangu miaka mingi nyuma, haikusaidia? Au ushiriki wa Rais kwenye filamu hiyo ndiyo itawavuta Watalii?

Tumeambiwa fedha zilizotumika kuandaa si za Tanzania, je huyu aliyetoa hizo pesa katoa kwa Manufaa ya Tanzania? Anafaidika vipi? Kuna tathmini yoyote imefanyika ili kujiridhisha kama pesa zilizotumika kusafirisha kundi kubwa la Watu kwenda kwenye uzinduzi zitapatikana kupitia filamu hii?

Katika kufanya kitu kama hicho usitarajie sana kufanikiwa, endapo onesho hilo halitafanikiwa, gharama zitafidiwa vipi? Maana Watu wanaweza kuangalia na wasione jipya la kuwavutia kwenda Tanzania.

Tanzania ipo katika kipindi kigumu cha mfumuko wa bei, fedha zilizotumika kusafirisha Watu kwenda Marekani na kukaa kwa siku kadhaa zingeweza kutumika kama ruzuku kwenye baadhi ya bidhaa ili kupunguza mfumuko wa bei.
 
Samia kafungua nchi tayari, wapigaji wameshika hatamu, yaani wale wezi wa mali za umma na wahujumu uchumi wanakomba kwa raha zao. Mama anaendeleza yale ya Jakaya,ama kweli hizi ni zama zao
 
Bwashee nalaani wizi kama upigaji wapige wote,kama ni mkanda wafunge wote.
Sio wachache wafunge mkanda juu washindane kulegeza,then fainali uzeeni nani atachekwa.
Ulishaona wapi kitu kama hicho kinafanyika!

Typical 'Pascal Mayala' approach; popo si mnyama wala si ndege!

Watu wa aina yenu hamfai kwa lolote.
 
Pascal Leo ulichofanya nimekumbuka enzi za drive inn cinema,au pale empress cinema walivyoanzisha sinema za mpaka asubuhi kilichotokea no kwamba wale vipofu waliokuwa wanaombaomba madukani mchana ikifiKa usiku wanaeñda empress cinema ikawa ndio nyumbani kwao kulala,Sasa Mayalla mtu kama shaka anamsifu mama Toka Lumumba Huku cinema yenyewe yeye na hata wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM sio wateja walengwa wa hiyo makala.
 
Ulishaona wapi kitu kama hicho kinafanyika!

Typical 'Pascal Mayala' approach; popo si mnyama wala si ndege!

Watu wa aina yenu hamfai kwa lolote.
So wafaao ni wapigaji,au kwa sababu Hakuna sheria iwezayo mfunga fisadi, maana tunajua jela ni kwa ajili ya watu masikini walioiba kuku sababu hawana ya kumuhonga hakimu.
Ndugu Mimi binafsi sijapata Neema hio tu ya kuzikwapua, maana huu ni upumbavu unakusanya vipi Ili zikaliwe na wajanja juu,KILA mtu ale kwa urefu wa kamba.
Kama taifa limeamua kuwa la wapigaji ifahamike hivyo KILA mtu na apige kulingana na fimbo yake.
 
Naona tunazungushana bure 'mkuu wangu 'Kalunya'.

Nionavyo mimi, ni kama na wewe inakuumiza sana kuona hali mbovu iliyopo, lakini badala ya kuilaani moja kwa moja, inakuwa kama umekata tamaa, au ungependa na wewe uwe upande wa pili ili ufaidi?

Hayo mapapa yanayotunyonga hayastahiri hata kwa sekunde moja kusifiwa hapa, au kuonekana kuwa sisi tusiokuwa na nafasi hizo tutamani kuwa kama wao. Hawa ni watu wa kulaani, na katika kitabu changu ningependa kabisa pawepo na sheria ya kuyanyonga/kuyapiga risasi hadharani.
Sina chochote cha kutamani kutokana na vitendo vya wahujumu hawa wa taifa letu; na kamwe, siwezi kumlaumu mtu kama "lile li bosi linalopanda daladala" kwa kutotumia nafasi yake ili na yeye aendeshe gari zuri.
Hapa ndipo ninapoachana nawe kabisa.

Sasa angalia: Ni taifa lipi "limeamua kuwa la wapigaji"?
 
Yeye kama atumii nafasi yake vizuri bahati haiji mara mbili wala Hakuna ujira au kuja kuzikwa na tuzo ya uadilifu wa uzalendo ajiandae tu na fedheha siku mfumo utakapo mtupa jongoo na uadilifu wake.
Kama toka juu wanaiba,wanalamba mikopo na misaada kisha wanamega zao wanaficha bank za Ulaya kwa faida zao binafsi.Sisi wadogo huo mwako wa kulipa kodi tutoe wapi. Sasa kama wanatoboa mtumbwi Ili kupata ubao wa kujisitiri wakati wa dhoruba hali tunazama wote kwann na sisi tusitoboe ubao, maana fainali uzeeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…