Hiyo iliisha jitokeza kipindi cha nyuma. Mara chache sana kutokea. Kama wewe ndio umeanza ushabiki hivi karibuni basi karibu.Mpaka ninavyoandika kuna Mechi Kati ya Newcastle United na Fulham ikiwa ni dakika ya 77. Dakika ya 74 Fulham walipata penati baada ya VAR kuonyesha mchezaji wa Fulham alikwatuliwa akiwa ndani ya Penalt box. Fulham wakapewa penati Yao.
Wakati Mitrovic anapiga Ile penati kwa mguu wa kulia mpira ukamgonga mguu wa kushoto na kumpoteza kipa ukaingia wavuni.
Nasema somo linaendelea Kwa sababu baada ya goli la Man U laililokubaliwa Jana, Leo refa kakataa goli Hilo la Fulham na kuwapa Newcastle free kick kwa maelezo kuwa Ile ni double kick.
Kwangu shule ya sheria na kanuni za soka inaendelea bila ada.
Karibuni Wajuzi.
Ukipata nafasi zitafute Sheria 17 za soka (laws of the game) uzisome maandishi yake. Utapata uelewa mpana sana.Nimeanza kushabikia soka 1982, nimeangalia Kombe la Dunia runingani 1990.
Sio kweli, ulichosema sio sahihiSheria hii ipo, penalty inatakiwa upige moja kwa moja
Labda hukunielewa au wewe sio mpenzi wa kuangalia mpira, tukio kama hilo lishatokea zaidi ya mara moja,kama dembele ishamtokea pia,ulichosema wewe ndio nimesema mimi na ipo hivyo siku zote,mpira ukikugusa sio goalSio kweli, ulichosema sio sahihi
Ni kwamba anaepiga penati, anatakiwa apige mpira mara moja kuelekea golini/nyavuni au kumpasia mwenzake. Lakini sio kujipasia mwenyewe au dribling au kukokota.
Alichokifanya huyo jamaa wa Fulham ni kuugusa mwenyewe mara mbili (mguu wa kulia na kushoto) kabla ya kuguswa na kipa au mchezaji mwenzake au mwingine
Sawa mkuuLabda hukunielewa au wewe sio mpenzi wa kuangalia mpira, tukio kama hilo lishatokea zaidi ya mara moja,kama dembele ishamtokea pia,ulichosema wewe ndio nimesema mimi na ipo hivyo siku zote,mpira ukikugusa sio goal