Hafla ya Kukabidhi Misaada ya Wahanga Wa Mafuriko iliyokusanywa na TPN; Jamiiforums na Michuzi Blog kwa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Tarehe 30-01-2010 katika ofisi za Chama Cha Msalaba Mwekundu; Masaki jijini Dar Es Salaam.
Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko. Pichani ni misaada mbalimbali ambayo ilikusanywa na Wadau mbalimbali.
Mlezi wa TPN Mzalendo Maua Dfatari (kati); Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo na Rais wa TPN Mzalendo Sanctus Mtsimbe wakiteta jambo kabla ya hafla ya kukabidhi misaada katika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu; Masaki; Dar Es Salaam
Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Dfatari (kati) akitoa maelezo kuhusiana na kampeni kwa; Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo (Kulia) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu; Masaki; Dar Es Salaam. Mzalendo Daftari aliweka wazi kuwa Kampeni yetu ni ya Kukisaidia na Kukiwezesha Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross na haina uhusiano wowote na kampeni ya Red Alert inayoendeshwa na Vodacom ambayo hata hivyo wameiga kutoka TPN na Wadau wake baada ya wao kudokezwa kuwa tutaendesha kampeni ya jinsi hiyo. Alisema TPN imefurahi kuwa imetoa changamoto na sasa wadau mbalimbali wanasaidia na kuendesha kampeni kuwasaidia wahanga ingawa ilikuwa ni jambo jema kuunganisha nguvu kwani wote lengo letu ni moja. Aliasa kuwa Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha kuwa misaada inafika kwa walengwa. Kampeni yetu inaendelea kwa kutuma SMS yenye neon TPN kwenda namba 15522.
Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko. Pichani ni misaada mbalimbali ambayo ilikusanywa na Wadau mbalimbali. Mz. Mtsimbe alisema hadi sasa zaidi ya watu 1880 wanachangia katika kampeni ya SMS. Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na ndoo; magodoro; miswaki na dawa za miswaki; sabuni; vyandarua; mablanketi; maji ya kunywa; Nguo mbalimabli za kike, kiume,watoto, Mataulo, mashati, Suruali; Viatu na Madawa ya vyooni vyote vikiwa na dhamani ya TZS Million 5.
Mkurugenzi Mtendaji wa CAPS Limited na Mdau wa TPN Mzalendo Peter Marealle akikabidhi madawa ya choo kwa Mlezi wa TPN kwa ajili ya matumizi ya vyo vya Wahanga wa Mafuriko. Dawa hizi zinaua wadudu wote na harufu mbaya na hivyo kuzuia uwezekano wa magonjwa ya Kuhara na kipindupindu. Madawa hayo yana dhamani ya Zaidi ya TZS Millioni 1.3.