Nilibahatika kumuona wakili Ngalo akisoma taarifa ya kesi hizo kwenye ITV. Taarifa inajulisha amelishwa maneno. Alikuwa akisoma huku anajiumama. Taarifa hiyo ilisomwa kwa dakika 8!.
Huu ni udhibitisho wa yale maneno ya Adam Malima. Sijawahi kuona taarifa ya Ikulu ikisomwa inside news kwa dakika 8!.
Pamoja na ukweli kuwa ITV ni ya Mengi, na ana uhuru wa kuitumia atakavyo, news inabaki kuwa news, kuna professionalism ndani yake. Hiyo taarifa kusomwa yote as if it was a live event, breaking news or development news was wrong proffessional.
Jinsi ilivyokuwa ndefu, nikamkumbuka marehemu John Mdolwa aliyekuwa mhariri mkuu ITV,
Angekuwepo, isingeachwa kama ilivyo hata kama Mengi angelazimisha, Mdolwa angesema "Its unprofessional".
Kuhusu kesi, Mzee Mengi anapenda sana kulianzisha ili kuuthibitishia umma, how clean he is, na akikuta somewhere somehow he is dirty, atazifuta baadhi ya kesi. Mfano hai ni ile kesi dhidi ya gazeti la Mtanzania baada ya kuandika habari kuwa licha ya Mengi kuwa ni Tajiri, lakini ana madeni kibao!. Mzee alifungua kesi, alipoonyeshwa document ya benki kuthibitisha, aliifuta kesi kimya kimya.
Ila pia kitu kizuri, kuna baadhi ya waandishi wanaomchambua sana lakini wanabaki salama na mahali penye usalama, si pengine zaidi ya humu jamvini.
Idumu JF.