Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Wazawa ni mimi mlala hoi, ninayepata mlo mmoja kwa siku, ninayepinda mgongo shambani/kazini kutwa kwa malipo kiduchu ni mimi ngozi nyeusi ambaye baba, babu, baba ya babu na babu ya babu yangu mzaa mama na mzaa babu walizaliwa kamachumu muleba na kufia muleba, na mimi ningali Tanzania na wale wengine wote wanaofanana na mie ndio wazawa, usipoelewa hilo basi kammulize Simba
Mtu asiniambie eti Rostam ni mzawa. Si mzawa hata kidogo hata kama babu yake alizaliwa Igunga au Bukene. Hivi partner wake wa karibu asiwe Lowassa ila ni Habib muiran wafilisi nchi? Eti wanaomtetea si mnafuta njaa na leo na kesho kutwa wakati unga unapanda bei?
Akiomba kusamehewa, Mwangunga alisema yote yalifanywa kwa nia njema. Naona nia njema imekuwa utamaduni na uhalali wa maovu yote tunayofanyiwa na wakubwa hawa. Alianza Lowasa akasema serikali kusaini mkataba na Richmond ilikuwa kwa nia nzuri ya kuliepusha taifa na giza baada ya mtera kukauka, juzi Pinda kaangua kilio barazani akidai kauli aliyotoa usukumani aliitoa kwa nia nzuri ya kuwatisha wauuaji wa ndugu zetu Albino, Lipumba naye akaja na yake kutaka kubebwa na chadema huko Mbeya kwa madai kuwa walimuwekea pingamizi Shitambala kwa nia nzuri ili upinzani uchukue kiti cha ubunge. Sitashangaa kesho akisimama Mzindakaya na kusema pesa alizokwapua BOT ilkuwa kwa nia nzuri ya kuwawezesha wananchi wa jimbo lake kupata maziwa!
Hivi UKIUWA na wewe ni MBUNGE, tena kwa KUKUSUDIA yaani UNAPANGA na kwenda kufanya kitendo. Mbunge huyu akienda bungeni (kama Dito vile) na kuomba msamaha, basi asamehewe? Kwa kesi ya Pinda naweza kusema ni HASIRA ambayo ilipanda bila kupanga na KUROPOKA. Ila huyu Waziri, aliyepokea maombi, akaweka sahihi na huku akijua alishaahidi kuwa HATAFANYA HIVYO, sidhani kama anastahili msamaha. Ni sawa na kesho, ikitokea PINDA aropoke tena, nitakuwa wa kwanza kumvalia BANGO.
Huyu kweli wapinzani ndiyo walitakiwa kulala naye mbele. Wakati anafanya maovu hayo alikuwa na akili timamu. Alijua anafanya nini. [/SIZE]Na kama alikuwa hajui/kasahau maneno ambayo mwenyewe aliahidi na hayo wala si mengi kama katiba basi huyu wakomae naye.
- Tupo ukurasa mmoja mkuu, saafi sana. Huyu mama majuzi alikuwa anahangaika kugawa rushwa ya kumsaidia Auntie Sophia kuwa mwenyekiti wa UWT, leo anaomba radhi on what?
- Tupo ukurasa mmoja mkuu, saafi sana. Huyu mama majuzi alikuwa anahangaika kugawa rushwa ya kumsaidia Auntie Sophia kuwa mwenyekiti wa UWT, leo anaomba radhi on what?
Inawezekanaje kitu kilichozuiliwa na MUHILI mmoja wa utawala (Bunge) uvunjwe na MUHIMILI mwingine (Serikali), Mwanasheria Mkuu wa serikali alikuwa wapi kugundua hili mapema? Mwanasheria wa Wizara alikuwa wapi asigundue hili? Nasikia harufu ya RUSHWA, hapa ni WIZI MTUPU. Na akiwafutia leseni hao wazungu kama keshakula hela yao wanaweza mkomalia wakaja KUMKOLIMBA, akae mkao wa machale chale. Labda kama Wataliano hawamo maana hawa hawana dogo, mafia kwenda mbele!!!
Ni lini watawajibika au kuwajibishwa? msamaha maana yake umekubali makosa na kaa pembeni wengine wafanye kazi. lakini muda bado upo itabidi waangaliwe.
Una hakika kuwa babu wa babu yako alizaliwa Kamachumu?
Ulimkamata? Huoni kama ungefanya hivyo ungeondoa aibu ya chama chako kaka? in simple language ulipomuona ulifanya nini? au unadhihirisha Chukua Chako Mapema?
KLHN International
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Shamsa Mwangunga amekuwa Waziri mwingine wa serikali ya Rais Kikwete kuomba radhi Bungeni kufuatia kile ambacho kimeelezewa kuwa ni kudharau Bunge kwa kuchukua maamuzi ambayo hayakuzingatia hoja ambayo iko mbele ya Bunge. Mhe. Mwangunga ameliangukia Bunge leo hii baada ya Mbunge wa Kwera Mhe. Chrisant Mzindaka kuona kuwa Waziri huyo amedharau hoja yake ambayo ilikuwa inasubiriwa kutolewa maamuzi Bungeni kuhusu suala la vitalu vya uwindaji.
Mwaka jana Bw. Mzindakaya alitoa hoja Bungeni ili serikali isitishe kutoa leseni kwa wawindaji wa nje ambao muda wao unamalizika mwaka huu mpaka taarifa itakapotolewa na Waziri juu ya mapendekezo yaliyotolewa kuboresha sekta hiyo ya uwindaji. Hata hivyo imekuja kugundulika kuwa Waziri Mwangunga ameshatoa maamuzi hayo na kuwaongezea leseni wawindaji hao kitu ambacho "kilimkorofisha" Mhe. Mzindakaya. Endapo Bunge lingeamua kupitia hoja hiyo na kumchukulia hatua Mhe. Mwangunga basi angekutwa na dharau ya Bunge (Contempt of parliament) kosa ambalo linalingana na lile la kudharau Mahakama (Contempt of court). Adhabu ya kosa hilo ni siku saba jela.
Vyanzo vyetu kutoka Dodoma vinasema kuwa baada ya kuona kuwa upepo hauendi upendo wake Mhe. Mwangunga akifuata njia iliyotengenezwa na Waziri Mkuu Pinda jana ambaye aliomba msamaha kwa wale wa Tanzania wanaoona amekosea naye mama Mwangunga aliona hana njia nyingine isipokuwa kuomba msamaha kwa Wabunge. Inaonekana Bungeni kumekuwa na hali ya huruma na baadhi ya wabunge wa CCM na hata wale wa upinzani wametangaza kumsamehe.
Hata hivyo haijulikani huko mbeleni ni kiongozi gani mwingine naye atakuwa tayari kuomba msamaha kwa mtindo huu na hivyo kukwepa kuwajibishwa. Maoni ya watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifuatilia masuala haya wanaona kuwa itakuwa vigumu sana huko mbeleni kumwajibisha mtu yeyote kwani wotesasa watakuwa wanasimama kuomba samahani na wengine kumwaga machozi kwa "uchungu".
Tatizo la nchi hatutaki kufuata taratibu na sheria. Waziri amedharau bunge, kuomba radhi kwa maneno pekee haitoshi, ilitakiwa zifuate hatua zingine za uwajibikaji ili kukomesha mambo ya namna hii. Kesho atatokea mwingine atafanya uozo then ataomba radhi. Huu si utawala bora unaotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na watu wake. Tuache mzaha na maslahi ya taifa letu. Sheria zifuate kwa wote na si kubagua huyu mkuu huyu mdogo. Ifikie mahali tusioneane haya na tutangulize maslahi ya Taifa mbele zaidi ya maslahi ya Vyama vya Siasa.
Tatizo la nchi hatutaki kufuata taratibu na sheria. Waziri amedharau bunge, kuomba radhi kwa maneno pekee haitoshi, ilitakiwa zifuate hatua zingine za uwajibikaji ili kukomesha mambo ya namna hii. Kesho atatokea mwingine atafanya uozo then ataomba radhi. Huu si utawala bora unaotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na watu wake. Tuache mzaha na maslahi ya taifa letu. Sheria zifuate kwa wote na si kubagua huyu mkuu huyu mdogo. Ifikie mahali tusioneane haya na tutangulize maslahi ya Taifa mbele zaidi ya maslahi ya Vyama vya Siasa.
Kwa kuwa amekiri alikosea, ina maana alitakiwa kufuta hivyo vibari na kupisha hoja ya Wabunge indelee na mkondo wake sio?
Samahani bila kurekebisha makosa ina manufaa gani kwa Watanzania?
Subutu!!!! Afute vibali wakati wameshakula vya watu,,, Tayari walishakunja mikwanja yao, wa kupeleka mtoto ulaya keshaenda,,, wa kununua nyumba kesha nunua, wa Vog naye keshalipia,,,, hela hawana tena. Kama unabisha wathubutu kufuta hivyo vibali uone waliotoa pesa zao watakavyong'aka.
Hata hivyo mikikimikiki ya wizara hii haiwezi.
sheria ifuate mkondo wake. Kwa haya maneno ya Zitto aliyoyasema bungeni, nanukuu, "Tukiwa makini na kufuata Sheria namba 3 ya mwaka 1988 ya Haki,Madaraka na Hadhi ya Bunge tunaweza tukaamua leo waziri aende Keko kwa siku saba.Hata hivyo,hatuwezi kufika huko kwa sababu amekuwa muungwana,ameomba radhi"