News Alert:...... Uteuzi cabinet

News Alert:...... Uteuzi cabinet

Mwanri amekuwa Naibu Waziri TAMISEMI.Kwangu naweza nikawa tofauti kidogo na wana JF waliowengi na comment zao kwakuwaangalia watu wafuatao.
1.Uteuzi wa Celina Kombani TAMISEMI kama Waziri unaweza ukasaidia kuimarisha utendaji kwani Kombani amefanya kazi kwa muda mrefu serikali za Mitaa na ata baadaye alipokwenda kusoma na kurudi kwenda SUA kama Afisa Utumishi kule.Ninaweza nikawa na Imani naye.

Kawambwa ninaimani naye kwani kwa muda mrefu yeye hana kashfa yoyote na si mtu wa kupenda popularity yeye ni mtu wa kazi na Engineer huyu kumpeleka Miundombinu ni sawa kabisa kulingana na proffessional yake.Pamoja kwamba watu ni walewale lakini unapopelekwa baadhi ya wizara kulingana na utaalamu wako na uzoefu unaweza ukafanya jambo la kueleweka.

Nawasilisha.
 
Mzee Mwanakijiji,mimi naona sio kuchagua tu kama unavyosema lazima mtu atambuliwe utendaji wake.Kama atakuwa anachagua na kutojua utendaji wake ndio matatizo yanapokuja.Atakuwa anabadili mawaziri kila siku kwakuwa hana taarifa zao za utendaji.

Ni vizuri kuchukua Watanzania walio majuu lakini lazima nao waje nyumbani kabla hawajawa mawaziri na wajue nini chakufanya.Ni kitu kizuru kwani watahamisha ule ujuzi wa nje walioupata na uzoefu wao lakini wanatakiwa wajue mazingira ya kwetu kkwani mazingira ya nje na ya huku si sawa.Wajue wapi watawekeza na nini chakufanya.

Na ndio hapa naona umuhimu wa kitu kinachoitwa socialization na Recruitment hasa kwa vijana wadogo.Tungekuwa na pool ya recruitment hya mambo yangekuwa mpeto tu kwani hazina ya watu wenye mwelekeo upo.
Nawasilisha
 
Kumbe I was right, Kawambwa ni anko! Ahsante Domo Kaya wewe ninakuamnia sana, vipi kulikoni siku hizi huopnekani mkuu?

Field Marshall ES;

Mwamini jamaa kadiri unavyoweza lakini those gentlemen are not genetically related!
 
Anko Kikwete na mimi naomba wizara jamani, mbona Anko Shukuru Kawabwa kwa muda wa miaka miwili na nusu tu ameshazunguka wizara 4???? Je kwani unampango wa kumpa uwaziri mkuu??????? maana hizo mbio si bure lazima unampango nae mkubwa zaid.


Aaaaaah umejuaje...?! Kauka basi usiseme sana kwa sasa maana utamchanganya Mheshimiwa Pinda!
 
HAM, Binafsi napingana sana na haya maswala la kutazam degree ikiwa mtu huyo hajawahi kufanya kitu ama mabadiliko yoyote ktk system ambayo ni mbovu..
Hawa na elimu zao huendelea kumtumia punda aliyechoka. Elimu nzuri ni pale unapoleta changes ktk wizara yoyote ile na wananchi wakaweza kuiona.
Hawa wasomi wetu wapo katika sinia moja na sisi ktk vumbi la kisomo cha arobaini..Elimu waliyopata ni elimu ya kuiga hwengi wao wanashindwa kuitumia ktk sinia hili zaidi ya kujumuika nasi na kuzivua hizo Phd zao..
sana sana watakuja tuibia tu kisha heshima tulizokuwa tukiwapa zitaondoka...
 
Hawa wasomi wetu wapo katika sinia moja na sisi ktk vumbi la kisomo cha arobaini..Elimu waliyopata ni elimu ya kuiga hwengi wao wanashindwa kuitumia ktk sinia hili zaidi ya kujumuika nasi na kuzivua hizo Phd zao..
sana sana watakuja tuibia tu kisha heshima tulizokuwa tukiwapa zitaondoka...

Mzee Mkandara umenifurahisha sana na haya maneno yako niliyobold, yamenikumbusha maneno ya mzee Mandela katika kitabu chake "Long Walk to Freedom", alipokuwa anasimulia walipokamatwa yeye na viongozi wenzake wa ANC mwaka wa 1963. Mandela anasimulia kuwa aliwaheshimu sana wenzake hao kwa jinsi walivyokuwa watanashati kuliko yeye, lakini walipovuliwa nguo na kulazimishwa kubaki uchi, anadai alifanya jitihada za ziada kujizuia kucheka alipowaona wenzie walivyo, kumbe ati ule utanashati wao ni nguo tu, akaandika kitabuni mwake "clothes make the man!"

Ni kweli kuna watu wana PhD katika fani zao, lakini wakipewa majukumu yaayohitaji elimu hizo huwa wanazivua hizo PhD na kufanya madudu kuliko hata wale wasio na elimu, ambao hatimaye huishia kusema "kumbe hatuchekani!" Yaani utakuta lijamaa na PhD yake linasalandia kujichotea pesa zilizoletwa kusaidia wenye UKIMWI, ili naye aendeshe gari zuri kwa kuwa hata "wasioenda shule" wana magari mazuri kuliko yeye! Anavua PhD na kuingia kwenye mkumbo wa kughushi stakabadhi na malipo bandia sawa tu na wanavyofanya hao anaoita "hawajaenda shule"! Mfano mwingine wa wazi kabisa, ona Profesa wa sheria alivyohangaika kughushi stakabadhi na mkataba wa mauzo ya nyumba huko Italia, ili naye ajipatieko "vijisenti"! Mbele ya "vijisenti" watu wanavua sio PhD tu, hadi kile cheti cha darasa la saba mtu anakivua anabakia kama "ngumbaru", yaani ni kama kusema "unyama unyama tu", na twajua kwa hakika wanyama huwa hawana vyeti vya elimu!
 

Nilipoona MSOLLA nikakukumbuka, sasa nadhani kuna umuhimu wa kuandaa DOSSIER KAMILI la kumuondoa

kuna namna mbili

ya kwanza ni kufanya PETITION online kisha tutalisambaza kwa kila Mtanzania mwenye e-mail

ya pili ni KUTAFUTA CD ziote zinanzomhusu kisha tutazilepleka kule WIKI LEAK,EU na kwingineko kisha tuangalie upepo unaendaje

ikishndikana tunaingia kule kwenye mambo yake Private...ndio huyu ni public figure hivyo hawezi kuwa immune na lazima atakuwa na skeletons in his closet



Mkubwa shukrani..hii ndio kasi mpya ninayoitaka mie na wachovu wenzangu wengi huku newala..Thanks once again..
 
Dua,
Ahsante rafiki yangu. NIlikuwa Bongo kwa shughuli za kibinafsi. Unajua tena internet za Bongo unalipa shilingi alfu moja mia saba kwa saa moja. Haikunipa muda mzuri wa kuchangia. Lakini nilipata fursa ya kukutana na wana JF kibao.

Mkubwa, i will be heading there soon, for a research work and would like to meet some of the JF comrades pia..Hope you enjoyed the rainy season..
 
Mwamini jamaa kadiri unavyoweza lakini those gentlemen are not genetically related!

Ninaziaminia source zangu zote mkuu, ikiwa ni pamoja na huyu mkuu Domo Kaya, kuwa jamaa ni anko, labda sasa kazi kwako ndugu yangu either usuke au unyoe, na wewe ungekuwa unamjua Domo Kaya ni nani usingerusha hizi nyepesi nyepesi!

Nasikia mkuu sasa anko anaelekea kwenye u-PM, Pinda ni geresha tu!
 
Ningependa kupata maoni ya watu wanaomjua Kawambwa kutokea UDSM, na hizo wizara alizopitia...kuhusu utendaji wake.

Au ana kazi maalum ya JK ya kukagua wizara kujua utendaji wa mawaziri watendaji wengine wakuu kwa kupitia nyaraka na kunusa ufisadi wao nk?
 
Back
Top Bottom