Hapa kuna matatizo sana.
Black Panthers wanatakiwa wawe cast wawili. Kuna mkubwa ambaye atakuwa ni variant kwenye hizi storyline za multiverse, na kuna mdogo, yule Toissant mtoto wa T'Challa, ambaye wanataka wamuweke akiwa mkubwa(miaka 10 zaidi)
Kuhusu huyo mdogo, hakuna taarifa zimetoka.
Kuhusu huyo mkubwa, waigizaji wanakataa hiyo role. Damson Idris ameikataa. John Boyega ameikataa, David Oyelowo amaeikataa.
Inasemekana wanaikataa kwasababu wamegundua waigizaji weusi wanafuatiliwa sana wakiwa kwenye roles kubwa, kwahiyo linaweza kuwatokea lile lililomtokea Jonathan Majors na role yake ya Kang.
Damson Idris ni wa moto sana siku hizi, alitaka kuchukua role ya John Stewart DC, sema Aaron Pierre akaipata. Anaona kama kuigiza role ndogo ya kuwa variant hakumtoshi.
John Boyega anasita sita kufanya kazi na disney, kuna role aliicheza kwa ajili ya disney wakashindwana.
David Oyewolo amekatataa vikali, amesema haiwezi legacy ya Chadwick Boseman.
Actors wawili waliowahi kusema wangependa kuigiza black panther ni Aldris Hodge, na Y'lan Noel.
Mashabiki wanampendelea Aldris Hodge kwasababu ya jinsi alivyoigiza Hawkman kwenye Black Adam.