Next president of Kenya without a doubt

Next president of Kenya without a doubt

Kwani wewe ni gani inatawala uko kwenyu? Usiikatae leo kesho ukasema ndio. Umeona sisi nachangia politcs senu?
Tengeneza jamvi la wakenya tu hapa toka kama hautaki wengine wachangie politics za kwenye wakati hata mambo ya kwenye bible na Qur'an tunajadili hapa
Kwani wewe ni gani inatawala uko kwenyu? Usiikatae leo kesho ukasema ndio. Umeona sisi nachangia politcs senu?
 
Hawa NASA walifaa kuweka tamaa zao pembeni na wawe wazalendo, kwamba waishie kuwa na mgombea wa urais na makamu wake basi, sasa wameishia kutengeneza wadhifa wa waziri mkuu kinyemela na nyadhifa zingine za ovyo ili kila mmoja anyofoe vya kwake.

Ningewaona wa maana sana kama kweli wangeishia kuwa na mtu mmoja afuate urais na makamu wake, wengine wahusike katika kumpigia debe mgombezi. Sasa hizo nyadhifa wanazozitengeneza hazipo hata kwenye katiba, eti wameahidiana kwamba baada ya ushindi watabadilisha katiba ili wapeane hizo nyadhifa. Yaani katiba ya nchi ya watu zaidi ya milioni 40 ibadilishwe kuwafurahisha watu wawili.

Halafu baada ya hapo itakua ni uongozi wa vurugu tupu, maana tutakua na four centres of power, kila mmoja atakua anatoa tamko na kupingwa na mwengine. Nikikumbuka jinsi Kibaki na Raila walivyotuzingua kwa walivyokua wanaburuzana, yaani nahisi huruma kwa nchi yangu ikitokea hawa watashinda.
 
Uhuru anaweza kushinda. Ingawa wataenda round ya 2 na Raila

Unajuaje ni Raila ndiye atakayechuana na UhuruRuto? Kwani upinzani mpaka sasa hawaeleweki yaani wameshindwa kumpendekeza mmoja wao, sasa kama wameshindwa ni wazi hapo umoja wao ushasambararika ni Uhuru kama kawa atashika dola yaani Jubilee!!!! Kwani hiyo ni afadhali Abaluhya na Gusii washikane na Uhuru ili angaa wapate nafasi za uongozi serikalini kuliko kubaki kucheza rumba na sarakasi barabarani/majukwaani. Mhe Eugene Wamalwa kacheza vizuri.
 
Kalonzo msiyoka namkubali kuliko mwanasiasa yeyote Yule kenya

Nilikuwa amkubal gorge saitot ila wakenya wakamuua
 
Ndo nani huyo? Na anatoka Kundi gani? Kalenjin, Mjaluo au Pokot?
Anaitwa Kalonzo Musyoka,rafiki wa karibu wa Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu,wa term ya mwisho ya Rais Kibaki.

Kabila lake ni Mkamba.Jina lake aka Almaarufu kama "Watermelon".Ni miongoni mwa vigogo wanne wa NASA,muungano wa wapinzani.Uchaguzi uliopita alikuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga.
 
This time sidhani kama tutapata mshindi in the first round.
Uhuru anaweza kuibuka mshindi ila kufikisha 50% itakuwa vigumu.
Yule atakuwa wa pili 1st round, atakuwa mshindi 2nd round.
Huu ni mtazamo wangu kibinafsi
Hivi do you believe UHURU alishinda uchaguzi uliopita?
 
Back
Top Bottom