Neymar Jr. ataweza kurudi na uwezo wake wa zamani?

Neymar Jr. ataweza kurudi na uwezo wake wa zamani?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Itakumbukwa kuwa Mwaka 2023 Mwezi wa 9, Mshambuliaji wa The Al-Hilal ya Saudi Arabia, Neymar JR alipata majeraha kwenye Goti ambayo yanamfanya kukaa nje ya Uwanja kwa Muda wa Miezi 6-12

Majeraha haya ya goti yatamfanya Neyma JR kukosa Michuano ya Copa America 2024 inayo tarajia kuanza June 2024.

Mimi ni mmoja ya mashabiki wake wakubwa Katika mpira wa miguu kutokana na Uwezo wake na Ufundi alio kuwa nao. Lakini Binafsi naona Mambo yamebadirika kwa Neymar JR Kitu kinacho nipa Mashaka kuona kama NEYMAR JR anaweza Kurudi kwenye Ubora wake ambao tumemzoea

Neyma Ameongozeka Uzito na amekuwa mnene sanaa ukilinganisha na zamani. Sote tunafahamu changamoto kubwa katika kupunguza Unene na kufanya urudi katika hali yako ya Kawaida. Je, Neymar JR Tutegemee nini Toka kwake?

PICHA ZA SASA
IMG_5948.jpg

IMG_5947.jpg


Linganisha na PICHA ZA ZAMANI

IMG_5949.jpg

IMG_5950.jpg
 
Atunze pesa za kustaafu sasa. Nazario de lima kama sio ugonjwa wake wa hypothyroidism uliomfanya aongezeke unene kupita kiasi basi angekiwasha sana ktk ulimwengu wa soka. Cristiano Ronaldo alipata mshauri mzuri sana aliyembadili kutoka winger mkokotaji wa mpira kuwa mfumania nyavu. Hii hali ilimuwezesha kuepuka sana majeraha kwani hahitaji kukimbia sana uwanjani anachofanya ni kukaa kwenye nafasi akisubiri mpira umfate
 
Yes Neymar ni mchezaji wa kawaida mwenye kipaji kikubwa. Ukawaida umekuja kutokana na kuandamwa na majeraha lakini pia ana bahati mbaya kuwa kwenye kizazi kimoja na kina CR7 na Messi
 
Yes Neymar ni mchezaji wa kawaida mwenye kipaji kikubwa. Ukawaida umekuja kutokana na kuandamwa na majeraha lakini pia ana bahati mbaya kuwa kwenye kizazi kimoja na kina CR7 na Messi
 
Ni mchezaji mzuri mno ila aina ya uchezaji wake wa kukaa na mpira muda mrefu ndo unamponza,

Sitosahau Fifa club world cup akiichezea (Santos Fc) alivyomgaragaza Faza Puyol wa (Barcelona) kwa machenga, mpaka baad ya mechi Ikabidi Rais wa Barcelona aanze mchakato mzima wa kumleta neymar barca..... The rest is history sina deni nae.
 
Back
Top Bottom