NeyMaR kwa kila Sekunde anaingiza 15k+ Tsh

Sir_Finus

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
330
Reaction score
139
kwa mahesabu ya kawaida kabisa Kijana wa kibrazil umri wa miaka 25 kwa sasa tangu asajiliwe na PSG anaingiza kiasi cha 1.6B Tsh kwa wiki
kwa hiyo kwa siku anaingiza 220m Tsh (imekuwa rounded off)
kwa saa moja 9m
na kwa kila dakika ni 152,000/= Tsh
na kila sekunde ni rounded kama 2,500/= Tsh
Kwa hiyo kila sekunde anakula mwekundu na nusu kwa muda wa miaka mitano ya mkataba wake pale PSG...
Nawaza kwa mbali mtanzania ukiwa unakula hii kandarasi ni kipi utafanya...
MIMI NANUNUA BOMBADIER NISHINDANE NA MKULU, HALAFU NAFUNGUA MRADI WA MAHOSTELI PEMBENI YA YALE YA MKULU NA ANZISHA PROJECT YA TRENI YA UMEME KUELEKEA KENYA (JOKES)
ILA HUU MSHIKO MREFU SANA...
ACHA TUISHIE KUUANDIKA TU..

MTANZANIA MATAWI
Mwezi: 5,000,000/= Hapa unafanya BOT au Taasisi inayolipa poa
Siku: 167,000/=
Saa: 6,900/=
Dakika: 115/=
Sekunde: 1.9/=

Shilingi yako moja kwa sekunde na bado unatuwekea tinted mtaa na Range lazima upite nayo kutumwagia maji machafu na hata mambo yetu huksanyiki nasi..
vipi ukipata buku 2 jero

MODERATOR NAOMBA MMBADILISHE TITLE MUWEKE 2,500 SIO 15k
 
Ndio maisha mkuu wangu!! hiyo pesa yake ya wiki ndio pesa ambayo wizara ya kilimo ilipewa kwa mwaka jana!!
Ha ha haaa ni baada ya kupga mchinjo na kuwapa asilimia 3 halaf bdo ya mwaka huu tumeipgia makofi na kura za ndiooo...
Kweli ndo maisha kuelekea kwny uchumi wa viwanda bila kujali kilimo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nani alikuambia anayefanya kazi B.0.T ndio anapata mshahara huo,kwa taasisi yoyote ya serikali iliyopo Tanzania kupata mshahara huo lazima uwe kwenye ajira angalau Miaka 5-10 nakuendelea.
 
Mi ningekuwa nalipwa izo ningepangisha room state napaa asubuhi narud jion

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Duh hatari!! Huwa Najiuliza hivi hizo pesa ni za kawaida kama hizi zetu tunazodunduliza kwenye kibubu miaka mitatu zitoshe kununua kiji uwanja cha 10*10 kwa mrombo? Hizo hela zikiletwa huku zitafaa kutumia?
Mkuu kiuchumi ni kawaida,kadri kipato kinavyoongeza matumizi nayo huongezeka
 
Sijui hisabati ulisomea wapi?
Tangu lini dakika ikawa na sekunde 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchambuzi wako wa hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui hisabati ulisomea wapi?
Tangu lini dakika ikawa na sekunde 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
Halaf ujue kweli eti...
Tatizo nimeanza kutumia calculator alvel 2008 mpaka chuo..
Ni kweli aise nimepoteana mkuu..
Kwa hyo jamaa kwa sekunde anapokea parefu zaid kama buku 25 hivii...
Wewe umebutukia...
Wengine wanaweza pita dara..
Asante mkuu ngoja ni edit uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sir_Finus Mkuu hizo pesa ni za kawaida ulisha wahi kujiuliza Tajiri wa kwanza wa dunia hela zake anafanyia nini huku ukiangalia huyo neymar hata Top 500 ya matajiri wa dunia hayumo
Sio pesa ya kawaida, Neymar ameajiriwa na hapo amezungumzia mshahara, labda tutajie hao matajiri wanaowalipa huo mshahara wafanyakzi wao ndio tuwafananishe na Neymar. Maboss wa PSG ndio wafananishe na hao matajiri.
 
Sio pesa ya kawaida, Neymar ameajiriwa na hapo amezungumzia mshahara, labda tutajie hao matajiri wanaowalipa huo mshahara wafanyakzi wao ndio tuwafananishe na Neymar. Maboss wa PSG ndio wafananishe na hao matajiri.
Mkuu nikukutajia watu wote walioajiriwa na ambao wanamzidi neymar mshahara ni sawa na kupoteza muda wangu maana ni wengi sana-ila kwa ufafanuzi rahisi ni kuwa matajiri wote ambao wapo juu ya matajiri (mabosi) wa neymar wameajiri watu ambao wengi wana mzidi huyo neymar mara 100 ya mshahara wake.wewe ungesema kwa upande wa celebrities hapo neymar ungekuwemo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…