Neymar yuko fiti kukipiga kombe la dunia, atangaza vita

Neymar yuko fiti kukipiga kombe la dunia, atangaza vita

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Neymar.jpg

Mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar Jr amesema yuko fiti kucheza fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza Juni 14 nchini Russia bila kikwazo chochote.

Neymar ametoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya timu hiyo kuweka kambi jijini London Uingereza kujiandaa kwa fainali hizo.

Neymar amesema ana uhakika wa kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Uswis Juni 17. “Niko tayari kucheza, hakuna kitu cha kunizuia,” alisema mchezaji huyo ambaye hajacheza muda mrefu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

Hata hivyo, benchi la ufundi limejaribu kupunguza presha kwa nyota huyo kwa kuwa anahitaji muda kurejea katika kiwango bora tayari kwa fainali hizo.

Chanzo: EATV
 
manenooo meeeeengiii sidhani kama ataisaidia timu yake kwa aina ile ya mchezo ya kutaka kushoot kila mpira golini peke yake.
 
Ramos is watching ............
 
manenooo meeeeengiii sidhani kama ataisaidia timu yake kwa aina ile ya mchezo ya kutaka kushoot kila mpira golini peke yake.
Neymar akiwa timu ya Taifa anakuwa mtu mwingine kabisa
 
Back
Top Bottom