Kwanza kabisa nimefurahi sana hawa jamaa wamepiga mzinga😀😀 Disney mjanja sana anataka yeye ndio abaki kua Tycoon wa kutengeneza na kusambaza filamu. Kila Kampuni ikijitokeza inatengeneza muvi akiona ni kali anainunua inakua Kampuni mwenza! Kachukua Lucas film (watengenezaji wa star wars movies)Pixar Animation, Marvel Studios (kama msambazaji), 20Century Fox.
Kwenye sakata lake la mwaka jana kati yake na Kampuni ya Sony juu ya muvi za Spiderman aliona sony anazingua akasema anataka anunue kampuni yote kabisa. Sony wakakaa chini kusort out term zao.
Kila muvi wanayotoa wanapiga hela mnoo, hata kama muvi mbaya ilimradi inatoka Disney motion picture basi inapiga hela. Hatimaye sasa wamepiga loss kwenye muvi ya Mulan. Kama unampango wa kuicheki nakushauri hata usiangakie hii muvi itakupotezea muda. Stori ya kawaida pia matukio na mapigano yaleyale wala hata sio mazuri japo kuna waigizaji wakali kama Don yen na Jet Li. Naona ndio maana hata nusu ya bajeti waliyotumia haijaridi, safi kabisa nao waonje machungu (roho ya kimaskini hii)
Kama ulitaka kuangalia muvi zenye mandhari ya kichina wala usisumbuke kuitazama hiyo Mulan japo imepewa promo sana. Jaribu kuangalia hizi muvi.
View attachment 1584602
1.Nezha
Hii ni animation, lakini ni muvi nzuri sana sana na mapigano yake yanavuti. sema tu haijatoka hollywood ingekua imetoka disney ingefikisha mauzo ya Billion+ imefikisha 700M$ tu.
Muvi inahusu mtoto aitwae Nezha, stori inaanza Suprme lord (mungu wa kichina) anatenganisha roho yenye nguvu ya ubaya na wema. Roho ya wema ilitakiwa iende kwa mtoto wa kiongozi wa mjii fulani ili watumie kujilinda na ushetani. Roho ya ubaya mtoto ambaye angeipata basi angeishi kwa miaka mitatu tu baada ya miaka mitatu mungu angeshusha radi kubwa na kumuua.
Mambo yakavurugika sasa roho ya ubaya ikaenda kwa mtoto wa huyo kiongozi ambae alitakiwa awe mwema ile roho ya wema yenye nguvu kubwa zaidi wakala wa mashetani akaichukua akaipeleka kwa mtito wa mashetani (Dragons) waliokuwa wamefungwa na monyororo chini ya ardhi. Ilitakiwa huyo mtoto wa mashetani (jina lake Ao bing) atumie nguvu zake hizo kuwafungua baba zake/mashetani kutoka huko kuzimu.
Sasa ikawa vice versa yule dogo huko duniani (Nezha) akawa ni mtu wa vurugu hada mji mzima wakimuona wanakimbia anapiga mkono balaa. Kule kwa aobing baba zake wanamfunza awe mtenda mabaya lakini hawezi anapenda kutenda mema. Mwisho wa siku Nezha na Ao bing wanakutana zinachapwa ngumi hatari maana nezha anataka kuteketeza mji kwa kua wanamchukia ila Aobing anamziwia kwamba they are innocent.
At the end wanapatana wema unashinda ubaya, nezha anatakiwa apigwe na radi kama mungu alivyosema ila Aobing anamsadia kuziwia radi.
October 1 mwaka huu unatoka mwendelezo wake I'm so excited kuona kitakachoendelea maana kule kuzimu demons waliweza kukata monyororo
Lesson. Uovu unaondolewa kwa upendo sio kwa chuki dogo alikua anazidi kua mwovu kwakua walikua wanamchukia wanamuona ni demon.
View attachment 1584605
2.
Rise of the legend
Wong fei hong kijana yatima wa mtaani anaungana na mayatima wenzake kumpindua kiongozi wa kundi la kigaidi na biashara haramu aitwae Master lei (Samo Hong). Samo Hong akikaa nasfi ya ugaidi utamchukia maana mafia kweli. So fei anaenda kuomba kazi kwa master lei, Master lei anatoa agizo kwamba mtu atakemletea kichwa cha hasimu wake wa biashara basi atakua mwanae wa kuasili/adopted son.
Fei anashinda anafanywa kua moja ya watoto wa master lei kumbuka ameingia huko kwa mkakati maalumu. Mwisho wa siku wanshinda kumaliza kundi lote la master lei
View attachment 1584606
3. Jin yi wei
Kacheza Don yen maarufu kama 14 blade